Waziri
wa Mkuu Mizengo Pinda, amevunja ukimya na kuamua kutangaza nia yake ya
kutaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Pinda
alitangaza nia hiyo juzi usiku Ikulu ndogo ya Mwanza jijini Mwanza,
mara baada ya kuwaalika wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) toka mikoa sita ya Kanda ya Ziwa.
Habari
kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika zilieleza kuwa Waziri mkuu aliwaalika
wajumbe tisa kutoka katika wilaya zote za mikoa ya Mara, Mwanza,
Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera.
Pinda
aliyekuwapo jijini Mwanza kwa ajili ya kuendesha harambee ya Mfuko wa
Taasisi ya Benjamin Mkapa iliyofanyika jana usiku, alikutana kwa
‘mafungu’ na wajumbe zaidi ya 50 kutoka Mara, baadhi toka Mwanza, Geita
na Kagera.
“Wajumbe
wengine wa Shinyanga, Simiyu na wale Mwanza na Geita alikutana nao jana
(juzi) jioni ili kuwashawishi wamuunge mkono baada ya jina lake
kupitishwa na NEC,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo
hicho kilisema wajumbe toka wilaya hizo za Kanda ya Ziwa, walianza
kuwasili Ijumaa mchana jijini Mwanza kwa lengo la kuitikia wito wa
Waziri Mkuu kabla ya hawajatangaziwa nia yake.
SABABU ZA KUTANGAZA NIA
Waziri
Pinda aliwaeleza wajumbe hao sababu kubwa zilizomfanya aguswe kutangaza
kuwania nafasi ya Rais 2015, ni kutokana na ushawishi mkubwa toka kwa
maaskofu, masheikh, baadhi ya wabunge, watu maarufu pamoja na mke wake.
“Sikuwa
na nia hiyo kwa vipindi vyote vitatu vya ubunge wangu, lakini watu hao
akiwamo mke wangu, nimeshawishika kutaka nafasi hiyo,” alisema Pinda.
Alisema ameona hana sababu ya ‘kuzembea’ kutangaza nia ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao.
SIFA
“Ninazo
sifa za kunitosheleza kuwania nafasi hii, ikiwamo kutokuwa fisadi, pia
nimekuwa ndani ya viongozi wa nchi wa awamu zote nne tangu 1974 enzi za
Nyerere (Julius), Ali Hassan Mwinyi, Mkapa (Benjamin) na sasa Kikwete,” alidai.
Aidha,
alisema kutokana sifa hizo hataweza kuchangishiwa pesa za kuingia
madarakani kama wengine (hakuwataja), bali atawapa kiasi alichonacho ili
kuwawezesha kumsaidia.
Pinda maarufu kama “mtoto wa mkulima”, alidai anaamini viongozi wakuu waliopita madarakani na kuongoza nchi, wanamuunga mkono.
VIKAO VYA CHAMA
Kutokana
na nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya Maadili, Kamati Kuu na
Halmashauri Kuu ana uhakika jina lake halitaweza kukatwa na litafikishwa
katika mkutano mkuu wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama.
“Kama
wajumbe wa mkutano mkuu, mjiandae ‘kunibeba’ kwani kati ya majina
matano yatakayotajwa na kamati kuu, nitakuwamo na pia na kati ya matatu
pia nimo…nguvu zenu ni katika mkutano mkuu.”
Ilielezwa
kati ya majina matano ambayo yatapelekwa Kamati Kuu, moja ni la Pinda,
mwanamke, kijana, mgombea toka Visiwani na waziri mkuu mstaafu, Edward
Lowassa.
Hata
hivyo, hofu ya Pinda ilielezwa ni baadhi ya wajumbe walioalikwa kuwa
miongoni mwa wapiga debe wa baadhi ya walionyesha nia ya kugombea nafasi
hiyo akiwamo Lowassa.
Aidha,
habari toka ndani ya kikao hicho zilidai, wajumbe walioalikwa
kuhudhuria mkutano huo waligoma kupokea mgawo wa Sh. 50,000 zilizotolewa
baada ya kumalizika kwa kikao.
NAPE
Uamuzi
huo wa Waziri Mkuu kutangaza nia unaenda kinyume na chama chake ambacho
hivi karibuni kiliwafunga ‘midomo’ wanachama wake kutangaza nia hiyo
kabla ya muda akiwamo Lowassa, Bernad Membe na Frederick Sumaye.
Juhudi
za NIPASHE kumpata Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuzungumzia
‘nia’ hiyo ya Pinda, zilishindikana kutokana na simu yake ya mkononi
kutopatikana.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >



