Kiongozi
wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kwa mara ya kwanza ametabiri
hatima ya maisha yake duniani akisema kuwa anaamini Mungu anaweza kumpa
muda wa miaka miwili au mitatu ya kuishi.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akitoka ziarani Korea Kusini
kurejea Vatican, Papa Francis alisema suala la kuendelea kuishi ni
neema ya Mungu.
“Suala
hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu kutafakari
kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua kwa sababu
hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu nitakuwa
nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba,” alisema.
Papa Francis (77), pia alizungumzia uwezekano wa kustaafu endapo atahisi kwamba afya yake hairuhusu kuendelea na kazi.
Utamaduni
wa kuachia madaraka ndani ya kanisa hilo linalotajwa kuwa na waumini
wengi duniani uliasisiwa upya mwaka jana na mtangulizi wake, Papa
Benedict XVI aliyeng’atuka kutokana na matatizo ya kiafya.
Pamoja
na kwamba Papa Francis hajawahi kuzungumza hadharani kuhusu ni lini
pengine anaweza kufariki dunia, lakini baadhi ya vyanzo vya habari
kutoka Vatican vinasema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwaambia watu wake
wa karibu kuhusu siku zake chache zilizosalia duniani.
Wachambuzi wa masuala ya kiimani kwa nyakati tofauti walisema huenda kiongozi huyo ana tatizo la kiafya ambalo halijawekwa wazi.
Wakati
hayo yakiendelea taarifa za ndani zinabainisha kwamba kiongozi huyo
aliwahi kutolewa pafu moja baada ya kuathirika wakati akiwa kijana
nchini Argentina.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >



