Kwa
kawaida kila binadamu anayop siri yake moyoni ambayo hapendi hata siku
moja ifahamike. Lakini kwa upande wa wanaume haijalishi amekuwa na
mahusiano na mwanamke kwa muda gani au amejuana na mwanamke kwa muda
gani hiyo haiwezi kuwa ni kigezo cha kumuamini mpenzi wake kiasi cha
kumweleza siri zake za moyoni. Kuna uwezekano zipo atakazoficha kwa muda
lakini hapo baadaye akaamua kumweleza mwenzi wake, lakini kuna zile
nyingine ambazo nitataja baadhi ambazo kamwe mwanamke asitarajie kuona
mpenzi wake akifungua kinywa chake na kumweleza. Na hata ikitokea
mwanamke akazijua kupitia kwa wapambe, ni dhahiri mwanaume huyo
atakanusha kwa nguvu zake zote na hata aikibidi kutumia ubabe ili kuzima
hoja hiyo..
Kwamba
ana matatizo ya kifedha: Inawezekana wakati anakutana na mpenzi wake
mambo yalikuwa safi na alikuwa na fedha za kutosha kula bata na kuishi
maisha ya kifahari, lakini kama ikitokea mambo yakageuka ghafla bila ya
kutarajia kwa mfano alikuwa na njia zake za panya za kupata fedha nje ya
mshahara halafu njia hizo zikafungwa na mshahara ukawa hautoshi kabisa
kukidhi hata robo ya mahitaji yake na mpenziwe, hapo mwanaume anaweza
kutumia mbinu mbalimbali ili kuweka mambo sawa, ikiwezekana hata kukopa
ili kusitiri aibu lakini si kumwambia mpenzi wake kwamba mambo
yamegeuka, labda kama ni mkewe, lakini si mpenzi ambaye bado mambo
hayajaiva
Kwamba
aliwahi kubaka au kumla mtungo mwanamke na marafiki zake wakati fulani:
Inawezekana historia yake ya ujana ilikuwa na vibweka vingi ikiwemo
kubaka wanawake au kufanya mapenzi na mwanamke mmoja akishirikiana na
marafiki zake vijana wa mjini huita mtungo au kula mande. Mwanamke
asitarajie mwanaume atafungua mdomo wake na kuelezea huo upuuzi wake.
Kukiri
kwamba alikudanganganya ili akupate: Kuna wakati mwanaume hulazimika
kudanganya au kuingia na gia kubwa kama vijana wa mjini wanavyosema ili
kumpata mwanamke wa aina fulani. Kuna baadhi ya wanawake wamejiwekea
viwango vya aina ya wanaume watakaopenda watoke nao, shida ni pale kina
Bujibuji watakapokuwa wamefika bei lakini tatizo viwango viko chini,
hapo ndipo mbinu na mikakati vitatumika ikiwezekana kujivika uhusika
asiokuwa nao ili mradi ampate huyo mwanamke, na akimtia mikononi halafu
mwanamke akashtukia kwamba ameingizwa Kingi na kujaribu kuhoji,
asitarajie mwanaume huyo atakiri udhaifu. Lazima atajitahidi kutafuta
namna ya kukwepa kuonekana muongo ili mradi kulinda hadhi yake ya uongo
Kukiri
kwamba aliwahi kufungwa jela na kulawitiwa: Inawezekana mwanaume
aliwahi kufungwa jela, lakini kama inavyojulikana misukosuko ya jela ni
mingi ikiwemo kuingiliwa kinyume na maumbile, au inawezekana mwanaume
katika mazingira fulani aliwahi kuingiliwa kinyume na maumbile kwa
kulazimishwa katika mazingira magumu na ya aibu. Kamwe mwanamke
asitarajie kwamba mwanaume huyu atakuja kufungua mdomo wake na kumweleza
mwanamke kuhusu jambo hilo. hata akija kulisikia mwanaume huyo
atalipinga kwa nguvu zake zote.
Mwanaume
kukiri kwamba alikuwa ANASAFISHA KIWI CHA MACHO: Hata kama akikamatwa
live na mpenzi wake akisafisha kiwi cha macho, si rahisi mwanaume
akubali huo udhaifu, ni lazima atapinga kwa nguvu zake zote.