ULINZI
mkali jana uliimarishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, wakati
watuhumiwa wa vitendo vya ulipuaji mabomu jijini hapa walipofikishwa
mahakamani.
Askari
wasiopungua 100 wakiwamo wenye mbwa, askari wa usalama wa taifa,
magereza, askari kanzu na askari polisi wenye bunduki na mabomu ya
machozi walitanda eneo la mahakama na hivyo kuvuta hisia za wananchi
wengi.
Hatua
hiyo inaelezwa kuwa ililenga kuimarisha usalama wakati wa kesi ya
watuhumiwa hao 19 wanaokabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na vitendo
vya ugaidi kwa kulipua mabomu na umwagaji wa tindikali ikiendelea
mahakamani.
Kuimarishwa
kwa ulinzi huo kulikwenda sambamba na ukaguzi kwa kutumia vifaa maalumu
vya kutambua vitu vyenye chuma kwa watu walioingia eneo la mahakama.
Katika
eneo hilo ndugu, jamaa na marafiki wa watuhumiwa 19 walionekana
kufurika, lakini hata hivyo kutokana na ulinzi mkali watu hao
hawakuruhusiwa kuingia mahakama ya wazi yalipokuwa yakisomwa mashtaka ya
ndugu zao.
Ilipofika
saa 4:30 asubuhi watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani wakiwa chini ya
ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na magari zaidi ya 9 zikiwamo pikipiki
za polisi.
Katika
eneo la mahakama wakati watuhumiwa hao wakishushwa, ulinzi uliimarishwa
zaidi kwa kila askari aliyekuwa eneo hilo akionekana kushika silaha
yake tayari kwa tukio lolote litakalojitokeza.
Akizungumza
na MTANZANIA Jumamosi kuhusu ulinzi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha, Liberatus Sabas, hakuweza kueleza idadi kamili ya askari
waliomwagwa mahakamani hapo, ingawa alikiri uwepo wa askari wengi.
“Siwezi
kukuambia walikuwa askari wangapi, hilo ni suala letu la ndani, itoshe
kufahamu kwamba, tuliimarisha ulinzi vya kutosha na hii ni kutokana na
na aina ya kesi yenyewe,” alisema.
Mashtaka
Akisoma
mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Msofe, Mwendesha Mashtaka
wa Serikali, Augustino Kombe, alidai kuwa watuhumiwa, Yussuph Ally Huta
(30) na wenzake 12 wanatuhumiwa kwa kesi ya ugaidi nyumbani kwa Sheikh
Sudi Ally Sudi Julai 3, mwaka huu.
Kombe
aliwataja watuhumiwa wengine katika kesi hiyo kuwa ni Abashar
Omar(24), Kassim Ramadhan,(34), Jafar Lema(38), Abdul Mohamed Humud
(30), Said Temba (42), Idd Yusuph (32), Hassan Mfinanga (57), Anwar
Nasher Hayel (29), Yahaya Twahir (37), Yusuph Ally Ramadhan (23) na
Majid Michael.
Kombe
alidai kuwa watuhumiwa wote wanadaiwa kufanya njama za kufanya vitendo
vya kigaidi kati ya Januari na Februari mwaka huu, kwa kufanya njama ya
ugaidi nyumba ya Sheikh Sudi.
Katika
kosa la pili alidai watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya ugaidi ambapo
Julai 3 mwaka huu, katika eneo la Majengo mjini Arusha walirusha bomu la
mkono na kumjeruhi, Sheikh Sudi na Muhad Hussein.
Akisoma
shtaka la nne alidai kuwa linawakabili mtuhumiwa, Yahaya, Lema,
Abdulmohamed na Temba wanaodaiwa kutoa ushirikiano uliosababisha
kufanyika kwa kitendo cha kigaidi ambapo wanadaiwa kutoa msaada wa fedha
kati ya Januari na Julai mwaka huu.
Washtakiwa bomu la Soweto
Mwendesha Mashtaka wa Serikali alidai katika kesi hiyo ya mauaji na kujaribu kuua inawakabili watuhumiwa 13.
Aliwataja
watuhumiwa katika kesi hiyo kuwa ni Yusuph Huta (30), Yahaya Twahir
(37), Jafar Lema (38), Ramadhan Waziri (28), Kassim Ramadhan (34), Abdul
Mohamed Humud (30), Abashar Omar (24), Abdulrahman Hassan (41), Morris
Muzi (44), Miganya Miganya (28), Baraka Bilango (40), Hassan Omar na
Said Temba.
Akisoma
maelezo ya watuhumiwa hao alidai kwamba, kwa pamoja washtakiwa wote
waliwaua, Judith Mushi, Ramadhan Juma, Fahad Jamal na Amir Daffa.
Kombe
aliiambia Mahakama kuwa katika kesi hiyo watuhumiwa hao walijaribu
kuwaua, Agustino Theodory, Sylvester Jakaranda, Abdallah Halela, Peter
Mshanga, Raphael Mohamed, Emanuel Lucas, Abraham Shangwe na Patrick
George.
Washtakiwa wakukutwa na mabomu
Mwendesha
Mashtaka Kombe aliendelea kueleza kuwa kesi ya kukusanya zana, kukutwa
na zana na kusamabaza zana kwa lengo la kufanya ugaidi inawakabili
watuhumiwa 10.
Mwendesha
Mashtaka Kombe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Yussuph Huta, (30),
Hassan Omar (40), Miganya Miganya (28), Sumaiya Ally (19), Morris Muzi
(44), Hassan Mfinanga (57), Abashar Omar(24), Ramadhan Waziri (28) na
Kimolo Issa.
Kombe
alidai kuwa katika kosa la kukusanya zana na kutenda ugaidi ambapo
watuhumiwa hao wanadaiwa kukusanya mabomu mawili kati ya Juni 23 hadi
Julai 22 Mwaka huu kwa lengo la kufanya ugaidi.
Watuhumiwa wa tindikali
Mwendesha
mashtaka wa Serikali, Marselino Mwamunyange, aliiambia mahakama hiyo
kuwa washtakiwa wanne wanakabiliwa na kosa la ugaidi.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Kasssim Ramadhan (34), Jafar Lema (38) na Hassan Mfinanga (57).
Akielezea
maelezo ya kosa hilo, Mwendesha Mashtaka Mwamunyange alidai kuwa
watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya kitendo cha ugaidi katika eneo la
Msikiti Mkuu wa Arusha cha kummwagia tindikali Mustapha Kiago na
kumsababishia majeraha mwilini.
Mwendesha
Mashtaka Mwamunyange alidai kuwa katika kesi hiyo watuhumiwa
wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi na kutenda njama ya kufanya ugaidi.
Aliwataja
washtakiwa hao kuwa ni Yusuph Huta (30), Ramadhan Waziri (28), Kassim
Ramadhan (34) na Jafar Lema(38), ambao kwa pamoja wanadaiwa kufanya
kitendo cha kigaidi kwa kummwagia tindikali Sheikh Juma.
Mwamunyange
alidai kwamba, kosa jingine linalowakabili ni kutenda njama ya kufanya
ugaidi ambapo wanadaiwa kati ya Julai 2009 hadi Julai 2013 watuhumiwa
hao walitenda kosa la kusababisha majeraha.
Watuhumiwa wa bomu
Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Felix Kwetukia alidai mahakamani hapo kuwa
watuhumiwa katika kosa la kufanya ugaidi nyumbani kwa Abdulkarimu Jonjo
ni Yussuph Huta (30), Kassim Ramadhan (34), Mustapha Kiago (49) na
Abdulaziz Mohamed (49).
Alidai kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya njama za kutenda kosa hilo kati ya Oktoba mosi hadi Oktoba 25 mwaka 2012.
Kwetukia
alidai kuwa kosa la pili kwa watuhumiwa hao ni la kufanya vitendo vya
kigaidi ambapo wanadaiwa kufanya kosa la kutupa bomu lililotengenezwa
kienyeji na kumjeruhi Sheikh Jonjo ambapo kosa la tatu ni la kufadhili
na kuwezesha vitendo vya kigaidi kufanyika.
Ushawishi wa ugaidi
Mwendesha
Mashtaka wa Serikali Kombe katika mashtaka hayo aliwataja watuhumiwa
kuwa ni Ibrahim Lenard a.k.a Sheikh Abuu Ismail (37), Anwar Hayel (29)
na Yasini Shaban (20).
Alidai
kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kati ya Machi 8 hadi Julai 14 mwaka huu
waliwashawishi vijana kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Al- Shabaab.
Mwendesha
Mashtaka aliwataja waliosajiliwa kujiunga na kikundi hicho kuwa ni Abu
Haris, Abu Shafy, Abu Mujahd, Soud Kabaju, Ahmed Islam, Mwinyi Mwinyi,
Qassim Salaf na Rashid Salaf.
Kwa
upande wake Hakimu Mkazi Msofe aliwataka watuhumiwa wote wasijibu
chochote kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hizo.
“Washtakiwa
hamtakiwi kujibu chochote kwani Mahakama hii haina mamlaka ya
kusikiliza kesi zinazowakabili na mtaendelea kukaa chini ya ulinzi kwani
kesi hizi hazina dhamana,” alisema Msofe.
Upelelezi
wa kesi zote bado haujakamilika na upande wa mashtaka waliomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kutajwa ambapo kesi hizo zitatajwa tena Agosti 15,
mwaka huu.
CHANZO:Mtanzania
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

