BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Simba huyo aliwaelekeza walinzi hadi katika mzoga wa mamake
Mtoto wa simba aliwaongoza askari wa kulinda wanyama kwenda ulipo mwili wa mamayake ambaye alikuwa ameuawa katika mbuga moja ya kuhifadhi wanyama nchini India, kitendo ambacho maafisa wa wanyama pori wanakilelezea kuwa si cha kawaida.
Askari
wa wanyama pori ambaye alimwona mtoto wa Simba akijificha vichakani,
alimfuata na kugundua mwili wa Simba aliyeuawa katika kilima jirani.
Mtoto
huyo wa simba aliulinda mwili wa mama yake hadi pale mlinzi wa wanyama
pori aliporudi na maafisa wa wanyama pori na polisi kuondoa mzoga huo.
Uchunguzi
uliofanyiwa mwili wa simba huyo ulibainisha kuwa alikufa katika
mapigano na wanyama wengine huenda aliuawa na kundi la nyati.
Naibu mhifadhi wa Misitu katika eneo la Gir, Anshuman Sharma, amesema tabia yasimba
huyo mtoto ni nadra kutokea na ni cha aina yake, kitu ambacho hajawahi
kushuhudia katika miaka yake mingi ya kufuatilia tabia za simba.
Gir katika jimbo la Gujarat ni mahali wanapopatikana kwa wingi simba wa Asia na kwa mujibu wa sense ya wanyama iliyofanyika mwaka 2010, kuna simba 411 katika mbuga hiyo.
"Jumamosi
mchana, nilikuwa nafanya doria katika hifadhi ya Tulsi-Shyam
nilipomwona mtoto wa simba akichificha katika vichaka,"mlinzi wa msitu
Rana Mori ameiambia BBC.
''Watoto wa Simba huambatana na mama zao''
Watoto
wadogo wa simba nadra kuwakuta peke yao , kwa ujumla wanafuatana na
mama zao na Bwana Mori anasema alianza kumtafuta mama ya simba huyo
mtoto.
"Nilimfuatilia
mtoto wa simba ambaye aliniongoza hadi kwenye mwili wa mama yake
uliokuwa umelala katika kilima kidogo. Simba huyo jike aliitwa Rupa
[likiwa na maana ya Mzuri].Kwanza alionekana kama aliyelala usingizi,
lakini wakati hatikisiki, nilimsukuma na fimbo yangu. Ndipo nilipogundua
kwamba simba huyo jike alikuwa amekufa," amesema.
Wakati
Bwana Mori aliporejea na kundi la maafisa kuondoa mzoga huo, walimkuta
mtoto huyo wa simba akiwa amekaa kando ya mwili wa mama yake.
Simba
huyo jike ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na moja , alivunjika
mbavu na kupata majereha ya ndani na kufa kutokana na kuvuja damu
nyingi.
Mtaalam
wa Simba Yadvendra Dev Jhala wa taasisi ya Wanyama Pori ya India
ameiambia BBC kuwa hajawahi kusikia tukio kama hilo linalomhusu mtoto wa
simba.
''Simba na walinzi wao''
Lakini
amesema katika eneo la Gir hakuna mgogoro kati ya simba na binadamu na
"kwa ujumla Simba wanawafahamu vizuri walinzi wao binafisi ".
Bwana
Sharma anasema wanafahamika kwa tabia yao ya maisha ya kijamii: "Si
kama Mbwa, hawatoi kucha au kutikisa mikia, lakini wanawatambua walinzi
wanaowaona kila siku.."
Maafisa
wa wanayama pori wanasema kwa ujumla watoto wa simba ni wategemezi mno
wa mama zao kwa ajili ya maisha yao hadi wanapofikia umri wa miaka
miwili na nusu hadi mitatu.
Mtoto huyo wa simba mwenye umri wa miezi 15, kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa maafisa wa misitu.
"Mama
yake, Rupa, alionekana kuwa mpweke na aliwinda peke yake,Lakini kwa
sasa simba huyo jike ametoweka, tunatarajia mtoto huyo wa simba
atajiunga na kundi lingine, au simba mwingine jike huenda akaanza
kumtunza," amesema Bwana Sharma.
Source: BBC
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Matukio
Friday, 22 August 2014