BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
SAPRAIZ! Beautiful
Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) ameibua viulizo baada ya kuonekana
akirandaranda na pete ya ndoa kidoleni ikidaiwa kuwa amevalishwa na
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa siri kubwa, Ijumaa Wikienda lina
stori exclusive.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) akionyesha pete aliyovishwa na Diamond.
IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada
ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusiana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda
liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo na kujua mbivu na mbichi.
Kwa
mujibu wa rafiki wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata
mashosti zake hawajui kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao
kuhusu nini kinaendelea huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao
wamefunga ndoa ya siri.
Muonekano wa karibu zaidi wa pete hiyo katika kidole cha Wema.
ALISHAMVISHA YA UCHUMBA
Kuna
maelezo kwamba Diamond alifanya hivyo ili kuzuia mwanaume mwingine
kumvisha Wema pete ya ndoa kwani alishamvisha ya uchumba tangu mwaka
2011 kwenye Ukumbi wa New Maisha ulipo Masaki jijini Dar.
WEMA LAIVU
Wiki iliyopita jitihada za kumnasa Wema akiwa na pete ya uchumba zilizaa matunda ambapo mwanahabari wetu alimuweka ‘mtukati.
Wema
alipotakiwa kuanika ukweli juu ya pete hiyo, alikubali na kueleza kuwa
ameamua kufunguka kwa mwanahabari wetu baada ya kuwa kimya tangu
alipovishwa pete hiyo.
Wema Isaac Sepetu akiwa na mpenzi wake Diamond.
HAJAFUNGA NDOA LAKINI…
Wema
alisema si kweli kwamba amefunga ndoa ya siri ila Diamond alimvisha
pete hiyo kama urembo akijua kabisa kwamba yeye ni wife material (anafaa
kuwa mke).
“Sijafunga ndoa jamani. Hii pete alininunulia baby wangu Nasibu (Diamond) wakati tukiwa South Africa (Afrika Kusini).
WEMA AIONA PETE, YAMVUTIA
“Alininunulia
na kunivisha tulipokwenda kwenye Tuzo za MTV Africa (MAMA). Nakumbuka
tuliingia kwenye duka moja nikaiona hii pete ikanivutia sana,
nikamwambia Nasibu ndipo akaninunulia na kunivisha palepale.
Wema Isaac Sepetu akiwa na mkwewe, mama Diamond.
“Cha kushangaza ni kwamba imewatatiza wengi na kuhisi ndoa tayari.
“Hii
pete ndogo niliinunua mwenyewe hapahapa Bongo na kuivaa kama urembo
tu, hakuna tofauti na hilo kuhusiana na hizi pete nilizovaa kidole
husika,” alisema Wema ambaye kidoleni kwake kunaonekana pete mbili,
kubwa na ndogo.
WEMA NI WIFE MATERIAL?
Alipoulizwa
kwa nini Diamond aliamua kumvisha pete hiyo kabla ya ndoa, Wema
alifunguka: “(kicheko) hilo sina uhakika nalo but amegundua mimi ni wife
material hataki kunipoteza. Kanipa heshima anayostahili kupewa
mwanamke...”
AMSHUKURU MTABIRI
Wakati
huohuo, Wema amemshukuru mtabiri, Maalim Hassan Yahya ambaye mwanzoni
mwa mwaka huu alitabiri kuwa mastaa hao wataoana mwezi ujao (Agosti)
mwaka huu akiomba Mungu na iwe hivyo.
“Natamani hiyo ndoa na nasubiria hiyo siku ili utabiri utimie, ni jambo la heri jamani,” alisema Wema.
DIAMOND VIPI?
Alipotafutwa
Diamond ili afunguke kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ya kiganjani
iliita bila kupokelewa. Wakati huohuo, mashabiki wa mastaa hao,
wamewashauri mama Wema na mama Diamond kuwa kitu kimoja ili kufanikisha
ndoa hiyo ya watoto wao.
NI PETE YA PILI YA NDOA!
Ukiacha
pete hiyo ya ndoa aliyovishwa na Diamond, Wema aliwahi kuvishwa pete
kama hiyo alipofunga ndoa na jamaa aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe ambayo
haikudumu hata mwezi mmoja.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI