Habari Kali
Loading...

Maximo apumzisha silaha zake hatari, kisa Simba

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >


Kocha mkuu wa Yanga, Marcio Maximo.
Goodluck Ngai na Said Ally
WACHEZAJI wa kimataifa wa Yanga, kiungo Andrey Coutinho na mshambuliaji Geilson Santos ‘Jaja’, wamepunguziwa muda wa kufanya mazoezi na kocha wa timu hiyo, Marcio Maximo ili kuwaepusha kupata majeraha katika kipindi hiki cha kuelekea pambano lao dhidi ya mahasimu wao Simba litakalopigwa Jumamosi ijayo.
Wachezaji hao waliotua Yanga hivi karibuni wakitokea Brazil, watacheza kwa mara ya kwanza mchezo wa watani wa jadi, huku presha ikiendelea kuwa kubwa.
Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijjini Dar, juzi, Maximo aliwatumia wachezaji hawa lakini baada ya muda mfupi akawatoa na kuwapa mazoezi mengine, ikiaminika kwamba ni katika jitihada za kuhakikisha hawapati majeraha yoyote kabla ya Jumamosi.
Kwenye mazoezi hayo, kocha huyo aliwachezesha wachezaji wake wa timu kubwa mechi dhidi ya wale wa Timu B ila wachezaji wanaoaminika kuanza katika mchezo huo wa mwishoni mwa wiki hawakutumika kwa muda mrefu.
Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza waliopunguziwa muda wa mazoezi kuepuka majeraha ni Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga, Hussen Javu na Hamis Kiiza.
Wakati huohuo, Maximo amebadili mfumo wake wa uchezaji. Badala ya kutumia mshambuliaji mmoja kama alivyofanya katika mechi zake za awali, kwa sasa katika mazoezi yake anaonekana kutumia washambuliaji wawili, yaani badala ya mfumo wa 4-5-1, kwa sasa Yanga inajifua ikitumia 4-4-2.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top