Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi.
Na Wilbert MolandiSIMBA imeambulia pointi tatu katika mechi tatu, uongozi wa timu hiyo chini ya Rais Evans Aveva umeamua kujipanga kikamilifu hasa wakati huu ambapo wanajiandaa kuivaa Yanga kwenye Ligi Kuu Bara, maandalizi ya timu hiyo yameonekana kuwa makali chini ya Kocha Patrick Phiri jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Tangu kikosi cha Simba kilipotua Afrika Kusini, Jumatano iliyopita, Phiri raia wa Zambia, ameamua kuongeza dozi kwa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku tofauti na ilivyokuwa awali wakati wapo Tanzania, ambapo tangu kuanza kwa msimu, Simba imekuwa ikifanya mazoezi mara moja kwa siku.
Kutokana na mabadiliko hayo ya ratiba ya mazoezi, inaonekana kuwa Simba imedhamiria kupata ushindi katika mechi ya Yanga ambayo itapigwa Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Simba, Humphrey Nyasio, ameliambia gazeti hili kuwa, programu aliyoiongeza Phiri itaendelea kwa muda wote ambao watakuwa kambini nchini humo wakiwa wamefikia kwenye Hoteli ya Eden Vale.
“Lengo la mazoezi hayo ni katika kuwaongezea stamina wachezaji na kuwajenga kisaikolojia baada ya sare tatu mfululizo.“Lakini kesho (leo) hatutafanya mazoezi ya asubuhi na jioni kwa kuwa tutakuwa na mechi ya kirafiki saa tatu na nusu usiku dhidi ya Orlando.
“Mechi hiyo itakuwa kwenye Uwanja wa Orlando ila mashabiki hawataruhusiwa kuingia, itahusisha viongozi tu,” alisema Nyasio.Aidha, Nyasio aliongeza kuwa kuna kocha Mzungu ambaye alifika mazoezini hapo kwa ajili ya kuwanoa makipa Hussein Sharrifu ‘Casillas’ na Manyika Peter Junior.
“Kocha huyo Mzungu hatujampa mkataba lakini tulimuomba asaidie kikosi chetu kwa muda,” alisema Nyasio.
Wakati huohuo, ofisa habari huyo aliongeza kuwa, wachezaji wa Simba ambao wapo kwenye kambi ya Taifa Stars wataijiunga na wenzao waliopo Afrika Kusini, keshokutwa Jumatatu mara baada ya mechi kati ya Stars na Benin itakayopigwa kesho Jumapili. Wachezaji hao ni Amri Kiemba, Haruna Chanongo, Said Ndemla, Miraji Adam, Joram Mgeveke na Jonas Mkude.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >