MAJONZI yameanza
kuwakuta baadhi ya waumini wa kanisa katoliki Bongo kufuatia kiongozi
wao wa dunia, Papa Francis (77) kuweka hadharani hatima ya maisha yake.
Katikati
ya wiki hii, Papa Francis akiwa anarejea Vatican kutoka ziarani Korea
Kusini alisema anaamini ana miaka miwili au mitatu ya kuishi duniani na
si vinginevyo.
“Najaribu
kufikiria kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua
kwa sababu hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu
nitakuwa nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba,” alisema papa huyo
kauli iliyozua sitofahamu duniani.
Licha
ya kwamba Papa Francis hakusema lini anaweza kuiaga dunia lakini baadhi
ya vyanzo vya habari kutoka Vatican vinasema kiongozi huyo amekuwa
akiwaambia wasaidizi wake wa karibu kuhusu siku zake chache zilizosalia
duniani.
Wachambuzi wa masuala ya kiimani kwa nyakati tofauti walisema huenda kiongozi huyo ana tatizo la kiafya ambalo halijawekwa wazi.
Jijini
Dar es Salaam, baadhi ya waumini wa kanisa katoliki waliozungumza na
gazeti hili walisema kauli hiyo ya papa imewatia majonzi kwani inawapa
tafsiri ya kumkosa siku si nyingi.Samuel Msokali, anaabudu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maxmillian Kolbe, Mwenge yeye alisema:
“Nimepokea
kwa majonzi makubwa kauli ile ya papa. Kama anaumwa atuweke wazi
waumini wake. Kama amepewa maono na Mungu pia atuweke wazi tujue.”
Mama Juliana, yeye anaabudu Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, alisema:
Mama Juliana, yeye anaabudu Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, alisema:
“Siamini
kama kweli papa alisema yale maneno. Ni makali sana na yanachoma,
nilitoa machozi niliposikia, nimeanza kulia hata kabla ya siku yake
haijafika.”
Muumini
mwingine anayeabudu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu
Anuarite, Makuburi (aliomba jina lake lisiandikwe) alisema anaamini papa
ameona katika maono kifo chake kwa sababu ya usafi wa moyo.
“Mimi
naamini papa ni msafi wa moyo kwa hiyo ameoneshwa na Mungu kwamba muda
wake wa kumtumikia duniani umeisha. Kule kusema ni kutuweka tayari
kupokea taarifa,” alisema muumini huyo wa kiume.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >



