CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimempa kibarua kingine Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, kuendelea na mazungumzo ya kusaka mwafaka na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ili kunusuru mchakato wa Katiba mpya.
Pamoja na hatua hiyo, CCM imesema imesikitishwa na hatua ya kuvunjika
kwa mazungumzo yaliyohusisha viongozi wake na wale wa CUF, Chadema na
NCCR-Mageuzi.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa kikao cha Kamati
Kuu (CC) ya CCM kilichofanyika mjini Dodoma juzi, Katibu wa NEC, Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye, alisema pamoja na kutopatikana kwa mwafaka, wameazimia Bunge Maalumu la Katiba liendelee na vikao.
Alisema hatua ya Kinana kuendelea kukutana na vyama pamoja na wadau
wengine, itasaidia kuendelea kupata maridhiano kuhusu kuendelea mchakato
wa Katiba mpya kwa mujibu wa sheria.
“Kamati Kuu inaendelea kuwasihi Watanzania wote kuendelea kushikamana
na kuvumiliana pale wanapopishana kimtazamo juu ya hoja mbalimbali za
Katiba kwa amani, utulivu na Utanzania wetu ni muhimu kuliko tofauti
zetu za kimtazamo,” alisema Nape.
Alisema CCM inaridhishwa na juhudi za Kituo cha Demokrasia Tanzania
(TCD), pamoja na vyama vinavyounda Ukawa kutafuta mwafaka wa kisiasa kwa
lengo la kuimarisha amani, utulivu, mshikamano na kuaminiana kati ya
wadau mbalimbali.
“Kamati Kuu inaunga mkono juhudi za TCD za kuendeleza mashauriano
kati ya vyama na ndani ya vyama kwa lengo la kupunguza mivutano, kujenga
uaminifu, ustahimilivu na umoja kati yao,” alisema.
Mawaziri wafyekwa ziara ya JK
Akizungumzia utoro wa mawaziri katika Bunge Maalumu la Katiba, Nape
alisema mkakati wa CCM hivi sasa ni kupunguza idadi kubwa ya mawaziri
kwenye ziara za Rais Kikwete.
Alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza utoro na hata kuwafanya wengi wao kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge la Katiba.
“Mbali na mawaziri, pia CCM itawabana wabunge wasiokuwa na sababu za
msingi kutohudhuria vikao hivyo, ili waweze kushiriki,” alisema Nape.
Alisema ziara ya Rais Kikwete iliyoanza mjini Morogoro jana, itakuwa
na mawaziri wachache, lengo likiwa kuwafanya wengine wahudhurie vikao
vya kamati za Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.
“Hatuwezi kufanya shughuli za Serikali zisimame, lakini tutaangalia
namna ya kupunguza zile zisizo za lazima ili mawaziri waweze kuhudhuria
hivi vikao, hata leo rais anaanza ziara Morogoro, lakini idadi ya
mawaziri kwenye ziara yake imepunguzwa ili wengine wafanye kazi ya Bunge
la Katiba.
“Kuna taarifa za wabunge wetu kutohudhuria, lakini kwa kiasi fulani
wana sababu, ila tutaangalia kama sababu zenyewe ni za msingi,” alisema
Nape.
Alisema kuwa kuna kamati za kusimamia na kuangalia mahudhurio ya wajumbe hao na kuwa zitashughulikia suala hilo.
“Ni vigumu kuhudhuria kwa asilimia 100, lakini tutaangalia namna
nzuri ya kufanya ili wasio na sababu za msingi wahudhurie hivyo vikao,”
alisema.
Nape alisema Kamati Kuu ya CCM imewataka wajumbe wote kuhakikisha
wanahudhuria vikao vyote vya kamati na kuijadili rasimu kwa mapana huku
wakitanguliza mbele masilahi ya taifa kama njia ya kupata Katiba
inayotarajiwa na Watanzania walio wengi.
Wiki iliyopita, Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Khamis
Hamad, alisema kwa kiasi kikubwa wajumbe wa Bunge hilo kutoka Tanzania
Bara wakiongozwa na mawaziri wamekuwa watoro kwenye vikao vya kamati.
Alisema hali hiyo hufanya kuchelewa kuanza vikao kwa baadhi ya kamati kutokana na akidi kutotimia.
Kauli ya Ukawa
Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu msimamo wa kurudi kwenye
mazungumzo na CCM, mwenyekiti mwenza wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema umoja huo una nia ya
dhati ya kutetea masilahi ya taifa.
Alisema kama kweli CCM imekubaliana kusaka mwafaka, wao wako tayari
kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili waweze kujadili mustakabali wa nchi
na si masuala ya kisiasa.
“Tupo tayari kurudi kwenye meza ya mazungumzo kwa sababu Ukawa
inafanya kazi ya kutetea masilahi ya wananchi, na kwamba hatufanyi kazi
kwa masilahi ya vyama vyetu,” alisema Mbatia.
Aliongeza Katiba si jambo la lelemama, bali ni suala la utashi ambalo
kila mmoja anapaswa kulitambua, hivyo basi CCM wanapaswa kuwa makini
kwa kutanguliza masilahi ya wananchi kwanza na kuweka kando ya chama
chao.
Mbatia alisema Ukawa hawajawahi kukataa mazungumzo na CCM yanayolenga
masilahi ya wananchi, hali ambayo inaweza kusaidia kupatikana kwa
mwafaka wa suala hilo.
“Kama CCM wamekaa chini na kujadili suala hilo ni sawa, kwa sababu
linaweza kuleta mwafaka wa upatikanaji wa Katiba mpya, hivyo basi
wanapaswa kuondoa itikadi ya chama kwenye kikao hicho,” alisema.
Katibu wa Ukawa ndani ya Bunge, Julius Mtatiro, alisema kuwa ili
waweze kufikia mwafaka wa suala hilo, CCM inapaswa kusitisha vikao vya
Bunge Maalumu la Katiba waweze kurudi kwenye meza ya mazungumzo.
Alisema bila ya kufanya hivyo, hakutakuwa na majadiliano yatakayozaa
matunda kwa sababu wanaingia kwenye mvutano ambao utarudisha nyuma
mchakato wa Katiba.
“Ili tuweze kufikia mwafaka, CCM wanapaswa kusitisha vikao vya Bunge
Maalumu la Katiba na kurudi kwenye meza ya mazungumzo, hapo ninaamini
tunaweza kuingia kwenye maridhiano,” alisema Mtatiro.
Credit: Mtanzania
Credit: Mtanzania
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >



