KIJANA mmoja
aliyefahamika kwa jina la Yona Nathal, mkazi wa Ubungo ya River Side
jijini Dar es Salaam, Jumanne iliyopita alijikuta katika timbwili zito
na kundi la washereheshaji maarufu wa kike Dar ‘ma -MC’ baada ya
kubainika kuwachanganya kimapenzi.
Yona Nathal akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
AWEKEWA MTEGO
Ilidaiwa
kuwa Yona ameshawatokea baadhi ya ma-MC hao kwa nyakati tofauti na
kula nao raha kwa siri lakini siku moja wakajuana na kusambaziana
taarifa.
Inazidi
kudaiwa kuwa, kwa vile habari zake zilishasambaa kwenye umoja wa ma- MC
hao, hivyo waliweka azimio la kumnasa kwa sababu aliibuka tena na
kumtongoza MC mmoja ambaye pia ni mke wa mtu (jina tunalo).
MC
huyo alikubaliana na Yona wakutane kwenye Hoteli ya Legho iliyopo
Shekilango, Ubungo jijini Dar ambapo ma- MC wa kike na wa kiume
walikusanyika kwa ajili ya kumtia mikononi kijana huyo waliyedai
anawadhalilisha.
Akijitetea baada ya kunaswa.
KIDUME ANASWA
Ilikuwa
saa mbili usiku, Yona alishuka kwenye daladala akiwa ametinga suruali
nyeusi ya kitambaa, shati jeupe na miguuni amevaa kandambili nyekundu
aina ya bata.
Baada
ya kushuka alimpigia simu MC mwenye ahadi naye ambaye naye alimwambia
ameshafika Legho. Walipokutana uso kwa uso Yona alimuomba ‘amuhagi’ MC
huyo lakini cha kushangaza, akajikuta amezungukwa na kundi la ma- MC
wengine ambao walianza kumzodoa wakimwambia ana tabia chafu ya
kuwadhalilisha.
“Jamani naomba mnisamehe sana, mimi sina nia mbaya na hawa ma- MC ni maneno yakeYona Nathal.
Ilikuwa
mbilinge kubwa, ikabidi Yona awe mpole baada ya kutaitiwa ambapo
aliomba msamaha huku akisema hakuwa na nia mbaya ila ana hisia kali za
mapenzi na ma-MC wa kike hususan wakati wakiwafunda maharusi kwenye
kitchen party.
“Jamani
naomba mnisamehe sana, mimi sina nia mbaya na hawa ma- MC wa kike,
hisia zangu ndizo zilizoniponza. Navutiwa nao sana,” alisema kijana
huyo.
Wakati
akihojiwa, kijana huyo aliwataja ma -MC wengine zaidi ya sita maarufu
hapa ambao ni wake za watu na kukiri kuwa ameshakula nao ‘mambo matamu’.
HASIRA ZAIDI
Maneno
hayo yalipandisha hasira za ma-MC hao ambapo walitaka kumpa kichapo
lakini ghafla walitokea askari wa Kituo cha Polisi Urafiki-Ubungo, Dar
na kumuokoa kisha kumpeleka kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Ndani ya kituo hicho cha polisi, Yona alifunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. URP/RB/6607/2014 UCHUNGUZI.