Habari Kali
Loading...

Jaja, Coutinho wapewa siri kuiua Simba

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >


Mshambuliaji wa Yanga, Geilson Santana 'Jaja'.
Na Wilbert Molandi
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, ameonekana kupania timu yake iwafunge wapinzani wake Simba mabao mengi, baada ya kuonekana akiiongezea mbinu safu yake ya ushambuliaji kwenye mazoezi yake.
Hiyo ni baada ya kuiona safu ya ulinzi ya watani wao wa jadi, Simba haipo imara kwenye mechi zake tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara ilizozicheza.Safu hiyo ya ulinzi, pia iliwahi kulalamikiwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, Patrick Phiri ambayo imeonekana kuwa na upungufu tangu aondolewe Mkenya, Donald Musoti na nafasi ikichukuliwa na Mganda, Emmanuel Okwi.
Timu hizo zote pinzani, hivi sasa zipo kwenye maandalizi ya nguvu kujiandaa na mechi ya ligi kuu Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo, alionekana akiwapa mbinu hizo mbalimbali washambuliaji wake jinsi ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza wakiongozwa na Mbrazili, Geilson Santos Santana kwenye mazoezi ya jana Ijumaa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Loyola, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho.
Akiwatumia viungo wake Mrwanda, Mbuyu Twite na Hassani Dilunga, kocha huyo alionekana akitoa maelekezo ya jinsi ya kuwachezesha viungo washambuliaji waliotokea pembeni, Haruna Niyonzima na Husseni Javu.
Niyonzima na Javu wenyewe walikuwa na jukumu moja pekee la kupiga krosi safi zilizowafikia washambuliaji, Jaja na Coutinho kabla ya kuziunganisha kuingia wavuni kwa njia ya vichwa, kupiga mashuti na kumchambua kipa, Ali Mustapha ‘Barthez’.
Wakati mazoezi hayo yanaendelea, Twite na Dilunga walionekana kufuata vyema maelekezo ya kocha huyo kutokana upigaji wao wa pasi zilizowafikia miguuni.
Kocha huyo, aina yake ya mashambulizi anapenda yaanzie pembeni akiwatumia viungo washambuliaji wanaotokea pembeni kwa ajili ya kupiga krosi zitakazomfikia Jaja na Coutinho kabla ya kufunga.
Katika mechi hiyo ijayo dhidi ya Simba, kocha huyo huenda akatumia mfumo huo wa kushambulia kwa kushtukiza kwa kuwatumia mawinga kupiga krosi kwa Jaja.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top