Mwisho wa reli? Lile
penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa Bongo
Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya
Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho
baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha
mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.
Staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
TUJIUNGE INSTAGRAM
Suala
la Wema kukashifiwa liliibuka baada ya wadau mbalimbali ambao ni
mashabiki wa Wema wanaojiita Team Wema kuhoji kwenye Mtandao wa
Instagram kwamba ni kwa nini Diamond alimtumia Wema kwa kukata mauno
jukwaani (hivi karibuni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza) badala ya
kumfungulia biashara ya maana?
“Tujaribuni
kumshauri Wema maana tunaona anatumiwa vibaya na huyu Diamond.
Haiwezekani ampandishe kwenye majukwaa halafu amkatishe mauno namna ile
kama kweli ana nia ya kumuoa,” aliandika mmoja wa wadau ambaye ni mfuasi
wa Team Wema.
Team Wema walidaiwa kufungua mjadala huo wa kumshauri
‘msanii wao huyo wa ukweli’ kufuatia kusambaa kwa picha zinazomuonesha
Wema akiwa na shosti wake, Aunt Ezekiel Grayson wakikata mauno jukwaani
kupitia wimbo wa Diamond wa Mdogomdogo.
WATOA MIFANO YA WAREMBO
Wadau
hao walimtaka Wema kuiga mifano ya warembo wenzake waliopita kama Nancy
Sumari (2005), Hoyce Temu (1999), Faraja Kotta (2004) na wengine wengi
kwa jinsi wanavyojishughulisha na shughuli mbalimbali na kuweza
kuendesha maisha yao bila kudhalilishwa majukwaani.
Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’
WAKERWA WEMA KUWA MCHEZA SHOO WA DIAMOND
Team
Wema walikwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba, wanasikitishwa na Wema
kutojulikana moja kwa moja anafanya kazi gani ya maana, zaidi ya kuwa na
uhusiano na Diamond ambaye anamgeuza kama mcheza shoo wake wa kukata
mauno.
DIAMOND AWAJIBU
Baada
ya wadau hao kumshauri Wema huku wakihoji baadhi ya mambo ambayo
walidai yanamdhalilisha, kupitia mtandao huohuo wa Instagram, Diamond
alishindwa kuvumilia ushauri huo uliomgusa na kuamua kuandika waraka
wake unaodaiwa kumdhalilisha Wema.
Katika waraka huo, Diamond
alieleza kwamba yeye kama yeye huwa anamtimizia Wema mahitaji ya muhimu
kama mpenzi wake na suala la kumpa mtaji wa kufanya biashara.
WARAKA WENYEWE:
“Nafikiri
ningewaona kweli mna akili na mapenzi ya dhati kwa huyo msanii wenu
(Wema) kama mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze
starehe zisizo na faida, huenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye
kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe,
mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula
vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia
kazi. “Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha
anampeleka ng’ombe wake kwenye maji safi ila yeye ng’ombe mwenyewe ndiyo
anatakiwa aamue kunywa maji!
Aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda.
“Au
mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza
nimuigizie miye? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie miye? Ni juhudi
zako kwanza! Leo hii hata ningepewa mamilioni ya mamilioni kama
nisingekuwa na moyo wa kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu,
nisingefikia hapa nilipo! Kama nimekuchefua lamba ndimu usitapike.”
WAMGEUKIA DIAMOND
Baada
ya waraka huo, mashabiki na wadau waliopo kwenye mtandao huo
walimgeukia Diamond kwa kumlaumu kwamba anavyofanya siyo vizuri mbona
amemfungulia dada yake Esma Platnumz duka la maana lakini Wema amekuwa
akimtumia tu bila faida yoyote?
MARTIN AJIVUA UMENEJA
Kutokana
na waraka huo, aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda naye aliandika
wa kwake na kutangaza kuachia ngazi ya umeneja kwa mwanadada huyo.
MAMA WEMA AFUNGUKA
Baada
ya meneja huyo kubwanga manyanga, wanahabari wetu walimsaka mama mzazi
wa Wema, Miriam Sepetu na kumuuliza juu ya mtazamo wake kuhusiana na
penzi hilo la mwanaye ambapo alisema kwa sasa penzi hilo limemchosha
hivyo anaacha ‘liserereke’.
Alisema kuwa anawaachia wenyewe waendelee kwani ni watu wazima sasa hadi pale atakapohitajika kutoa msaada kama mzazi.
Mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu
“Jamani
sitaki mniweke kwenye masuala ya Wema na Diamond, wao wazungushane wee
mpaka watakakoamua wenyewe maana wao ni watu wazima.
“Siwezi kuwaingilia, acha liserereke tuone mwisho wake,” alisema mama Wema.
Jitihada
za kumpata Wema zilishindikana baada ya simu yake kuita bila
kupokelewa, achilia mbali kutojibu ujumbe aliotumiwa katika Mtandao wa
WhatsApp huku mmoja wa marafiki zake akisema kuwa ishu hiyo
imemchanganya.
TUJIKUMBUSHE
Penzi
la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila
kukicha. Waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kabla ya kurudiana Oktoba,
mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa
kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.