Kikosi cha timu ya Simba.
Na Wilbert MolandiWAKIWA mjini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye kambi ya maandalizi ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Simba wanatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Klabu ya Bidvest Wits FC ya Afrika Kusini, leo Jumatatu.
Timu hiyo, ipo kambini huko tangu wiki iliyopita ikijiwinda na pambano lao dhidi ya Yanga litakalopigwa Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba tayari imecheza mchezo wa kwanza dhidi ya Orlando Pirates ya Johannesburg inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini na kutoka sare ya 0-0.
Bidvest Wits FC itakayocheza na Simba leo (Jumatatu) yenyewe inashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya nchini humo ikiwa na pointi 13 huku Kaizer Chiefs ikiongoza ikiwa na 21 na Ajax Cape Town ikifuatia na 14.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Humphrey Nyasio, alisema mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa usiku kwenye Uwanja wa Bidvest uliopo Johannesburg.
Nyasio alisema, mechi hizo wanazoendelea kuzicheza wakiwa huko Afrika Kusini, zitamuwezesha kocha mkuu, Mzambia, Patrick Phiri kuona upungufu wa kikosi chake kabla ya kukutana na watani wao wa jadi, Yanga.
Aliongeza: “Mechi nyingine ya mwisho nchini humu, tutacheza dhidi ya Superspot United Jumatano (keshokutwa).”
Aidha Nyasio alisema, msafara mwingine wa wachezaji waliobaki na Taifa Stars kucheza mechi ya kalenda za Fifa, unatarajiwa kuelekea Afrika Kusini leo Jumatatu ambao ni Amri Kiemba, Joram Mgeveke, Said Ndemla, Haruna Chanongo, Miraji Adam na Jonas Mkude.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >