Habari Kali
Loading...

HII NDIO FAIDA YA MSICHANA MWENYE MAKALIO NA HIPSI MAKUBWA...!! BASI SHUKA NAYO HAPA KUFAHAMU

Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
MREMBO MWENYE HIPS
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati na asidi mbaya kiafya ambazo huwa na madhara za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe.
kuwa, makalio makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.

TIBA YA FANGASI WANAOSHAMBULIA SEHEMU ZA SIRI


Wiki iliyopita tulieleza kwa urefu kuhusu tatizo la fangasi kwa wajawazito baada ya kueleza tatizo la kuwashwa sehemu za siri kunakotokana na fangasi  na tukaahidi kwamba tiba na ushauri tutafafanua leo.
Kabla ya kueleza tiba tufafanue kwamba kuna baadhi ya mambo yanayosababisha watu kuwashwa sehemu hizo nyeti kama vile kuwa na fangasi tuliowataja  katika matoleo yetu yaliyopita.
Wengine huwashwa kutokana na kutumia dawa za antibayotiki kwa muda mrefu. Dawa za antibayotiki ni kama, ampicillini, amoxyclini, ciproflaxine, doxylline, erythromycine, gentamcycine na nyingine nyingi hivyo basi, jamii isitumie ovyo dawa hizi bila ushauri wa daktari.
Kutumia dawa hizo husababisha fangasi kwani huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha sehemu za siri kukiwa hakuna kinga. Sababu nyingine ni unene kupita kiasi. Mtu akinenepa anaweza kupata fangasi kwa sababu unene husababisha jasho sehemu za siri na kuongeza unyevunyevu sehemu hizo, pia michubuko kutokana na kubanwa na chupi.
Sababu nyingine ni utumiaji wa dawa ya jamii ya steroid, dawa hizi ni kama prednisoline, hydrocortisone, dexameltasone na nyingine nyingi. Hizi nazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi kuzaliana kwa wingi sehemu nyeti.
Pia kuna magonjwa yanayosababisha kupungua kwa kinga nayo ni kisukari, Ukimwi na magonjwa mengine yanayopunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi.
Kuwepo na joto kupita kiasi na kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka pia husababisha fangasi sehemu za siri.
Dalili
Dalili kwa maradhi ya fangasi hutofautiana kati ya mtu na mtu ila dalili kubwa ni kutokwa na majimaji meupe wakati mwingine kama mgando wenye rangi ya njano ukiwa umeambatana na muwasho  sehemu za ndani au kwenye mashavu ya sehemu za nje za siri za mwanamke.
Nje ya sehemu hizi za siri hutokea wekundu na maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa pia mgonjwa atajikuta akikojoa mara kwa mara.
VIPIMO
Wote wenye dalili hizo wanashauriwa kwenda kwa daktari ambapo baada ya kumuona ataanza kumchunguza mgonjwa sehemu yake ya siri ambao kitaalamu huitwa PV exam.
Daktari pia atachunguza kama kuna uchafu wowote unaotoka, wingi wake, rangi yake, harufu yake, na mgonjwa awe huru kumsimulia daktari tatizo lake kama anaona haya niliyoyataja.
Mgonjwa atachunguzwa kama ana mitoki sehemu za siri na daktari ataangalia shingo ya kizazi, sehemu ya haja kubwa kama kuna  bawasiri (haemorrhoids) nk.
Itaendelea wiki ijayo.

'Moyo wangu ulisimama kwa dakika 45'


Ruby Graupera uliancha kudunda kwa dakika 45 ingawa baadaye alipata fahamu
Kwa namna alivyoonekana tu Ruby Graupera Cassimiro alikua amepoteza maisha.
Moyo wake uliacha kupiga kwa dakika 45, madaktari waliokuwa wakimfanyia upasuaji kumzalisha mtoto, waliwakusanya wanafamilia kwa ajili ya kusema buriani.
Kilichofuata hapo baadae mapigo ya moyo yakaanza tena kurudi na kuonesha kwenye kifaa maalum mithili ya kompyuta
Graupera Cassimiro alikua hai.Daktari Jordan Kanurr ameonyesha kushangazwa na tukio hilo wala pia hakuwahi kusikia kwa Madaktari aliokuwa akifanya nao kazi.
Mama huyu mwenye umri wa miaka 40, ambaye alijifungua mtoto wake akiwa na afya njema amewashtua sana madaktari.
''Nilikuwa nimekufa,'' Ruby aliambia kituo cha habari cha ABC . ''Mume wangu aliniambia niligeuka rangi mithili ya majivu.Mwili wangu ukawa baridi sana na kwamba mdomo wangu ulikuwa umekauka na hata kukosa rangi. ''
Ruby Graupera ametajwa kama mwanamke wa miujiza baada ya moyo wake kusimama kwa dakika 45
Baadaye Ruby alibandikwa jina na kuitwa mwanamke wa muujiza, ambaye moyo wake ulisimama kwa dakika 45 lakini akaanza tena kupumua.
Graupera alipata tatizo ambalo huwa ni nadra sana kushuhudiwa. Maji yanayomzunguka mtoto tumboni yalichanganyika na mzunguko wa damu wa mama na kusababisha moyo kukandamizwa hali iliyofanya mzunguko wa damu kusimama.
Alichokumbuka cha mwisho kabla ya moyo wake kusimama ni pale alipopelekwa hospitalini kwa kiti cha magurudumu na anasema kilichofuata, alilala usingizi mnono.
Baadaye Ruby aliacha kupumua. Madaktari walijaribu kumuamusha hata kwa kutumia mashine bila mafanikio. Moyo wake ulisimama kwa dakika 45.
Madaktari wanasema yaliyomkuta mzazi huyu ni miujiza mikubwa kwa kuwa hajapata madhara yoyote kwenye ubongo ingawa mapigo ya moyo yalisimama kwa muda mrefu.

MAAMBUKIZI YA FANGASI KWA WAJAWAZITO

WIKI iliyopita tuliona jinsi fangasi wanavyoambukiza na kusababisha madhara mbalimbali sehemu za siri.
Leo tunakwenda mbele zaidi kwa kuangazia akina mama wenye ujauzito ambao hupata fangasi hawa kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili.
Hata hivyo, ieleweke kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya ya fangasi wa Candida albicans.
Matumizi ya dawa za kupanga uzazi  maarufu kama vidonge vya majira huweza kusababisha mtu kukumbwa na maambukizi ya fangasi hawa.
Lakini pia wale wenye upungufu wa kinga mwilini (HIV/AIDS) nao wana hatari ya kupata magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis na nk.Wengine wanaopata maradhi ni wale waliopata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali au matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi.
Wenye utapiamlo (malnutrition) nao wanaweza kupata tatizo hili.
Wengine wanaoweza kupata ugonjwa huu ni wale wenye tabia ya kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kama nguo za kuogelea (swim wear), chupi zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nailon au zinazobana sana nk.
Lakini wale wanaojamiiana kwa njia ya kawaida kufanya kitendo hicho kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi vyenye glycerin wakati wa kufanya tendo la ndoa wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya maradhi haya.
UCHUNGUZI NA VIPIMO
Kabla ya vipimo vya uchunguzi, mgonjwa atafanyiwa vipimo vya uchunguzi wa uke  kitaalamu huitwa per Vaginal Examination (PV exam) kuona kama kuna uvimbe wowote ndani ya utupu huo au kama ana maumivu wakati wa kujamiiana.
Daktari ataangalia kama kuna uchafu wowote unaotoka, wingi wake, rangi yake, harufu yake, uzito wake na aina ya uchafu unaotoka kama ni sahihi kutokana na maelezo ya mgonjwa.
Kwa kifupi daktari ataangalia mambo mengi kama vile kuna uvimbe wowote wa tezi za sehemu ya siri yaani mitoki, shingo ya kizazi, bartholin glands nk. Ataangalia sehemu ya haja kubwa kama kuna skin tags, bawasiri (haemorrhoids) nk.  Inashauriwa kuwa kabla ya kufanya vipimo, daktari amjulishe mgonjwa aina ya kipimo, lengo lake na jinsi kitakavyofanyika ili kumuandaa kisaikolojia.
Daktari anaweza kuchukua kipimo na kuotesha kwenye maabara ili kuangalia aina ya uoto huo kama ni wa fangasi aina ya Candida albicans, ama la, atafanya kipimo cha mkojo (Urinalysis), na cha ugonjwa wa kisukari, HIV/AIDS, ugonjwa wa  kuvimba tezi la koo (goiter) na kadhalika.

MANUFAA YA KABICHI KIAFYA...SOMA HAPA KUFAHAMU





















Kabichi ni zao linalolimwa mahala pengi sana hapa duniani. Mboga hii imekuwa ikiwekwa katika hadhi ya chini katika mboga, na hata watu huitumia pale tu wanapoona hakuna jinsi ya kupata mboga ya aina nyingine. Na hivyo utaona ikitumika katika sehemu za jumuiya kama vile shule, magerezani na vyuoni kwani gharama yake ni ndogo hivyo huweza kuhimili hali ya kuinunua kwa matumizi ya watu wengi. Mboga hii ina manufaa mengi sana mwilini lakini iwe ni mpya ya kijani/nyekundu au hata zambarau na siyo ile iliyokaa sana sokoni hadi kusinyaa, hiyo haina manufaa. Mboga hii ina faida zifuatazo:

1. AHUENI YA VIDONDA VYA TUMBO

2. HUIMARISHA MFUMO WA MOYO

3. KINGA DHIDI YA SARATANI

4. INAUPA MWILI VITAMINI VIFUATAVYO:
Vitamin K, Vitamin B12, Vitamin B2, Vitamin A na Vitamin C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha kambalishe (fiber) Manganizi (Manganese), Potashiamu (Potassium) na Fatty-3 acids. Vyote hivi ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.
 

UVIMBE KWENYE MJI WA MIMBA (FIBROID)-4

MATIBABU YA UVIMBE KWENYE KIZAZI
Wiki iliyopita tulieleza matatizo ya uvimbe kwenye kizazi. Leo tunafafanua matibabu ya uvimbe kwenye kizazi kwamba hutegemea na vitu mbalimbali kama umri au kama mama ameishawahi kupata ujauzito au kama ni mjamzito.
Mgonjwa akiwa na uvimbe wa kizazi daktari anaweza kuangalia dalili alizonazo, ukubwa wa uvimbe  na sehemu ya uvimbe ulikojitokeza.
Kama mgonjwa yupo katika hali mbaya au kapungukiwa damu basi ataona kama anahitaji kuongezwa  damu bila kuchelewa au mgonjwa mwenye uvimbe kama anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura.
Daktari atamfanyia uchunguzi kujua ikiwa mgonjwa ana maambukizi ya vijidudu kwenye uvimbe au kama uvimbe umejivilinga (torsion) au kama utumbo umejikunja (intestinal obstraction).
Wagojwa ambao wana uvimbe kwenye uzazi wakati huo huo ni wajawazito kwa kweli upasuaji wa kuondoa uvimbe hautakiwi kufanyika.
Wagonjwa walio wengi  wenye uvimbe kwenye kizazi  hawana dalili yoyote hivyo basi, hawapati tiba, pia wale ambao wana uvimbe mdogo huku wakiwa  wameishafunga siku za hedhi, hawahitaji matibabu pia ni lazima daktari achunguze kama hana uvimbe sehemu nyingine ya mfumo wa uzazi.
Mama mwenye ujauzito halafu uvimbe ukajikunja  anaweza akafanyiwa upasuaji  ili kunusuru maisha yake pia uvimbe hautakiwi  kutolewa wakati wa upasuaji wa kumzalisha mama.
Matokeo ya matibabu kama yamefanyika vizuri na kwa wakati unaotakiwa huweza kupunguza ukubwa wa uvimbe kwa zaidi ya asilimia 50 na kuweza kupotea kabisa bila upasuaji kwa asilimia 30 na uvimbe hupotea baada ya miezi mitatu.
Matokeo yake mgonjwa hurudi katika hali yake ya zamani na kama alikuwa na tatizo la kupata mimba basi huweza kupata kirahisi.
Mama anaweza kufanyiwa upasuaji kama anatokwa na damu nyingi au kama uvimbe ni mkubwa sana hivyo hupasuliwa ili kuondoa uvimbe na hupasuliwa tumboni.Ikiwa mgonjwa ana mtoto hupewa dawa za kuondoa uvimbe ikishindikana ndipo upasuaji hufanyika.
MADHARA YA UVIMBE KWA WAJAWAZITO
Madhara ya uvimbe kwenye kizazi ni mtoto kutokaa vizuri kwenye mfuko wa uzazi, kuziba njia za uzazi,   kutokwa damu kwa wingi wakati wa kujifungua na kutokwa damu wakati ana mimba pia kupoteza damu nyingi.
Ushauri:
Ni vizuri kuhudhuria kliniki mara kwa mara kwani uvimbe ni ugomjwa unaotibika hospitali.

Je,kufanya mapenzi ni tiba ya saratani?

Many partners
Kulala na wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo,kulingana na utafiti.
Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal wamebaini kwamba ikilinganishwa na wanaume walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa kupatikana na ugonjwa huo kwa asilimia 28.
Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo kati yao Wanaume 1,590 walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti mwaka 2009.
Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye saratani ya kibofu cha mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa familia zao wenye saratani.
Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha yake,tisho la kupata ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia 19 kwa aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani

UVIMBE KWENYE MJI WA MIMBA (FIBROID)-3

Uvimbe huweza pia kukandamiza viungo jirani na uzazi (pressure effets) ambapo mirija ya mkojo na kibofu cha mkojo na utumbo mkubwa wa haja kubwa na uvimbe unaweza kusababisha usipate choo(consipation) wakati mwingine huweza kusababisha mkojo usitoke (urinal retention), dalili zingine ni kama kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspararemia), uchafu sehemu za siri na kushindwa kubeba mimba (infertity) asilimia kati ya 27- 40 ya wenye uvimbe hupata tatizo la kutokushika mimba.
Dalili zingine ni kutokwa au kuharibika mimba (spontaneous abortion), hii hutoka kwa wagonjwa kati ya asilimia 40 kabla ya kutoa uvimbe na asilimia 20 baada ya upasuaji wa kutoa uvimbe.
Vipimo
Vipimo muhimu kujua au kutambua  uvimbe kwenye kizazi ni kama vile mgonjwa anapohudhuria hospitali  anavyopimwa tumboni (bimanual pelvic examination).Vipimo vya mahabara ni kama  kujua wingi wa damu ili kujua  kama mgonjwa amepungua damu (andemia) na aina ya pili ni upimaji kugundua kama mtu husika ana upungufu wa madini ya chuma (iron defficienty).
Vipimo vya damu kujua kama mgonjwa amepata maambukizi  kwenye uvimbe, tunapima ESR kuona kama imepanda.Vipimo vingine Ultasound husaidia  kugundua aina ya uvimbe na kutofautisha kama mgonjwa ana ujauzito au ni uvimbe pekee.
Vipimo vingine ni kama dawa kupitishwa kwenye mirija na baada ya hapo kupigwa x-ray  pia husaidia kugundua kama uvimbe uko ndani.Vipimo vingine ni kama MRI hivyo ni vya uhakika zaidi na ni uhakika  kwani hujua ukubwa wa uvimbe na madhara yake, vipimo vingine kama IVP husaidia kuona kama uvimbe umeenea kwenye mfumo wa mkojo hasa kibofu cha mkojo.
Kipimo kingine ni HYSTROSCOPY hiki husaidia kugundua na kuondoa  uvimbe kama aina ya subrmucous myoma.Magonjwa yanayofanana na uvimbe kwenye kizazi (differential diagnosi) mara nyingi ni muhimu na husaidia kutofautisha na ujauzito pia kutofautisha uvimbe mwingine  kwenye maeneo ya mfumo wa kizazi, pia kutofautisha na saratani ya mfuko wa mayai (avarian cancer).
Itaendelea wiki ijayo.

WAREMBO MPOOOO..!!! HAYA NDIYO MADHARA YATOKANAYO NA NGUO ZA KUBANA (SKIN TIGHT)...SOMA HAPA KUYAJUA


Nguo za kubana

                        Nguo za kubana

KADIRI siku zinavyokwenda kumekuwapo na ugunduzi wa vitu mbalimbali vinavyochangia kuleta mabadiliko katika jamii. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa hasi au chanya kutegemea na aina ya  bidhaa iliyogunduliwa na matumizi yake. Zipo bidhaa zinazoonekana kuwa na matokeo ya haraka na mazuri baada ya kutumika, lakini wakati huo huo kuwa na madhara kiafya kwa mtumiaji.
Nchi nyingi zinazoendelea hasa zilizopo barani Afrika ikiwamo Tanzania zimekuwa ndizo waathirika wakubwa wa bidhaa zinaotajwa kuwa na madhara huku vijana wakiwa ndiyo kundi kubwa linaloathirika. Sababu za kundi hilo kuathirika zaidi ni kutaka kwenda na wakati kwa kujaribu kutumia kila bidhaa zinazotoka nje ya nchi bila kujua madhara yake.
Miongoni mwa bidhaa hizo ni nguo za ndani zilizoundwa maalumu kwa ajili ya kupunguza unene, pia kutengeneza umbile la mvaaji katika mwonekano wenye mvuto aupendao. Nguo hizo zimetengenezwa kwa mtindo wa mbano, (Skin tight)ambapo ikivaliwa hubana eneo la tumboni hadi kwenye mapaja na hufanya kazi ya kupunguza unene, zikiufanya mwili kuwa mwembamba kulingana na nguo husika ilivyo.
Licha ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kusaidia kwa kiasi kikubwa watu wengi kupunguza miili yao, utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa nguo hizo za ndani huchangia kwa kiwango kikubwa uwezekano wa mvaaji kupata matatizo ya kiafya.
Utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali wa nchini Uingereza, unaonyesha kuwa uvaaji wa nguo hizo unaweza kumfanya mvaaji kupata maradhi ya mgongo, saratani na kiwango kikubwa cha asidi mwilini.
Mmoja wa wataalamu wa afya katika Hospitali ya The London Clinic, Dk Johnson Wilson, anasema kubana kwa nguo hizo katika eneo la tumbo huzuia mzunguko wa asidi inayozalishwa ndani ya mwili na kuisababisha kupanda juu, badala ya kushuka chini.
Anasema kuwa hali hiyo inatokana na msukomo unaotokea kwenye tumbo, hivyo kusababisha mlundikano wa asidi ndani ya mwili ambayo hupaswa kutoka baada ya kuzalishwa.
“Nguo hii inapovaliwa inatenganisha  eneo la kifuani na tumbo, hivyo asidi inayozalishwa inashindwa kushuka chini na matokeo yake inashia kwenya usawa wa  matiti na kurudi kwenye mrija unaopitisha chakula,”anasema DkWilson.
Kuhusu hatari ya saratani, Dk Wilson anasema kuwa kulundikana kwa asidi katika mrija wa chakula, kunamweka mhusika katika hatari ya kupata saratani ya koo na kinywa.
Anasema kwamba licha ya kuwa siyo watu wengi walioathirika na uvaaji wa nguo hizo, lakini matokea yake huonekana baada ya muda mrefu kutokana muda ambao mhusika atavaa nguo hizo.
“Hatari ipo zaidi kwa wanaovaa nguo hizi mara kwa mara, madhara yake hayawezi kuonekana kwa haraka zaidi, lakini kiafya kuna hatari ya kutengeneza saratani ya koo kutokana na kuzuia asidi na kusababishia irudi na kulundikana kwenye mrija unaosafirisha chakula,”anaonya.
Pamoja na hatari hiyo uvaaji wa nguo hizoi pia unachangia kusababisha ugonjwa wa ngozi unaotokana na mwili kubanwa kupita kiasi, hivyo hewa kushindwa kupita.
Dk Wilson anafafanua kuwa ikifikia hatua hiyo, kuna uwezekano wa kutengeneza mazingira ya bakteria na fangasi kujificha kwenye mwili hivyo kusababisha mvaaji kupata maradhi ya ngozi yaliyo magumu kutibika.
Mtaalamu wa ngozi Dk Sam Bunting anasema, kubanwa kwa ngozi pamoja na joto linalosababishwa na msuguano, vinachangia kuleta madhara makubwa katika mwili wa binadamu.
“Hali hii inasababisha ugonjwa unaofahamika kwa jina la kitaalamu kama Intertirgo, ambao huwatokea watu wanaovaa nguo maalumu za kubana kwa ajili ya kutengeneza maumbile,”anasema.
Nguo hizo pia huchangia kuifanya misuli ya tumbo kuwa dhaifu, kutokana na kubanwa muda mwingi, hata inapoachwa huru inashindwa kuwa na nguvu yake ya kawaida.
“Kwa asili misuli ya tumbo haina nguvu na unapoibana kwa muda mrefu unaisababishia kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi, hivyo hulegea na kuwa  dhaifu zaidi hata inapofunguliwa au kutolewa nguo inayobana,”anasema.
Kwa upande mwingine, mtaalamu wa misuli Dk Robert Shanks anasema kuwa nguo hizo zinachangia pia kusababisha maumivu ya mgongo kwa mvaaji. Anasema nguo hiyo inapovaliwa, kunakuwapo na ugumu kwa viungo vya mgongo kujongea kwa urahisi, hivyo kusababisha maumivu ya mgongo mara kwa mara.
“Viungo na mifupa iliyopo kwenye mgongo inapaswa kujongea, lakini kuibana kupita kiasi kutasababisha kushindikana kwa hali hiyo hivyo mvaaji lazima atakumbana na maumivu ya mgongo mara kwa mara”
Pamoja na madhara hayo, nguo hizi pia huweza kusababisha kizuizi katika mzunguko wa damu kwani mishipa inayotakiwa kufanyakazi hiyo inashindwa, kutokana na maeneo ya tumbo hadi kwenye nyonga yanakuwa yamebanwa.
“Ni vigumu mzunguko wa damu kufanyika vizuri katika maeneo yaliyobanwa kupita kiasi; ni wazi kuwa nguo hizi siyo rafiki, huifanya damu isizunguke inavyopaswa,”anasema Dk Shanks na kuongeza:
“Ikifikia hatua hiyo, kuna dalili mvaaji kuweza kupata maimivu ya miguu kwa kuwa mishipa ya damu iliyopo katika maeneo hayo inashindwa kufanya kazi yake vizuri.”
Kwa upande wake mtaalamu wa masuala ya ngozi nchini Tanzania, Dk Isack Maro, anasema kuwa madhara yanayotokana na uvaaji huo siyo makubwa ikilinganishwa na ripoti ya utafiti unavyoeleza.
“Inawezekana kukawapo uwezekeno wa kupata maradhi ya ngozi kutokana na mwili kubanwa kwa muda mrefu, hivyo jasho kushindwa kutoka na kutengeneza mazingira ya fangasi,”anasema Dk Maro na kuongeza:
“Madhara yapo, lakini siyo kwa ukubwa huo. Inawezekana kuwakumba watu wachache mno kati ya wengi, lakini sidhani kama yanaweza kuwa kwa ukubwa huo.”
  

UNAFAHAMU HILI: ZABIBU NI KINGA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO?? SOMA HAPA



Zabibu au Grapes

Hivi karibuni uchunguzi mpya umeonyesha kwamba kula zabibu au vyakula vyenye zabibu ndani yake kunapunguza shinikizo la damu, husaidia moyo kufanya kazi zake vyema na kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.


Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliotolewa kenye mkutano wa Majaribio ya Baiolojia huko California, zabibu zina uwezo wa kupunguza shinikio la damu, husaidia mwili uweze kuvumilia sukari (glucose tolorance) na kupunguza kiwango cha mafuta aina ya triglycerides mwilini ambayo ni chanzo cha matatizo ya moyo.


Wataalamu wanasema zabibu pia zinaweza kupunguza uvimbe, uharibifu unaotokana na free radicals zinazozalishwa mwilini na shinikizo la moyo.

Kwa ujumla zabibu zinazuia hali inayoitwa Metabolic Syndrome suala ambalo linatokana na mada za phytochemicals zilizoko kwenye matunda hayo.


Metabolic Syndrome ni mchanganyiko wa matatizo ya kitiba ambayo yanaongeza uwezekano wa kupatwa na maradhi ya mishipa ya damu pamoja na kisukari.


Hivyo wataalamu wanatushauri tule zabibu au kuongeza zabibu katika vyakula wanavyokula kila siku, ili tujikinge na ugonjwa wa Metabolic Syndrome, ugonjwa wa moyo na kisukari.

UVIMBE KWENYA MJI WA MIMBA (FIBROID)-2

Naendelea kuelezea dalili  za uvimbe kwenye mji wa mimba ili uweze kuzijua na kuchukua hatua mapema.
Dalili hutegemea  na sehemu uvimbe  ulikojishikiza, ukubwa wa uvimbe na kama mama ana ujauzito, uvimbe  huambatana na kutokuwa  na mpangilio wa hedhi  hii hutokea kwa akina mama asilimia 30 ambapo mama huingia kwenye  siku zake mara mbili kwa mwezi au kutoingia kabisa akifuatiwa na kumwaga damu nyingi wakati wa hedhi ambapo anaweza kupata upungufu wa damu.
UVIMBE KATIKA KIZAZI
Dalili
Dalili za uvimbe kwenye mfuko wa uzazi ni kutokwa na damu kusipokuwa na mpangilio (abnormal uterine bleeding).
Hii huwapata akina mama kiasi cha asilimia 30 na huwa damu inatoka sana au kuendelea kutokwa na damu kwa muda mrefu zaidi ya siku 10 ambapo mgonjwa hupata madhara ya kupoteza madini ya chuma na kusababisha upungufu wa damu (iron deficiency anaemia) wale wenye uvimbe kwenye misuli ya uzazi ujulikanao kama sub mucous myoma wenyewe hupitiliza muda wa kuona siku zao na kutokwa vitone vidogo vya damu
. Kutoka kwa damu hutokana na muingiliano wa mishipa ya damu kwenye uzazi ambapo hukandamizwa  na kusababisha kuta za ndani ya uzazi kutofanya kazi zake vizuri na wale  wenye uvimbe wa ndani ya ukuta wa uzazi (pedunulated submcous) wenyewe hupata tatizo la kutokwa damu mara kwa mara ambapo mgonjwa anaweza kutokwa damu leo halafu ikisimama baada ya siku tatu inatoka tena.
Maumivu ya tumbo husababishwa na kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu ya mfuko wa uzazi na wakati mwingine uvimbe hupata vijidudu (infection)na kuleta maumivu makali ambayo husambaa hadi kiunoni na kwenye miguu.
Itaendelea wiki ijayo.

UCHUNGUZI: MAKALIO MAKUBWA KUNA VINGI NDANI YAKE!! SOMA HAPA



Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.

Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makalio makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.

Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari. 
 
 

Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.
  

Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari.
 Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka. 

Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.
   

UGONJWA WA TUNDU KATIKA MOYO KWA WATOTO

Kama kawaida safu hii huwa tunajadili masuala mbalimbali yanayohusu afya na tiba ili kupata ufahamu zaidi juu ya kuimarisha afya zetu na ya jamii kwa ujumla.
Leo tutazungumzia ugonjwa unaojulikana kama tundu katika kuta za ventrikali za moyo au kwa kitaalamu Ventricular Septal Defect (VSD).
Tatizo hili hutokea mara nyingi ambapo watoto 2-6 kati ya 1,000 uzaliwa nalo.
Tundu katika kuta za chini za moyo au VSD ni pale panapokuwepo na uwazi katika sehemu ya kuta ya septum inayotenganisha chemba za ventrikali zilizo chini ya moyo.
Moyo unapoanza kuumbika huanza kama bomba lililo wazi na kuendelea kujigawa katika sehemu mbalimbali na kuunda kuta.
Iwapo kitendo hicho hakitatekelezwa ipasavyo, hutokea uwazi katika kuta ya septum kwenye chemba za chini.
Kuwepo tundu hilo huruhusu damu yenye oksijeni kupita kutoka chemba ya kushoto ya chini ya moyo na kuingia katika chemba ya kulia ya chini ya moyo, badala ya kuingia kwenye mshipa wa aorta na kuelekea nje ya moyo kama inavyotakiwa.
Tundu la VSD linaweza kuwa dogo, la kati au kubwa. Tundu dogo katika kuta za chini za moyo huruhusu damu ndogo tu kutoka upande mmoja wa moyo kwenda wa pili hivyo haliathiri utendaji wa kawaida wa moyo na kwa kawaida huwa halihitaji matibabu maalumu.
Matundu ya aina hiyo huziba yenyewe wakati moyo unapoendelea kukua kipindi cha utotoni. Matundu yenye ukubwa wa kati na kubwa katika kuta za chini za moyo huruhusu kiwango kikubwa zaidi cha damu kupenya toka upande mmoja wa moyo kwenda mwingine, na mara nyingi huhitaji matibabu maalumu.
Watoto wenye tundu dogo katika moyo, huweza kukua bila matatizo yoyote, wakati wale wenye tundu kubwa huanza kuonyesha dalili mapema.
Vifuatavyo ni vihatarishi ambavyo vinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa na tundu katika kuta za chini za moyo. Mama kuwa na maambukizi ya Rubella katika kipindi cha ujauzito au kuwa na ugonjwa wa kisukari cha wakati wa ujauzito ambao haujadhibitiwa na kuwa mnywaji wa pombe au mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Mjamzito akitumia bila ushauri wa daktari baadhi ya dawa za hospitali katika kipindi cha ujauzito pia huweza kusababisha mtoto azaliwe na tundu katika kuta za chini za moyo.
DALILI
Iwapo tundu ni dogo huwa halina dalili yoyote na pale mtoto anapoendelea kukua tundu hilo hujifunga lenyewe. Lakini tundu likiwa kubwa, japokuwa mtoto anayezaliwa huwa haonyeshi dalili yoyote katika kipindi  hicho lakini baadaye huwa na dalili zifuatazo.
Rangi ya ngozi yake, midomo na kucha hubadilika na kuwa ya bluu, kunyonya au kula huwa kwa shida sana, ukuaji na kupumua kwa shida, kuchoka haraka, kujaa miguu na kuvimba tumbo, kuwa na mapigo ya moyo ya haraka.
Mtoto mwenye tatizo hili anapopimwa na daktari kwa kifaa, huweza kusikia ishara ya ongezeko la sauti ya ziada ya mapigo ya moyo wa mtoto hali ambayo kitaalamu huitwa holosystolic murmur.
Itaendelea wiki ijayo.

