1. OR TAMBO INTERNATIONAL AIRPORT (ORTIA), JOHANNESBURG - AFRIKA KUSINI.
Kiwanja
hiki ndicho kiwanja bora zaidi Afrika na kina uwezo wa kuhudumia zaidi
ya watu Milioni 17 kwa mwaka na kwa sasa kiwanja hiko kimefanyiwa
marekebisho na kuongezwa miundo mbinu na kukifanya kiweze kuhudumia
zaidiya abiria Milioni 28 kwa mwaka.
Hata
hivyo, ORTIA ndicho kiwana kikubwa zaidi cha ndege na pia kilicho na
pilikapilika nyingi kabisa Afrika na pia kiwanja hiko kina wafanyakazi
zaidi ya 18,000 walioajiriwa kiwanjani hapo na makampunim tofauti
tofauti. Jina la kiwana hiko limetoka na aliyekuwa akipinga masuala ya
ubaguzi wa rangi Afrika ya kusini kipindi cha makaburu aliyejulikana
kama Oliver Reginald Tambo kama kumuenzi.
2. CAPE TOWN INTERNATIONAL AIRPORT, CAPETOWN - AFRIKA KUSINI.
Kiwanja
hiki kipo Capetown Africa ya kusini na ifikapo mwaka 2015 kitakuwa kina
hudumia zaidi ya Abiria Milioni 14 na pia kiwanja hiki hutumika sana
kwa ajili ya shughuli za kitalii kwasababu mji wa Capetown una vivutio
vingi vuya utalii nchini humo.
3. KING SHAKA INTERNATIONAL AIRPORT, DURBAN - AFRIKA KUSINI
Kiwanja
hiki kilifunguliwa mnamo mwezi Mei 2010 na pia kina julikana kwa jina
la LA MERCY AIRPORT kipo kilometa takriban 35 kaskazini kutoka katika
mji wa Durban. Pia inasemekana kiwanja hiki ni kikubwa mara tatu zaidi
ya Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Durban (Durban International
Airport).
4. CAIRO INTERNATIONAL AIRPORT, CAIRO - MISRI
Hiki
ni kiwanja cha ndege kikubwa zaidi Misri na ni cha pili kwa kuwa na
pilika pilika nyingi za watu na pia zaidi ya ndege 65 hutumia kiwanja
hiko kwa mwaka.
5. HURGHADA INTERNATIONAL AIRPORT, HURGHADA - MISRI
Kiwanja
hiki kinajengo la abiria moja tu ambayo inafanya kazi kwa sasa na pia
kinaongezwa kinaongezwa jengo lingine la abiria ambalo litakifanya
kiwanja hiki kiweze kuhudumia zaidi ya abiria milioni 7.5 kwa mwaka.
Hata hivyo ni zaidi ya ndege 40 hutumia kiwanja hiki kwa mwaka.deee