MKONGWE
wa muziki wa dansi nchini, Muhidin Mohamed Mwalimu Gurumo ‘Maalim
Gurumo’ amezikwa jana kwenye makaburi ya kijijini kwake, Masaki,
Kisarawe mkoani Pwani, lakini wosia aliouacha kuhusu mazishi yake umezua
utata, Risasi Mchanganyiko limedokezwa na wengi.
Kwa mujibu wa chanzo, wakati wa uhai wake Maalim Gurumo ambaye
alikuwa mwanamuziki wa bendi mbalimbali nchini, ikiwemo Ottu na baadaye
Msondo Music Band, alisema atakapotangulia mbele ya haki asizikwe siku
inayofuata.
Mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin 'Maalim' Gurumo enzi za uhai wake.
LIMWAMBIA NANI?
Kwa mujibu wa chanzo, Gurumo
alimpa wosia huo mjomba’ake aitwaye Selemani Mikole ambaye ndiye
aliyemlea alipofika jijini Dar es Salaam baada ya kufiwa na baba yake
mzazi, mzee Mohamed Mwalimu Gurumo.
“Gurumo alikataa kuzikwa siku inayofuata. Mjomba wake ndiye aliyetoa siri hiyo mara baada ya Gurumo kufariki dunia.
Waombolezaji wakiwa na simanzi.
“Yaani alitaka hivi, mfano amefariki dunia leo (jana Jumanne) basi
mazishi yake yawe baada ya siku mbili, yaani keshokutwa (Alhamisi).
“Mjomba’ake alimuuliza sababu ya uamuzi
huo, akasema yeye ni mtu mwenye mashabiki wengi, angeomba pawe na muda
ili wengi waweze kuhudhuria mazishi yake,” kilisema chanzo hicho.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salim.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salim.
WAISLAM WATOFAUTIANA
Jumatatu iliyopita kwenye
msiba wa nguli huyo nyumbani kwake, Mabibo-Makuburi jijini Dar es Salaam
baadhi ya waombolezaji wenye imani ya Kiislam walisikika wakipingana na
wosia huo wa marehemu.
Baadhi walisema si sawa Muislam kuzikwa baada ya saa ishirini na nne
huku wengine wakisema wosia wa marehemu ndiyo maelekezo makuu ya
mazishi.
Mke wa marehemu Pili Saidi akiomboleza kifo cha mumewe.
“Hapa hatuzungumzii sheria za dini,
tunazungumzia kutii wosia wa marehemu. Siku zote wosia wa marehemu
unazingatiwa kwanza,” alisikika akisema mwombolezaji mmoja baada ya
kuambiwa mazishi ya marehemu huyo ni Jumanne na si Jumatatu kama
alivyoamini.
Mtoto wa marehemu Mariamu Gurumo akiomboleza kifo cha baba yake.
Mtoto wa marehemu Mariamu Gurumo akiomboleza kifo cha baba yake.
UISLAM UNATAKAJE?
Risasi Mchanganyiko lilipata
nafasi ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Kiislam wa jijini Dar es
Salaam ambapo kila mmoja alitoa mwongozo wake anaoujua kuhusu imani ya
Kiislam inavyosema kuhusu mazishi ya muumini wake.
“Kwenye Uislam kuna ngazi tatu tu baada ya kifo. Kuoshwa, kuswaliwa
na kuzikwa. Kama mtu anakata roho asubuhi na madaktari wakathibitisha,
mwili wake hautakiwi kulala,” alisema shehe mmoja huku akiomba
kusitiriwa jina.
Waombolezaji wakiangua kilio baada ya msafara wa msiba kuwasili Masaki, Pwani.
MAALIM HASSAN NAYE ALONGA
Risasi Mchanganyiko
pia lilizungumza na mtabiri maarufu nchini kwa sasa, Hassan Hussein
Yahya ‘Maalim Hassan’ ambaye kwa upande wake aliweka wazi mambo haya:
“Kusema kweli Uislam mwili haulali. Labda kama mtu amekutwa na mauti
usiku, lakini siku inayofuata lazima akasitiriwe (akazikwe).
“Endapo kuna dharura sana, basi zisipite
saa ishirini na nne tangu kifo. Lakini hilo la Gurumo sidhani kama ni
tatizo, unajua imani ipo, lakini pia tunaheshimu mila na desturi zetu
Waafrika.”
Ndugu na jamaa wa marehemu wakiomboleza.
Ndugu na jamaa wa marehemu wakiomboleza.
SHEHE MKUU MKOA WA DAR ES SAALAM
Gazeti hili pia lilizungumza na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum ambapo alisema:
“Katika Uislam hakuna sheria kwamba mtu akifa lazima azikwa siku
hiyohiyo, wala hakuna siku zilizotajwa kuwa ndizo za marehemu kuwepo
kabla ya mazishi. Ila kumzika marehemu mapema ni suna.
“Mbona Mtume Mohamed (S.A.W) alikufa Jumatatu akazikwa Jumatano?”
KUMBE SI DHAMBI
Pia Risasi Mchanganyiko
lilizungumza na baadhi ya Waislam wanye elimu ya imani hiyo kwa undani
ambapo wengi walisema mwili wa marehemu kuzikwa ndani ya saa 24 ni
sheria ya kawaida lakini si dhambi kama ikitokea ukapitiliza saa hizo.
Waombolezaji wakifukia kaburi la Gurumo huko Masaki, Kisarawe mkoani Pwani.
ALIJITABIRIA KIFO?
Akizungumza na gazeti hili
juzi kwa majonzi makubwa, mtoto wa marehemu aitwaye Mariam Gurumo
alisema baba yake ni kama alijitabiria kifo kwani Aprili 9, mwaka huu
(siku nne kabla ya kifo) walikwenda Kisarawe kwa ajili ya kusalimia
ndugu, jamaa na marafiki na kurudi Dar.
“Hiyo safari ilikuwa niende mimi. Nikaenda nyumbani kumuaga, lakini
akasema lazima twende familia yote. Basi tukajaza mafuta kwenye lile
gari alilozawadiwa na Diamond (Toyota FunCargo) tukaenda.
“Tulipofika, baba akazua tukio jingine, akasema lazima tutembelee
makaburi ya familia kwa ajili ya kuyasafisha na kupiga dua kuwaombea
marehemu waliolala pale jambo ambalo kwetu sisi watoto tulilishangaa,”
alisema mtoto huyo.
Saidi Mabela akitoka kaburini baada ya kumhifadhi kiongozi mwenzake, Gurumo.
Akaendelea: “Lakini tulipojiandaa kwenda makaburini, mvua kubwa
ilinyesha. Kwa hiyo tukamwacha baba tukaenda sisi kufanya shughuli hiyo.
TATIZO LAANZA HADI KIFO
Mtoto huyo aliendelea
kuweka kwamba, wakati wanarudi kutokana na milima na mabonde ghafla hali
ya mzee Gurumo ikawa mbaya. Walipofika Msanga akaomba kwenda
kujisaidia. Mara mvua kubwa ikanyesha tena naye akanyeshewa na kulowa
chapachapa.
Alisema kuwa, hali hiyo ilimsababishia mzee Gurumo kuzidi kudhoofu
zaidi kutokana na tatizo la mapafu kubana na kushindwa kupumua sawasawa.
“Tulifika Dar, hali ikazidi kuwa mbaya ndipo ikatulazimu kumkimbiza
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu ambapo Jumapili
akafariki dunia majira ya saa tisa alasiri,” alisema mtoto huyo
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >