Na Gladness Mallya
Mke wa mkongwe wa Nyimbo za Injili Bongo,
Rev. Cosmas Chidumule aliyejitambulisha kwa jina la Cesilia Maiko na
wanaye, wanadai kutelekezwa na staa huyo huku mama huyo akiandamwa na
maradhi ya kisukari.
Mke wa mkongwe wa Nyimbo za Injili Bongo, Rev. Cosmas Chidumule anayetambulika kwa jina la Cesilia Maiko.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni jirani wa familia hiyo,
Chidumule aliyewahi kutamba na Wimbo wa Yesu ni Bwana, alidaiwa kutoweka
nyumbani kwake kwa muda mrefu hivyo kuiacha familia kwenye maisha
magumu na wakati mwingine kukosa hata chakula.Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alifika nyumbani kwa Chidumule maeneo ya Kinondoni B, Dar, mwanzoni mwa wiki hii ambapo alishuhudia hali halisi ya nyumbani hapo na hakumkuta Chidumule ila alifanikiwa kuzungumza na mkewe.
Akizungumza kwa huzuni huku akibubujikwa na machozi, mke wa Chidumule, Cesilia alisema wameishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka 36 na wamejaliwa kuwa na watoto wanne lakini mmoja Mungu alimpenda zaidi hivyo ni marehemu.
Aliendelea kusimulia kwa uchungu kwamba,
mwaka 2000, aliugua ambapo mumewe Chidumule alimpeleka Hospitali ya
Taifa Muhimbili na kugundulika kuwa ana ugonjwa wa kisukari.
“Baadaye mume wangu alianza kuaga nyumbani kuwa anakwenda kwenye huduma, akawa anakaa huko wiki mbili bila kuniuliza naendeleaje na familia kabla ya kuamua kuondoka moja kwa moja.
“Ukweli ninateseka na sina msaada wowote kwani wanangu hawana kazi, ninatakiwa kwenda hospitali kila mara lakini wakati mwingine nakosa fedha.
“Wakati mwingine tunakosa hata chakula kwa kuwa sina nguvu tena ya
kufanya kazi. Naomba msaada kwa Watanzania wenzangu kwani nateseka sana.“Baadaye mume wangu alianza kuaga nyumbani kuwa anakwenda kwenye huduma, akawa anakaa huko wiki mbili bila kuniuliza naendeleaje na familia kabla ya kuamua kuondoka moja kwa moja.
“Ukweli ninateseka na sina msaada wowote kwani wanangu hawana kazi, ninatakiwa kwenda hospitali kila mara lakini wakati mwingine nakosa fedha.
“Ni miezi mitatu sasa, Chidumule hajakanyaga hapa nyumbani (Kinondoni B) na aliondoka tangu tulipomaliza msiba wa mtoto wetu, amenishtaki Ustawi wa Jamii ambapo niliitwa lakini waligundua sina kosa ndipo akaambiwa kama vipi aende mahakamani hivyo ndiyo nasubiri kuitwa mahakamani (bila kutaja kosa),” alisema huku akiangua kilio.
Jitihada za kumpata Chidumule ziligonga mwamba kwani simu yake ya kiganjani haikuwa hewani muda wote hivyo jitihada zinaendelea.
Kama umeguswa na habari hii na ungehitaji kumchangia mama huyu chochote ulichonacho, wasiliana naye kwa namba 0653 117535.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >