
Kundi la
muzikiwa wa Hip Hop kutoka Tanga Wagosi wa Kaya limerudi rasmi kwenye
ulingo wa burudani ya muziki baada ya kuwa kimya kwa muda wa miaka 8.
Kundi hilo linaloundwa na Fredrick Mariki a.k.a Mkoloni na John Simba
a.k.a Dr John lenye makazi yake jijini Tanga na Dar es salaam lipo
kwenye hatua za mwisho kukamilisha album waliyoipa jina la “UAMSHO”.
Akiongea na mwandishi wa safu hii, Mkoloni alifafanua kuwa “Wagosi
wa Kaya tunatarajia kufyatua album ya kihistoria baada ya kukaa kimya
kwa miaka 8 na bado tumeona nafasi yetu ipo wazi kwa kile tulichokuwa
tunakifanya kwenye gemu,”alisema Mkoloni.
Album hiyo ya UAMSHO inatarajiwa kuwa na jumla ya nyimbo 12 huku akiweka
wazi baadhi ya nyimbo na wasanii walioshirikishwa, alizitaja nyimbo
hizo kuwa ni pamoja Gahawa, Bao ambazo wameshazitoa sambamba na video
zake na Tizauya kaya (tunarudi nyumbani) ambao wamemshirikisha Komando
Lady Jay Dee, Thabit, Potofu, Unaaharibu, Kipo cha kuwaambia ambapo
wasanii wengine watakaoshirikishwa ni pamoja na Prof Jay na wengineo.
Akielezea sababu za kuwashirikisha wasanii hao, Mkoloni alisema kuwa “Kitu
ambacho watu wanapaswa kujua ni kuwa wasanii wengi tutakaowashirikisha
ni wale ambao hatujawahi kufanya nao kazi tokea kuanza muziki na ni
wasanii ambao wanaheshimika mbele ya jamii kutokana na uwezo wao wa
kufanya kazi na ukaribu wao kwa jamii yetu”
Wagosi wa Kaya ambao kazi zao wamekuwa wakizifanyia katika studio ya
Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam hawakuweka wazi kama
wamesaini lebo katika studio hiyo, "pale Tongwe rec sisi tunafanya
kazi zetu hilo la kuhusu kuwa chini ya lebo kama lipo litafahamika
kwani sisi ni watu wazima na hatuna tabia ya kuficha mambo”,alisema Mkoloni.
Kundi la Wagosi wa Kaya tokea mwaka 2001 mpaka sasa limeshaingiza sokoni album tatu ambazo ni Ukweli Mtupu mwaka 2002, Ripoti Kamili mwaka 2003, Nyeti mwaka 2005 na album ambazo hazikufanikiwa kutoka ni Tizauya Kaya mwaka 2005 waliyofanya Bongo Rec chini ya utayarishaji wake P Funk na X mwaka 2006 waliyofanya PKP chini ya utayarishaji wa Duke Tachez wa Tamadunimuzik, sasa huu ni mwaka 2014 ambapo jamii ya mashabiki wanasubiri album yao nyingine mpya inayoitwa UAMSHO kutoka Tongwe Rec.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >