Habari Kali
Loading...

MAAJABU YA MTOTO KUFUFUKA

Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
MAAJABU! Mtoto Irene Emmanuel Joseph (1) mkazi wa Kibamba-Mji Mpya jijini Dar, ameendelea kuwa gumzo kufuatia kufariki dunia Agosti, mwaka jana akiwa na miezi 9 na kudaiwa kufufuka katika mazingira ya ajabu hivi karibuni akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi minne, Uwazi linakuletea.
                                     Mtoto Irene Emmanuel Joseph baada ya kufufuka.
UWAZI KAMA KAWAIDA YAKE
Tukio la kupatikana kwa mtoto huyo akiwa hai lilitikisa Jiji la Dar, Jumamosi iliyopita ambapo umati ulifika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo ili kumshuhudia kwa macho.
Kama ilivyo ada, Gazeti la Uwazi ni kuchimba kwa kina matukio yenye kuishangaza na kuisikitisha jamii. Nalo lilifika nyumbani hapo kwa lengo la kukusanya taarifa kwa undani ili kuwapelekea wasomaji wake.

MAZINGIRA YA KIFO CHAKE
Akizungumza na gazeti hili nyumbani hapo, mama mzazi wa mtoto huyo, Helena Raphael alisema kuwa, ilikuwa Agosti mwaka jana akiwa kwenye eneo la biashara yake, Mbezi Mwisho, Dar, Irene aliugua ghafla. Alionesha kulegea na kuwa kama mtoto mwenye degedege.
“Nilimwambia mume wangu, tukampeleka kwenye zahanati moja iliyopo palepale Mbezi ambapo daktari akabaini kuwa tatizo la mwanangu ni kubwa hivyo akatushauri tumkimbize Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Pwani ambapo iligundulika kwamba alikuwa na upungufu mkubwa wa  damu.
“Pale hospitali madaktari walianza kutafuta mishipa ili wamchome kwa lengo la kumwongezea damu lakini cha ajabu mishipa ya mwanangu ikawa inavimba tu. Ilipofika saa 6 usiku, alifariki dunia bila kuwekewa damu. Nililia sana kama mzazi!”
Irene Emmanuel akiwa na baba'ke.
MAITI YAMDUWAZA MAMA MTU
“Baada ya kifo, sikuwahi kuuona mwili wa mwanangu maana waliupeleka mochwari. Siku ya kuaga mwili hapa nyumbani kwa ajili ya mazishi, nilishangaa sana kumwona mwanangu ana alama ya duara kwenye shavu kama zile alama za Wamasai.
“Niliwasimulia baadhi ya waombolezaji wakasema kwa upande wao waliuona mwili wa mwanangu ukitoka jasho jingi kama mtu aliyetoka kufanya kazi ngumu juani na ulivimba sana,” alisimulia mama huyo na kuongeza:
“Pamoja na hayo, tulimzika mwanangu  kwenye makaburi yaliyopo hapahapa Mji Mpya huku tukiwa na shaka juu ya  kifo chake.”
MAMA AANZA KUZUNGUKA MAKANISANI
Helena anasema baada ya mazishi, alianza kwenda kwenye makanisa mbalimbali kumwomba Mungu amrejeshe mwanaye na mwishowe akajikuta amefika kwenye kanisa la Nabii Flora lililopo Salasala, Dar ambako aliambiwa mtoto wake alikuwa hai.
“Nilikuwa naenda kusali kila siku ndipo siku moja Nabii Flora alinifuata na kuniambia mwanangu hajafa alikuwa yupo sehemu lakini nguvu zake haziwezi kumrudisha tena.
“Kuna dada mmoja pale kanisani alisikia Nabii Flora akiniambia hivyo, aliniita pembeni na kuniambia kuna mganga mmoja Dodoma ana uwezo wa kumrudisha mtu aliyekufa kimazingara, akanipa namba zake nikamwambia mume wangu na kuanza kuwasiliana naye.”Irine siku chache kabla hajafariki.
MGANGA ADAI AMEMPATA MTOTO
“Siku ya kwanza kumpigia simu huyo mganga alituambia tushike shilingi mia moja mkononi, tukafanya hivyo, akasema kweli mtoto wetu yupo hai na atamrudisha. Siku chache mbele tulimtumia hela alizotuagiza na akatuambia tusafiri kwenda Dodoma tukamchukue mtoto wetu kwani tayari alishampata.”

WAZAZI WAONANA NA MTOTO
Helena anasema kuwa, Februari mwaka huu yeye na mume wake walisafiri mpaka Dodoma eneo la Pandambili na kuonana na mganga huyo akiwa na mtoto wao ambaye alionekana kutokuwa na afya nzuri. Walitakiwa wamuache kwa muda ili aendelee na matibabu mpaka arejee kwenye hali ya kawaida.

MGANGA ATINGA DAR NA MTOTO
“Baada ya miezi miwili kupita mganga alitutaarifu kuwa anakuja Dar na mtoto. Kweli, alifika hapa usiku wa Aprili 10 akiwa na mtoto wetu ambaye kwa sasa ni mzima kabisa.
“Tuna furaha sana kuonana na mwanetu tena haya kweli ni maajabu ndiyo maana watu wengi wamefika hapa kushuhudia na wengine wamelala hapahapa tangu jana,” alisema mama huyo.


Hili ni kaburi la mtoto Iline.
MGANGA ANENA
Naye mganga aliyedai kumfufua mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Bino alikiri kupokea simu kutoka kwa wazazi hao na kusema:
“Niliongea na mizimu ikaniambia mtoto yupo hai katika mazingira ya kawaida ila alichezewa kimazingara. Nimewasaidia wengi tu na ninao watu wengi niliowarudisha huko Dodoma,” alisema mganga huyo.

MJUMBE ATHIBITISHA KUZIKWA KWA MTOTO HUYO
Mjumbe wa mtaa huo, Maimuna Abdallah alithibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mtoto Irene, Agosti mwaka jana na kuongeza kuwa yeye ndiye aliyetoa barua ya utambulisho wa makazi kwa baba mzazi wa mtoto huyo ili aweze kupatiwa mwili wa mwanaye kutoka Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya mazishi.
“Na mimi nimeshangazwa sana na tukio hili kwa sababu tangu nizaliwe sijawahi kusikia wala kuona mambo haya, niwaambieni tu kuwa kweli yametokea mtaani kwangu,” alisema mjumbe huyo.

MAJIRANI WAO
Baadhi ya majirani na wazazi wa Irene waliliambia Uwazi kwamba, japokuwa mtoto huyo alifariki dunia mwaka jana na kuzikwa lakini walivyomwona wao ni yeye yule waliyemzika!
“Yaani hakuna shaka kabisa kwamba huyo mtoto ni Irene mwenyewe, sijui nini kilifanyika lakini kusema kweli ni mwenyewe na kweli kifo chake kiliacha maswali hapa mtaani,” alisema jirani mmoja.

Majirani wakiwa kwenye tukio hilo.
UWAZI LATINGA KABURINI
Ili kuthibitisha kuzikwa kwa mtoto huyo, gazeti hili lilifika kwenye kaburi alilozikwa mtoto Irene mwaka jana na kulikuta limeshaota majani huku mchwa wakiwa wameanza kuutafuna msalaba sehemu ya chini.
Msalaba huo ulisomeka hivi; IRENE EMMANUEL, KUZALIWA 01/10/2013. Hata hivyo, sehemu yenye tarehe ya kifo ndiyo ililiwa na mchwa.

MPANGO WA KULIFUKUA KABURI
Baba mzazi wa Irene alipoulizwa kama wana mpango wa kulifukua kaburi alilozikwa binti yake, alisema hawajafikiria hilo.

KWA SASA IRENE
Kwa sasa, mtoto Irene yuko kwa wazazi wake huku mganga huyo akisema ataendelea kumpatia dawa mpaka atakapoimarika zaidi na kuendelea na makuzi.

MWANAMKE MWENYE ‘MAHIPS’ MAKUBWA AINGIA KATIKA KITABU CHA KUMBUKUMBU ZA GUINNESS

Mikel Ruffinelli ndiye mwanamke anayejulikana rasmi kuwa na ‘mahips’ makubwa zaidi duniani.


MIKEL RUFFINELLI ndiye mwanamke mwenye ‘mahips’ (nyonga au makalio) makubwa zaidi duniani hivi sasa na ameingia katika Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia cha Guinness.  
Mikel Ruffinelli akiwa katika pozi.
Mama huyo ambaye ni Mmarekani, anasema anajisikia raha mustarehe na umbo lake hilo alilo nalo.
Ruffinelli ambaye ni mama wa watoto wanne, mkazi wa Jimbo la California, Marekani, anasema anaishi maisha ya kawaida na kuendesha kazi zake vizuri ambapo mumewe, Reggie Brooks, pia humsifia kwamba anampenda jinsi alivyoumbika.
Akiwa amepozi na mumewe, Reggie Brooks.
Kwa mujibu wa gazeti la ‘WorldWide Werid News’, Ruffinelli alikuwa na umbo la kawaida kabisa wakati wa ujana na hakuwa na tatizo lolote la kuongezeka uzito, lakini, akiwa na umri wa miaka 22, alianza kuona ‘mahips’ yake yanazidi kuongezeka baada ya kuzaa mtoto wake wa kwanza.
Aliongeza kusema kwamba kila alipokuwa anazaa, sehemu yake hiyo ya mwili ilizidi kuongezeka mpaka akawa anashindwa kupita kwenye mlango wa kawaida.  Japokuwa kiuno chake kina inchi 40 (sentimita 102), nyonga zake zinafikia inchi 100 (sentimita 254), hali inayomfanya avunje rekodi ya dunia.
Pamoja na kwamba watu humshangaa kila anapopita na humwomba kupiga naye picha za kawaida na za video kutokana na umbo lake hilo, bado hujisikia mwenye furaha.
Anasema: “Ninapotembea mitaani, watu hunipiga picha za kawaida na za video kutoka kwenye simu zao.  Watu wengine hufikiri kwamba nilifanyiwa upasuaji ili kuupa mwonekano wa kupendeza mwili wangu, lakini ukweli ni kwamba umbo hili ni la asili.”
Ruffinelli hana mpango wa kupunguza unene wake, lakini anakiri kwamba umbo lake hilo humfanya  nyakati fulani akate tiketi  za viti viwili anaposafiri kwenye ndege, kwani kiti kimoja hakimtoshi.
Umbo lake humlazimu kupita kiubavu katika milango mbalimbali na huwa hawezi kufunga mlango wa bafu lake wakati akioga kwani sehemu ya mwili wake huwa imejitokeza nje.

WANAUME WAENDA HOSPITALI NA KUWEKEWA DAWA ILI WAPATE UCHUNGU KAMA WA MWANAMKE ANAPOJIFUNGUA



Jamaa VKuna vioja tumekuwa tukivisikia sehemu mbalimbali duniani, na bado vingine vinaendelea kuibuka siku baada ya siku.
Leo hii kuna stori mpya ambayo imenifanya niendelee kuweka kumbukumbu kichwani kuhusu matukio makubwa na ya ajabu yaliyowahi kujitokeza China.
Tumekuwa tukisikia kuhusu matukio ya wanaume mbalimbali wakifanya operation za kubadili maumbile ya jinsia zao, hii ya leo kutoka China inahusu wanaume ambao waliamua kujitolea kufanyiwa majaribio ya kufungwa vifaa ambavyo vitawafanya wapate maumivu ambayo huwa anayapata mama mjamzito wakati wa kujifungua.
Hizi ni baadhi ya picha za jamaa hao wakiwa katika zoezi hilo katika jimbo la Shandong, China.
Jamaa I
Jamaa II
Jamaa III
Jamaa IV
Jamaa IX
Jamaa V
Jamaa VII
Jamaa VIII
  

MAAJABU...!! KUTANA NA MTOTO WA MIAKA 3 MWENYE UZITO WA KILO 70...!!


Meet a three-year-old boy who apparently weighs 70 kg and can not stop gaining weight, Cachoeiro de Itapemirim, Espirito Santo, Brazil.
Misael weighted 2.9kg when he was born
Misael weighed 2.9kg when he was born but every month since then, he has gained approximately 3 kilograms. The poor boy, who is supposedly suffering from Prader–Willi syndrome, now weighs 70kg and is struggling to walk.
Prader–Willi syndrome symptoms include constant craving for food and rapid weight gain
Classic signs and symptoms include constant craving for food and rapid weight gain. Misael eats frequently and consumes large portions and even then he still feels hungry. The boy also has serious behavioural problems and his parents have to hire a private taxi to transport the boy to a local hospital.
The boy also has serious behavioural problems such as stubbornness and hysteria
While syndrome itself is not life threatening, the compulsive eating and resulting weight gain can be. That is why restricting a child’s diet is a particularly important part of managing their condition. 
“And when we walk down the street, people stop, want to take pictures with him, people say that they never saw a boy this size.”
According to Misael’s father, when the boy and his parents walk down the street, people stop, want to take pictures with him. People say that they never saw a boy this size and want to know how old he is, how much he weighs. 
Although there is no cure for Prader-Willi syndrome, treatment aims to manage such symptoms as  a permanent feeling of hunger, which can easily lead to dangerous weight gain, reduced muscle tone, learning difficulties and behavioural problems
   

MAAJABU...!! WAMZIKA BABU YAO AKIWA AMEKAA HUKO KENYA...TAZAMA PICHA ZA JENEZA HAPA



Jeneza la KitiKuna taarifa ambazo kama ukibahatika zikakufikia, zinaweza kukuacha kinywa wazi ama kukushtua kwa namna fulani.
Stori ambayo nimeipata hivi punde kutoka 254 Kenya inahusiana na mazishi ya aina yake ambapo familia moja imefanya mazishi ya mzee wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Adriano Aluchio anayetajwa kuwa mzee wa kuheshimika kwenye jamii hiyo akiwa amekaa ndani ya jeneza lilichongwa kwa namna ya kipekee tofauti na ilivyozoeleka.
Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wamesema ni utamaduni wa jamii ya kabila la Lughia kufanya mazishi ya namna hiyo kwa mzee aliyeheshimika, kwa imani kuwa amefariki lakini anaendelea kuwalinda watoto wake pamoja na jamii yake.
Moja ya wazee katika jamii hiyo amenukuliwa akisema, “Mazishi kama hayo ya kumkalisha marehemu yalianza tangu zamani sana wakati wa mfalme Nabongo Mumia, na sisi tulitokea katika jamii hiyo, tukimzika amelala hatoridhika… Ataonekana akitembea huku juu….”
Baada ya mazishi hayo ya kipekee, walichukuliwa ng’ombe dume wawili na kupiganishwa juu ya kaburi kama njia ya kufukuza mapepo wachafu, huku wanakijiji wakipongeza kitendo cha mzee huyo kupewa mazishi ya hadhi.
Jamii ya Waidakho katika kabila la Walughia wanoishi katika kaonti ya kakamega wanajulikana sana kwa mchezo wao unaowavutia watalii eneo hilo la kuwapiganisha Fahali na kuku Jogoo.
  

MAAJABU..!! HII NDIYO HISTORIA YA MTOTO WA MIAKA 5 ALIYEBEBA UJAUZITO NA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME NCHINI PERU....



World's Youngest Mother LINA akiwa amelezwa mara baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji. 


























LINA MEDINA
 
LINA AKIWA MJAMZITO.
  
LINA AKIWA NA MTOTO NA MMOJA WA MADAKTARI WALIOMFANYIA UPASUAJI NA KUJIFUNGUA MTOTO HUYO KATIKA KITANDA CHA WATOTO CHA MATAIRI MANNE.

LINA Medina aliyezaliwa tarehe 27 Sept. 1933, huko Ticrapo, mkoa wa Huancavelica, nchini Peru, anatajwa kua Mama mwenye umri mdogo kuwahi kutokea katika historia ya Ulimwengu.

Tarehe 14 Mei 1939 Lina akiwa na umri wa miaka 5 na miezi 7, alijifungua mtoto wa Kiume aliy
e mpa jina la Gerardo Medina.

Ilianzaje?
Mwanzoni mwa mwezi Machi 1939 wazazi wa Lina ~ Tiburelo Medina na Victoria Losea waliamua kumpeleka Hospitali baada ya kuona tumbo likiongezeka kupita kiasi.

Wazazi wa Lina walidhani huenda ana uvimbe tumboni, lakini madaktari waligundua kua alikua ana ujauzito wa miezi 7.

Dr. Gerardo Lozada aliamua kumpeleka Lina kwa wataalam zaidi nao wakathibitisha kua ni kweli alikua mja mzito.

Alizaaje ?.
Mwezi mmoja na nusu baada ya kupelekwa hospitali kwa mara ya kwanza, Lina alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji, kutokana na njia yake ya uzazi kua ndogo.

Upasuaji ulifanywa na Dr. Lozada, Dr. Busalleu, na Dr. Colareta.

Alivunja Ungo lini?.
Dr. Edmundo Escomel alitoa ripoti kamili juu ya kesi ya Lina kupitia jarida maalum la maswala ya kiafya na matibabu liitwalo La Presse Médicale.

Ripoti hii ilibainisha kwamba Lina alianza kupata siku zake tangu akiwa na umri wa miezi 8, alitofautiana na ripoti ya awali iliyosema kua amekua akiona siku zake tangu alipokua na umri wa miaka 3.

Ripoti hii pia ilisema kua Lina alianza kuota maziwa akiwa na umri wa miaka 4, alipofikisha miaka 5 nyonga yake ilikua imesha tanuka.

Alizaa mtoto gani ?.
Mtoto alizaliwa na uzito wa kilo 2.7 na alipewa jina la daktari wake Gerardo.

Gerardo alilelewa akijua kwamba lina ni dada yake lakini alikuja kujua ukweli akiwa na umri wa miaka 10.

Gerardo aliendelea kukua akiwa mtoto mwenya afya njema lakini alifariki mwaka 1979 akiwa na miaka 40 kwa ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalam la Bone marrow.

Nani Baba wa mtoto ?.
Lina hajawahi kumtaja baba wa mwanae wala mazingira yaliyopelekea yeye kupata mimba.

Dr. Escomel alipendekeza kwamba inawezekana hata Lina mwenyewe alikua hajui, na kusema kuwa hakutoa majibu yanayojitosheleza.

Tuhuma kwa baba mzazi:
Hata hivyo Baba mzazi wa Lina alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Unyanyasaji wa kingono wa mtoto (Child Sexual Abuse) lakini aliachiwa baadae baada ya kukosekana ushahidi wa kutosheleza.

Na hivyo basi Baba halisi aliyempa mimba Lina hakuwahi kujulikana.

Maisha ya Lina baadae:
Miaka kadhaa baadae Lina aliolewa na Raúl Jurado ambaye mwaka 1972 walipata mtoto wa kiume.

Lina yupo hai mapaka sasa na anaishi maisha ya kimasikini huko Lima nchini Peru
   

MAAJABU: MTI ULIOANGUKA NA KUCHOMWA MOTO MIAKA 3 ILIYOPITA WASIMAMA GHAFLA




NI MAAJABU MKOANI TABORA,WILAYA YA UYUI,KATA YA UFULUMA KIJIJI CHA MFUTO..Ni mti ulioanguka na kuchomwa moto miaka 3 iliyo pita sasa wainuka na kusimama  wananchi wakaamua kuukata na kuchukua vipande vya mti huo kwa imani za kishirikina {kizimba}.Na maajabu mengine yakatokea ulipomalizwa mti na kubaki shimo ndani ya shimo pakawa na vitu vya thamani kama pesa nyingi,pingu za mjerumani n.k.Vilivyotumiwa na watu wa zamani.Watu wakachukua na kufanya shimo hilo kubaki jeupe,na hapo ndipo shimo hilo lilipoamua kuanza kulia kama binadamu.
  

MTOTO WA AJABU AIBUKA DAR, ATOA ELIMU AKHERA NA DUNIA

Mtoto Salim akitoa elimu kwa wananchi.
Umati wa wakazi wa Temeke wakiwa makini kumsikiliza mtoto huyo.
UMATI wa wakazi wa Temeke jijini Dar, jana walikusanyika kumshangaa mtoto, Salim mwenye umri wa mika 13 kufuatia uwezo wake wa kujua mambo mbalimbali sambamba na kutoa elimu akhera na dunia.

WAZUNGU WAMEDATA..!! SHINDANO LA KUJIPIGA PICHA ZINAZOTISHA NA ZA AJABU..TAZAMA PICHA HAPA


Kwa wale wapenda picha za kujipiga wenyewe yaani ‘Selfie’ kuna mchezo umeanzishwa mtandaoni unaojulikana kama ‘Selfie Olimpics’.



Mchezo huo ambao umeonekana kuwavutia vijana wengi zaidi unawataka watumiaji wa Facebook, Twitter na Instagram kupiga cpicha za hatari ‘The most dangerous and outlandish selfie ever’ na kuzipost katika mitandao hiyo.

Mtandao wa Business Insider umeripoti kuwa ukurasa wa Facebook uliofunguliwa masaa kadhaa yaliyopita tayari umepata likes 30,000 na kuna picha 28,000 tayari zimewekwa Instagram za mchezo huo.
Jionee mwenyewe baadhi ya picha za shindano la wataalam wa selfie.

MTI WA MAAJABU WENYE SURA NA UMBO LA BINADAMU WAGUNDULIWA KASKAZINI MWA MISRI..CHEKI PICHA HAPA



    Mti wa ajabu kama unavyoonekana ukiwa na sura kama ya binadamu pamoja viungo vinavyofanana na mwanamke!

     Na Mwandishi Wetu
    Watafiti wa mambo Kaskazini mwa Misri wameshikwa na butwaa baada ya kuugundua mti mmoja mkubwa wenye umbo kama la binadamu tena mwanamke wa kike na kusababisha taharuki kubwan nchini humo

    Habari juu ya maajabu hayo zilirushwa kwenye televisheni moja ya nchini humo na kusababisha wananchi nchini humo kuogopa huku wengine wakisema sasa huu ni mwisho wa dunia.

    Hata hivyo maajabu mengine ya mti huo kama unavyoonekana kwenye picha huwa hauoti matawi lakini ni mbichi na ukiusogerea karibu unatoa unakutana na baridi kari zaidi ya ile ya kipupwe"AC" hali inayofanya kuwa kivutio kwa watalii wanaomiminika kuustaajabu.

  

HUYU NDIO MWANAMKE MWENYE ULIMI MREFU ZAIDI DUNIANI..!! CHEKI PICHA HAPA



Msichana Chanel Tapper, 21 wa Houston huko Us amethibitika kuwa ndiye msichana mwenye ulimi mrefu kuliko wote Duniani na kuingizwa katika rekodi za Guinness.
Mwezi September 2011 alialikwa na Guinness huko Los Angeles na kupimwa urefu wa ulimi wake ambapo ulithibitika kuwa na urefu wa sm9.7 na kuwashinda wapinzani wake wawili.
Alieleza kuwa haoni tabu yoyote kuwa hivyo bali anachukulia kama kitu cha kufurahisha.
  

MAAJABU!! ANGALIA PICHA ZA BINADAMU ALIYE ISHI MIAKA 37 BILA KUOGA.





DELHI, IndiaAMA kweli majuu hamnazo, mzee mmoja nchini India ameamua kuishi maisha ya kipekee kwa kutooga kwa miaka 37 sasa.Kutokana na uamuzi wake huo, Kailash Singh (65) kutoka taifa hilo barani Asia, amevunja rekodi ya dunia.Singh, 65 ambaye mbali ya kutokuoa pia hajanyoa nywele zake ambazo kwa sasa zimefikia urefu wa futi 6 tangu mwaka 1974 baada ya kuchukua jiko.Unaweza kujiuliza ni kwanini aliamua kuishi maisha hayo,

Singh anasema kuwa aliahidiwa zawadi na mchungaji kama angefuata ushauri wake.Maisha ya mzee huyo wa Kiindi yametawaliwa na uvutaji wa marijuana na kusali kwa mungu wa Kihindu aitwaye Shiva huku akicheza pembeni ya moto.Singh ambaye ana watoto saba, kuna siku familia yake ilimlazimisha kwenda mtoni ili kuoga lakini alikataa na kuwakimbia.
  

MAAJABU HAYA! MAJI YA MTO YABADILIKA NA KUWA DAMU.. JIONEE MWENYEWE HAPA...!!



The waterway that runs through the city of Wenzhou, in southeastern Zhejiang province in China, turned bloody red leaving locals in a state of shock.

According to the residents of the area, where an unusual incident occurred, it has never happened before. The variant with an industrial contamination has been excluded as there are no chemical plants along the waterway length.

The witnesses claim that the at 4am the water flow was normal but by 6am it had changed colour and turned into “blood”. As there’s still no explanation what could happened to the water officials are taking water samples to find out the reason of the phenomenon.


Wenzhou is a well-known town in East China’s Zhejiang Province. The place is surrounded by mountains on three sides with the front of the city facing the Pacific ocean.

It is not the first time rivers turn red in China, in 2012 the Yangtze River also changed colour. There are different theories what could provoke the colour-change of water, including sand distribution due to upstream flooding, dye pollution and even the start of the Apocalypse. -naijapicks
bbc
Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top