Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kinondoni ACP, Camillius Wambura, amethibitisha
kutokea kwa tukio hiloa ambapo amesema uchunguzi wa tukio hilo bado
unaendelea ikiwa ni pamoja na kumtafuta mama mzazi wa mtoto huo.
Tukio
hilo limetokea Aprili 16, mwaka huu, ambapo wasamaria wema walifanikiwa
kumuokoa mtoto huyo kisha kumpeleka katika kituo kidogo cha Polisi
kilichopo Bunju A, na baadaye alihamishiwa katika kituo cha Polisi cha
Wazo, ambapo pia ilikutwa barua aliyoiandika mama wa mtoto huyo ikiwa
karibu na mtoto huo.
Aidha
aliandika barua yenye maelezo mafupi yanayoelezea maisha yake, huku
akielekeza lawama kwa mzazi mwenzake ambaye hakumtaja jina kuwa
amemtelekeza muda mrefu bila kumpatia mahitaji muhimu kabla ya mtoto
huyo kuzaliwa, hali iliyomlazimu kuchukua uamuzi wa kumtelekeza mtoto
huyo.
Aidha barua hiyo ambayo FikraPevu imeipata, inasema kuwa mama mzazi wa mtoto huyo alitaka kujiua kwa kunywa sumu, ingawa hakufanya hivyo.
“Sijamuacha
kwa ubaya ninampenda mwanangu sana ila kutokana na maisha yangu kuwa
magumu, nimeamua kumtelekeza hapa ili apate msaada kwa wasamaria wema,
mzazi mwenzangu kanikataa kuanzia kwenye mimba nimejaribu hata kutoa ila
imeshindikana” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Kwa
mujibu wa barua hiyo inaeleza kuwa mtoto huyo alizaliwa Machi 17, mwaka
huu, katika eneo la Mistuni kufukuzwa kila mahali, ambapo mtoto huyo
hajawahi kupata chanjo ya aina yeyote, ambayo inatakiwa kutolewa kwa
mtoto mchanga ili aweze kupata kinga ya kumkinga na maradhi mbalimbali.

Barua iliyoachwa na mama wa mtoto huyo
Ripoti
ya utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa)
katika mikoa 18 ya Tanzania Bara na Visiwani umebaini kuendelea
kushamiri kwa vitendo hivyo huku matukio 996 ya udhalilishaji
yaliripotiwa kutokea katika wilaya sita za Zanzibar.
Kati
ya matukio hayo, 242 yalihusu ubakaji, vipigo vilikuwa 388, ndoa za
utotoni 42, kutelekezwa 96, mimba za utotoni 228, ambapo kwa upande wa
Tanzania Bara ukionyesha kuwa Wilaya ya Babati mkoani Manyara inaongoza
ikiwa na matukio 132.
Ripoti
ya Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania, iliyotolewa na serikali
pamoja na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) mwaka 2011,
ilidhihirisha kuwa msichana mmoja kati ya watatu na mvulana mmoja kati
ya saba nchini Tanzania hukumbwa na unyanyasaji wa kijinsia kabla ya
kufikisha umri wa miaka 18.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >