MAHAKAMA
ya Kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa
jinsia moja, ambayo ilisababisha mataifa kadhaa ya magharibi kuinyima
misaada.
Sheria
hiyo ilizua mjadala si tu nchini Uganda bali kote duniani, kiasi cha
kuyafanya mataifa ya magharibi yalazimike kuingilia kati.
Mahakama
ilisema muswada uliopitishwa kabla ya kuidhinishwa na rais kuwa sheria
ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kuupitisha na kwa
hivyo ulikuwa kinyume na sheria.
Vitendo
vya mapenzi ya jinsia moja tayari vilikuwa vimeharamishwa nchini
Uganda, lakini sheria hiyo mpya ilitoa adhabu kali zaidi.
Sheria
hiyo iliharamisha hatua zozote za kueneza au kushawishi mapenzi ya
jinsia moja na wakati huo huo ikiwajumuisha wanawake wasagaji katika
kundi hilo.
Sheria
hiyo iliyosainiwa na Rais Yoweri Museveni, Februari mwaka huu pamoja na
mambo mengine inatoa adhabu ya kifungo cha maisha na inawataka Waganda
kuripoti matukio ya kishoga au kisagaji kwa mamlaka husika.
Wabunge
huenda wakalirudisha upya bungeni suala hilo, mchakato unaotarajia kuwa
mrefu ukizingatia sheria ya sasa ilichukua miaka minne hadi kupitishwa.
Lakini wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakisherehekea jana.
“Mimi
si mhalifu tena, leo tumeandika historia kwa vizazi vingi vijavyo,”
alisema Kasha Jacqueline, mmoja wa wanaharakati maarufu wa haki za
mashoga waliofungua kesi hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, alikuwa ameihusisha sheria
hiyo na sheria za kifashisti za utawala dhalimu wa Nazi nchini
Ujerumani.
Wakosoaji
pia walidai Museveni aliisaini sheria ili kupata uungwaji mkono wakati
wa kuelekea uchaguzi wa urais mwaka 2016, ambao utakuwa mwaka wake wa 30
madarakani.
chanzo: mtanzania
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

