BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Msongo wa mawazo ndo kitu kinachomtokea mara nyingi
zaidi na mara kwa mara kwa binadamu mtu mzima, ndo maana kuna misemo
kama, "Mtu mzima ni jalala la matatizo", na kwenye matatizo yanakuja
mawazo... na mawazo ya kisongamana ndo msongo wenyewe wa mawazo, sababu
za msongo wa mawazo hutofautiana kutoka mtu na mtu, kama msongo wa
mawazo unavyoharibu maisha yetu na kufanya tusifikirie vizuri ndivyo
hivyo hivyo kinachotokea hata kwenye miili yetu, na kufanya mifumo ya
mwili kudhurika kwa hali ya juu kama ifuatavyo...
Mfumo wa neva
Ukiwa
na msongo kimwili au kiakili, mwili hubadilisha nguvu zake na
kuzielekeza kwenye mfumo wa kupigana, huhisi kuna tatizo kimwili ambalo
linatakiwa kupambana nalo na kusababisha ushilikiano wa mfumo wa neva
kutuma taarifa kwenye tezi ya adreno kutoa homoni ya adrenaline na
cortisol, homoni hizi husababisha moyo kwenda mbio, presha ya damu
kuongezeka, kasi ya mfumo wa umeng'enyo wa chakula nayo kuongezeka
pamoja na kuongeza kiasi cha glukosi(sukari) kwenye milija ya damu, hali
hii inayosababishwa na msongo huisha mara baada ya hali ya
msongo(stress) kwisha.
Mfumo wa misuli
Kukiwa na
msongo(stress), misuli hupanuka, mvuto wa misuli kwa muda mrefu
husababisha uchovu, maumivu, kuumwa kichwa au kipanda uso na athari
nyingi nyinginezo.
Mfumo wa upumuaji
Msongo(stress)
hufanya mtu kutopumua vizuri kwa kusababisha upumuaji wa kasi ambao
husababisha mshituko wa maumivu ya kifua kubana kwa baadhi ya watu.
Mfumo wa mishipa na moyo
Msongo
wa hali ya juu husababisha mapigo ya moyo kwenda mbio, misuli ya moyo
kuvutika na mishipa inayopeleka damu kwenye misuli mikubwa na moyo
kusinyaa na kusababisha kujaa kwa damu inayotakiwa kusambazwa sehemu
hizi za mwili, kuruddia rudia kwa msongo wa hali ya juu husababisha
kuvimba kwa mishipa hivyo kutokea kwa ugonjwa wa moyo.
Mfumo wa homoni endocrini
Endocrini
ni homoni nzinazomwagwa moja kwa moja kwenye damu, mwili ukiwa kwenye
msongo sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus hutuma taalifa na
kusababisha tezi ya adeno kutengeneza homoni ya cortisol pamoja na
epinephrine ambayo wakati mwingine huitwa "homoni ya msongo'.
INI
Baada
ya homoni ya cortisol na epinephrine kutolewa, ini hutengeneza
glukosi(sukari) kwa wingi, sukari hii huenda moja kwa moja damuni na
kutumika kuupa nguvu mwili kwa ajili ya dharura.
Mfumo wa mmeng'enyo
Kwa
baadhi ya watu msongo hufanya mtu kula zaidi au kutokupata hamu ya
chakula tofauti na ilivyo kawaida, msongo unaweza kukusababisha ule
chakula tofauti tofauti au uvute sigara kwa wigi, au uzidishe utumiaji
wa pombe na vileo na kukufanya uzulike kwa kiungulia, au tumbo kujaa
gesi, tumbo linaweza kupata maumivu au kutapika pindi msongo ukiwa
katika hali ya juu sana.
Mfumo wa uzalishaji
Kwa
wanaume, homoni nyingi ya cortisol inayotolewa kwa shindikizo la msongo
huathiri ufanyaji kazi wa kawaida wa mfumo wa uzalishaji, msongo wa
hali ya juu husababisha homoni ya testosterone kutokufanya kazi vizuri
na kusababisha utengenezaji wa shahawa kuwa mdogo ambao huleteleza
ugumba wa muda.
Kwa wanawake msongo husababisha kuingia mara kwa mara
kwenye hedhi na tarehe kutokua za uhakika za kuingia kwenye siku zao au
kusababisha tumbo la hedhi kuuma sana na kupunguza hamu ya kufanya
mapenzi.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Thursday, 16 October 2014