1.Kuchat
kwenye mtandao mara baada ya kurudi nyumbani au kama una kazi za
ofisini ambazo inakulazimu uzifanyie nyumbani. Ni vyema kumuomba mwenzi
wako ruhusa kama hatajali kabla ya kukurupuka na kufungua lap top na
kuendelea na kazi zako.Ni muhimu kuomba ruhusa kwa mwenzi wako kwa
sababu huwezi kujua labda kuna jambo alikuwa anataka mjadili au anahitaji muda wa kuwa na wewe.
2.Kama
utakuwa na mtoko na wafanya kazi wenzako au marafiki zako. Kwa mfano
ile mitoko ya LEO TUPO HAPA PUB, ni vyema kumjulisha mwenzi wako mapema,
ili ajue uko wapi na sio mwenzi wako aje kujua baadae, sababu italeta
ugomvi.
3.Kama
utachelewa kurudi nyumbani kutokana na jambo lolote ni vyema kumjulisha
mwenzako, lakini pia hata kama utakula chakula huko ulipo ni vyema pia
kumjulisha mwenzako kwa sababu anaweza akawa amekuandalia chakula kizuri
halafu usile kitanuka mbaya. kumbuka, miongoni mwa mambo ambayo
yanawakera wanawake ni mwanaume kutokula chakula nyumbani ugomvi wake ni
MAJANGA....!
4.Kutoa msaada sio kwa vituo vya watoto yatima tu,
bali hata kwa ndug zako, kitu chochote iwe ni nguo au chakula ni au vitu
vingine ni vyema kumjulisha mwenzi wako kuliko kufanya mambo kimya
kimya. Mwenzako atakapojua anaweza kulalamika au akakaa kimya lakini
usije ukadhani ni mjinga kuna siku atalipiza kitu ambacho hutafurahiya.
5.Kuwaeleza
mashoga zako kuhusu mipango yenu. Katu usije ukawaambia mashoga zako
kwamba mna mpango wa kununua nyumba au kununua gari. Ni vyema mipango
yenu ikawa ni siri yenu kwani ikitokea mipango hiyo ikakwama utaishia
kuzodolewa na mashoga zako. kumbuka kwamba si kila shoga anapenda
maendeleo ya mwingine
6.Ghafla unabadili mtindo wa nywele bila kumshauri mwenza wako. Unaweza kuibua kisirani cha bure katika ushusiano wenu.
7.Kutupa
vitu ambavyo unaviona kama uchafu ndani ya nyumba wakti mwenzako
alikuwa bado anavihitaji kwa matumizi mengine. Kuna baadhi ya wanawake
wanapoamua kusafisha nyumba hutaka kutupa kila kitu anachoona kama ni
uchafu bila kumshirikisha mwenzi wake. Ni kosa kubwa, ni vyema
kushauriana wakati wa kusafisha nyumba ili kujua ni kitu gani cha kutupa
na kitu gani cha kuhifadhi.
8.Kuacha
vitu kwa mwenzi wako bila taarifa. Kama mko na mahusiano lakini kila
mmoja anaishi kwake, pale unapokwenda kupitisha usiku kwa mwenzako ni
vyema ukamuuliza kama unataka kuacha baadhi ya vitu vyako hapo kwake
kuliko kukurupuka na kuhamishia wardrobe nyumbani kwa mwenzi wako bila
taarifa. Utaonekana kama unalazimisha jambo fulani........
9.Kuombaomba.
Kuna baadhi ya wanawake au hata wanaume wanapenda kuombaomba misaada
kwa wenzi wao. Kuna wengine wako smart wao hutumia neno, "Niazime"
lakini si kwamba wanaazima bali wanaomba na hawawezi kurudisha, ni vyema
kuwa wastaarabu na kuweka mipaka, hata kama mtu anataka msaada aonyeshe
juhudi zake kwanza ndipo labda uombe msaada na sio kila siku anaomba tu
mpaka mtu anakuchoka..........