Straika wa Simba, EmmanuelOkwi.
Na Martha MbomaWAKATI kikosi cha Simba kikiendelea na maandalizi yake nchini Afrika Kusini, mapya yameibuka baada ya kudaiwa kuwa, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakikerwa na tabia ya straika Emmanuel Okwi kujiona bora zaidi ya wengine huku wakidai kuwa uongozi umekuwa ukimthamini zaidi ya wengine, kitu ambacho kinawapunguzia morali.
Taarifa zinadai kuwa, kwa wachezaji wengine hali imekuwa mbaya zaidi kiasi cha kufikia hatua ya kumnyima pasi uwanjani kwa makusudi, suala ambalo linaigharimu timu.
Simba haijapata ushindi wowote katika michezo mitatu ya awali ya Ligi Kuu Bara. Imetoka sare yote dhidi ya Coastal Union, Polisi Moro na Stand United. Lakini imedhamiria kuanza kushinda mchezo unaofuata dhidi ya Yanga Oktoba 18.Uongozi wa Simba hautaki kusema chochote kuhusiana na hilo, hasa ikizingatiwa kwamba umeelekeza akili yote kwenye mechi ya watani wa jadi, Oktoba 18.
Lakini chanzo cha kuaminika ndani ya kikosi cha Simba, kimeliambia Championi Jumatatu kuwa, wachezaji wa klabu hiyo wamegawanyika katika makundi kutokana na baadhi yao kujiona ndiyo bora kuliko wenzao wakati wote huku Okwi akidaiwa kuwa mmojawao.
Chanzo hicho kilidai kuwa, wachezaji kama wanne ambao wamekuwa wakipata nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza, wamekuwa wakimnyima pasi makusudi Okwi kutokana na tabia yake, jambo ambalo linaigharimu timu kwa kiasi kikubwa.
“Wachezaji wanakuwa kama wameweka kamgomo fulani kutokana na kutoridhishwa na tabia ya mchezaji mwenzao kuwaletea dharau wakati wao ni kitu kimoja na wapo klabu moja.
“Ndiyo maana baadhi yao wamekuwa hawampi ushirikiano anapokuwa uwanjani na kutoshirikiana, zaidi ni kipindi kile timu ilipokuwa ikiweka kambi Zanzibar, yeye alikuwa akipandishwa ndege wakati wengine wakipanda boti, hiyo ndiyo ilileta shida kabisa,” kilisema chanzo.
Championi lilifanya juhudi ya kuwatafuta viongozi wa klabu hiyo ili kuthibitisha suala hilo. Katibu wa timu hiyo, Steven Ally, alisema suala hilo limezushwa tu na halina ukweli wowote kwa sababu wao kama uongozi hawajapata taarifa rasmi kuhusu suala hilo.
Alipotafutwa Makamu wa Rais, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokewa lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Pope ambaye yupo nje ya nchi kwa shughuli binafsi, hakutaka kulizungumzia suala hilo kwa undani, badala yake alipobanwa alisema kwa ufupi: “Siyo kweli.”
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >