Habari Kali
Loading...

SHEIKH PONDA KUSOTA RUMANDE

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Kesi inayomkabili kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda imeendelea kupigwa kalenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro.

Ilielezwa mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo haiwezi kusikilizwa kwa sasa kwa kuwa jalada lake bado halijarudi kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali ya iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, kutoa maneno yenye kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa, makosa ambayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10 mwaka jana katika eneo la Uwanja wa Ndege Manispaa ya Morogoro.

Baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mary Moyo alisema kesi hiyo itaendelea kutajwa mpaka jalada hilo lililoitishwa Mahakama Kuu Oktoba 15 litakaporudishwa Mahakama ya Morogoro.

Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo jana chini ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na sihala za moto, mabomu ya machozi na mbwa huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzito wa mahakama hiyo.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Lilian Lutabula aliyeshirikiana na mwendesha mashtaka wa polisi, Zabron Msusi wakati upande wa utetezi uliwakilishwa na wakili Josephine Jackson kwa niaba ya wakili Bathoromeo Tarimu anayemtetea Sheikh Ponda.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Ponda alirudishwa rumande ambako ataendelea kupafanya kuwa maskani yake hadi Mei 5 mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea kutajwa mahakamani hapo

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top