Habari Kali
Loading...

SITTI MTEVU ALIVUA TAJI LA MISS TANZANIA 2014, LILIANI KAMAZIMA AMRITHI

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga (kushoto) akionyesha barua ya Miss Tanzania, Sitti Abbas Mtemvu baada ya kujivua taji hilo.
Waandishi wa habari wakiendelea kufanya yao.
Miss Tanzania aliyechukua nafasi ya Sitti Mtemvu, Lilian Kamanzima akiongea na wanahabari (hawapo pichani)
Lilian Kamanzima katika pozi.
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la wizara  husika kufuatilia ukweli wake.
“Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.
“Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” ameongeza.

“Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”
“Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.”
Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamanzima.
(PICHA/ HABARI: MUSA MATEJA, GABRIEL NG'OSHA/GPL)

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top