Habari Kali
Loading...

Taifa Stars kudadadeki

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >


Wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia gori.
Na Hans Mloli
UKITAKA raha jipe mwenyewe, Taifa Stars, jana, ilifanya kile kitu ambacho hakikutegemewa na wengi kwa kuishushia mvua ya mabao Benin katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Stars ambayo inashika nafasi ya 115 katika viwango vya ubora wa Fifa, ilionyesha soka zuri mbele ya wapinzani wao hao wanaoshika nafasi ya 78 katika viwango hivyo vya ubora na kuwafunga 4-1.
Wachezaji wa Stars wakicheza kwa kujiamini huku wakishangiliwa na mashabiki wachache walijitokeza uwanjani hapo mvua ikinyesha, walipata mabao kupitia kwa Nadir Harob ‘Cannavaro’ dakika ya 16, Amir Kiemba (40), Thomas Ulimwengu (49) na Juma Luizio (71).
Cannavaro alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Erasto Nyoni, Kiemba alifunga kwa kuubetua mpira akiunganisha krosi ya Mwinyi Kazimoto, Ulimwengu alicheza na nyavu baada ya kuunganisha krosi ya Mrisho Ngassa, kisha Ulimwengu tena akampa pasi nzuri Luizio ambaye aliutupia mpira wavuni bila purukushani yoyote.
Katika mechi hiyo, furaha ilinogeshwa na mashabiki wa kundi maarufu la Simba Ukawa, waliokuwa wamevaa fulana nyeupe na kofia zenye rangi ya bendera ya Tanzania, waliokuwa wakiimba na kucheza kwa muda wote wa mchezo huo bila kujali mvua iliyokuwa ikinyesha uwanjani hapo.
Bao la kufutia machozi la wageni lilifungwa na Suanon Fadel kwa shuti lililomshinda kipa Mwadini Ally.
Stars ilishuhudiwa na Kocha wa Yanga, Marcio Maximo aliyekuwepo jukwaani.
Kikosi cha Stars: Mwadini Ally, Shomari Kapombe, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu.
Mchezo wa utangulizi baina ya viongozi wa Kiislamu na Kikristo uliochezwa kwa dakika 30 kwa lengo la kuhamasisha amani, mwamuzi wa kati akiwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, uliisha kwa Amani kuifunga Mshikamano bao 1-0, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top