NJIA 4 ASILIA ZA KUDHIBITI PRESHA...SOMA HAPA



LICHA ya kusababisha vifo vingi duniani ikiwemo Tanzania, shinikizo la damu (High Blood Pressure), inaelezwa na wataalamu kuwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari ya moyo, kiharusi na figo. Hata hivyo ugonjwa huu unaweza kuzuilika na kutibika kwa njia asilia, mbali na matibabu ya kawaida.
POTASIAMU MWILINI
Ulaji wa mboga na matunda yenye kiwango kingi cha Potasiamu (Potassium) ni sehemu muhimu sana katika mikakati na mipango anayoweza kuwa nayo mtu ya kudhibiti au kushusha kiwango cha shinikizo la damu alichonacho, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Profesa wa Tiba za Kinga, Dk. Linda Van Horn wa Chuo Cha Tiba cha Feiberb.
Profesa huyo anasema kuwa ulaji wa Potasiamu kati ya miligramu 2000  na 4000 kwa siku kutasaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa. Vyakula vinavyoaminika kuwa na kiwango kingi cha Potasiamu ni viazi vitamu, maharagwe, nyanya, juisi ya machungwa pamoja na karanga na korosho.
KUWA MAKINI NA CHUMVI
Baadhi ya makundi ya watu yanayougua ugonjwa wa shinikizo la damu, ulaji wa chumvi kiasi chochote huwa na athari mbaya kwao, hasa wale wenye historia ya kifamilia ya kuugua ugonjwa huu.
Kwa kuwa siyo rahisi mtu mwenye shinikizo la damu kujitambua kama chumvi ina muathiri zaidi, inashauriwa kila mtu kupunguza matumizi ya chumvi katika vyakula vya kila siku.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya lishe ya moyo na mapafu, Dk. Eva anasema kuwa kiwango cha chumvi cha wastani anachotakiwa kutumia mtu kwa siku kisizidi miligramu 1,500. Kipimo hicho ni zaidi kidogo ya kijiko kimoja cha chai ambacho huwa na miligramu 1200. Kwa maana nyingine, matumizi ya mtu kwa siku nzima katika milo yote hayatakiwi kuzidi kijiko kimoja na nusu cha chai.
ULAJI WA CHOKOLETI
Aina nyingi za chokoleti (Chocolate) zina aina ya kirutubisho (flavanols) kinacholainisha mishipa ya damu na kuwezesha damu kutembea vizuri mwilini. Katika utafiti mmoja, asilimia 18 ya wagonjwa wa presha waliokula chokoleti walionesha kupata ahueni kwa presha kushuka. Kiasi cha chokoleti moja kinatosha kwa siku, muhimu iwe inayotengenezwa kutokana na Cocoa.
TATIZO LA KUKOROMA USIKU
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Alabama nchini Marekani, watu wengi wenye tatizo la kukoroma usiku, wana homoni ijulikanyo kama ‘aldosterone’ ambayo huongeza shinikizo la damu na inakadiriwa kuwa nusu ya watu wote wenye tatizo la kukoroma wana presha.
Mbali ya kukoroma kama dalili moja wapo ya kuwa na presha kwa baadhi ya watu, kusikia uchovu sana na kizunguzungu asubuhi nako ni dalili moja wapo, hivyo inashauriwa kumuona daktari akushauri kuondoa tatizo la kukoroma ili kujiepusha na matatizo yatokanayo na shinikizo la damu.
Kama hujui hali yako kuhusu  presha, ni vyema ukamuone daktari na kupima sasa.
 

