mat
Tukisema
dunia imekwisha,tutakuwa hatujafanya makosa maana matukio ya utesaji,
unyayasaji na ukatili kwa watoto wachanga yamekuwa yakichukua kasi
kubwa ndani ya jamii.
Mtuhumiwa Bhoke Steven (21) anayedaiwa kumfungia ndani mwanaye anayejulikana kwa jina la Steven Amos (miezi 10).
Hivi
karibuni mama mmoja, Bhoke Steven (21) (pichani), mkazi wa Kitunda,
wilayani Ilala, Dar es Salaam amejikuta matatani baada ya kudaiwa
kumfungia ndani mwanaye aliyejulikana kwa jina la Steven Amos (miezi
10).
Majirani
wa mama huyo ambao waliomba majina yao kutoandikwa gazetini, walidai
kuwa mama huyo alikuwa na tabia ya kumfungia ndani mtoto wake huyo na
yeye kutokomea kusikojulikana na amekuwa akifanya hivyo kwa zaidi ya
mwezi mmoja.
“Baada
ya kuona tabia hii imekithiri tuliamua kuwatafuta wazazi wa mwanamke
huyo kwani tuliona anaweza kusababisha kifo kwa mtoto huyo kwani
akiachwa huwa analia sana,” alisema shuhuda mmoja.
Bibi wa mtoto Steven Amos (miezi 10).
Alisema
baada ya kuwapata wazazi wa mama huyo walimkabidhi mtoto huyo na mama
akamtafuta mwanaume aliyezaa naye ambaye alimsaka mama wa mtoto huyo
wakamkuta Temeke ‘akiponda’ raha, akashauriwa arejee nyumbani,
akakubali.
Mama
huyo baada ya kurudi nyumbani kwake wananchi wenye hasira walimkamata
na kumfikisha Kituo cha Polisi Kitunda kisha akahamishiwa Kituo cha
Wilaya ya Kipolisi cha Ukonga, Sitakishari ambapo ametiwa mbaroni.
Mama
huyo alipohojiwa na mwandishi wetu wakati anapelekwa polisi kuhusu
sakata hilo, alikiri kutoweka nyumbani na kumuacha mtoto.“Ni kweli,
nilimuacha mtoto kwa kuwa hakuna msaada wowote ninaopata, hivyo
nikatoweka na sikuwa na makazi maalum,” alisema Bhoke.
Wakati
huohuo, mtu asiyejulika amemtelekeza mtoto anayekadiriwa kuwa na miezi
tisa maeneo ya Majumba Sita, Ukonga jijini Dar es Salaam na tukio hilo
limefikishwa Kituo cha Polisi, Stakishari.
Mtoto (jina halikufahamika) akiwa kituo cha polisi Stakishari Wilaya ya Ukonga baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi maeneo ya Gongo la Mboto.
Pia
mtoto mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita alifikishwa
katika Kituo Kidogo cha Polisi Gongo la Mboto, baadaye akahamishiwa
Kituo cha Stakishari baada ya kutelekezwa na mtu aliyekuwa naye .
Habari zinasema mtoto huyo amepelekwa Hospitali ya Amana na amelazwa
wodi namba moja kwa uchunguzi zaidi.Afisa mmoja wa polisi ambaye alidai
siyo msemaji amethibitisha kutokea kwa matukio hayo.