JOHARI ATOA SOMO LA UZAZI NA NDOA KWA WASANII WENZAKE WA KIKE



SOMO! Staa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’, ametoa somo kwa baadhi ya wasanii wa kike ambao wamekuwa wakijibweteka na kushindwa kudumisha upendo kwa wapenzi wao baada ya kujifungua.
Staa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Johari alisema miongoni mwa vitu ambavyo huwashushia upendo wanawake wengi ni uchafu baada ya kuzaa na kujikita na malezi kuliko kuwathamini wapenzi wao ndiyo maana ameamua kutoa filamu ya Mke Mchafu inayowagusa mabinti.
“Ujue kuna watu wanavunja ndoa zao kwa mikono yao wenyewe kutokana na mambo kama haya na wapo hata wasanii ambao wanafanya haya mambo, yaani mtu unaingia kwenye nyumba hutamani hata kuomba maji ya kunywa, nafikiri watabadilika kupitia filamu yangu itakayotoka soon,” alisema Johari.
    

TUZUNGUMZIE AFYA: MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO KWA WANAWAKE/WANAUME



LEO tuangalie tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo (Urinary disorders) kwa wanawake na wanaume.
Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa simple cystitis au Bladder infection na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa pylonephritis au kidney infection.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli. Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.
Lakini watu wengine wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi japokuwa kuna visababishi vingine vichache.Bakteria wa Escherichia coli hawapo peke yao huambatana na waitwao staphylococcus, saprophyti cus, pseudom onas, enterobacter n.k.
Maambukizi katika njia ya mkojo  lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo  na si pengine popote. Wapo wanawake wamekuwa wakiniuliza kuhusu tatizo la kutokwa na uchafu ukeni na kudhani ni ugonjwa huu, huo ni ugonjwa tofauti kabisa na huu tunaouchambua leo.
Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo, tuna maana ni kutoka eneo la nje la utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalamu huitwa Lower Urinary Tract Infect na ikihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.
Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake hutokea wakati wa kujisafisha, kutonawa vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani chafu. Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bakteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi.
Upungufu wa homoni ya kike iitwayo Oestrogen husababisha bakteria wasababishao maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi.Matatizo haya ya maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake, huwakumba pia watoto wadogo kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi, njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani.
Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao hupata maambukizi rahisi kutokana na viungo vyao vya uzazi kuwa vifupi na wanaponawa maji yasiyo salama kwa watoto wa kiume huwa rahisi bakteria kubaki katika ngozi inayoning’inia (govi), hivyo kusababisha tatizo hili.
Lakini pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambuzi kutokana na sababu ambazo tumezitaja hapo juu ambapo pia ni rahisi kwao kuambukizwa Ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana tunasisitiza tohara kwa wanaume.
Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo zaidi ni bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kusafiri kwa bahati mbaya  na kujikita katika mfumo wa mkojo. Bakteria wengine waambukizao njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia na trimonas na fangasi wanapojamiiana bila kutumia kinga.
Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo, mara kwa mara, ni vema kutumia kinga yaani kondomu na kwa mwanamke kila anapomaliza kufanya ngono akojoe ili kuondoa bakteria walioingia au waliokaa katika tundu ya mkojo wakisubiri kuingia.Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu, unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha huchangia tatizo hili.
Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo hata ndani ya kibofu pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.
Dalili
Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa, mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali japokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo au wengine huita UTI yaani urinary tract infection wana ugonjwa huu.
Dalili nyingine za maambukizi ni maumivu,  kutokwa na usaha au majimaji wakati wa kukojoa kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi moto wakati wa kukojoa mkojo.
Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Wengine wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo, au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.Mgonjwa anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu, kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili kuonesha kushoka.
Wagonjwa wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu  ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi.Matatizo haya ya mfumo wa mkojo kama tulivyoona huko juu huwapata watu wote wanawake na wanaume. 
Watu wenye  matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI. Kwa wanaume huhisi hata nguvu za kiume kupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo la ndoa.
WAJAWAZITO
Kwa wajawazito ugonjwa unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni. Bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhara mengine kama vile  shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo.
TIBA
Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin, Fosfomycin, Monurol, Furadantin, Sulfam ethoxazole, co-trimax, ampicillin, gentamicin na kadhalika lakini usitumie dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.
Ushauri
Tunashauri kwa mwanamke kwamba epuka kujisafisha sehemu za siri na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.
Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo.
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi.
Kwa mwanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kujipenyeza hadi katika korodani na huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kukufanya uwe mgumba.
Maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume (prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi. Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.
   
Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top