NI
Jumanne tena! Nawakaribisba wasomaji wangu wa safu hii makini kwa elimu
ya mapenzi katika maisha.Wiki iliyopita tulikuwa na mada ya ‘wengi
wanapenda harusi kuliko ndoa’. Wenye kuelewa walielewa.Wiki hii nina
mada nyingine kabisa inayosema dear, mpenzi ni maneno yasiyokuwa na
maana tena.
Hapa namaanisha kwamba, miaka ya zamani, wapendanao au wapenzi waliyatumia sana maneno haya katika kuoneshana upendo wa dhati.
Ilikuwa sifa kubwa kumsikia msichana akimwita boyfriend wake ‘dear’au mpenzi!
“Niambie my dear! Upo mpenzi?” ndivyo ilivyokuwa.
WAMEANZA KUHARIBU WANAWAKE
Mara
ya kwanza nilishangaa kumsikia mwanamke mmoja kwenye simu anamwita
mwanamke mwenzake dear. Tena alisema: my dear, zile sabuni za kuondoa
alama nyeusi usoni ulizinunua wapi?”
Kuna siku nilimsikia mwanamke
mwingine kwenye simu akisema: “Nakuja mpenzi wangu jamani. Kwanza we
umebeba na kile kitenge nilichokuagiza?”
AKILINI MWANGU
Awali
niliamini wanaozungumza nao kwenye simu huenda ni wanaume, lakini
meseji zilionesha upande wa pili ni wanawake wenzao. Kwa maneno ya
sabuni za kuondoa alama nyeusi usoni na kitenge.
LIMESAMBAA
Baada
ya hapo nilianza kufuatilia hatua kwa hatua nikaja kubaini waziwazi
kwamba, wanawake wengi wameshapoka maneno hayo kutoka kwenye kuyatumia
kwa wapenzi wao na kuwapachika mashoga zao.
MADHARA YAKE
Nilichobaini
kwa harakaharaka siku hizi ni kwamba, baadhi ya wake za watu wamekuwa
wakibebeshwa sifa ya umalaya kwa sababu ya matumizi ya maneno haya
mawili. Mfano, mke wa mtu yuko ndani kwake, anapokea simu ya mwanamke
mwenzake, anasema: Niambie my dear... we umefika kwani...basi na mimi
naoga nakuja...haya mpenzi wangu nakuja sasa hivi.
Kwa majirani wanaomsikia mwanamke huyo, baadhi yao huamini alikuwa akizungumza na mchepuko kwa sababu ya my dear na mpenzi.
HAYANA MAANA TENA
Wiki
iliyopita niliamua kufanya mahojiano na baadhi ya wanaume ambao
wanafahamu kuhusu wanawake kuyatumia maneno hayo mawili kwa kuitana
wenyewe.
Maoni yao yalisimama kwenye maana moja kwamba, maneno hayo kwa sasa hayana maana tena katika matumizi ya wapendanao.
“Sasa
kama mke wangu anamwita mwanamke mwenzake dear au mpenzi, akiniita mimi
kuna maana gani? Yaani mimi na shoga yake ni kitu kimoja?” alihoji baba
Abdul, mkazi wa Mabibo jijini Dar.
Baba
Steve wa Sinza-Mori, Dar: “Kusema ukweli wanawake wanavuruga mambo
mengi sana ila hatujui tu. Ukiachilia mbali hayo maneno kuyatumia
kuitana wenyewe kwa wenyewe we si unaona siku hizi kila mmoja anavaa
suruali.”
“Ah!
Mimi niliwahi kumuuliza mke wangu ni kwa nini anamwita mwanamke
mwenzake dear, akasema haoni tatizo, lakini ukweli mimi naona tatizo
lipo. Ipo siku na mimi nitampigia simu rafiki yangu anaitwa Sudi
nitamwita honey, nimsikie mke wangu atasemaje,” alisema Abdallah
Mkadala, mkazi wa Buguruni, Dar.
NI MBINU YA USALITI?
Baadhi ya wanaume walionesha wasiwasi wao kwamba, huenda wanawake wanaitumia fursa hiyo kuweza kusaliti!
Kivipi?
Kumbe inawezekana mwanaume akakaa na mpenzi wake ambaye anaweza kupokea
simu ya mchepuko akatumia neno dear au mpenzi kwa kumaanisha huku
mwanaume huyo akijua anaongea na mwanamke mwenzake!
WANAWAKE WENYEWE WANASEMAJE?
Pia niliweza kuzungumza na baadhi ya wanawake kuhusu matumizi ya maneno hayo. Niliwalenga zaidi wale wanaopenda kuyatumia.
Mama
Mwamtumu wa Makongo, Dar: “Kusema ukweli wanawake tumeshajiweka kwenye
mazoea, hasa sisi wa mijini. Lakini kiusahihi kabisa si maneno mazuri
kuyatumia sisi kwa sisi japokuwa maana ya maneno yenyewe ni upendo tu.”
Skola,
mkazi wa Bunju B: “Dear na mpenzi ni neno moja jamani! Ni kuonesha
upendo kwa mwenzako. Ila ni kweli kuna ukakasi. Mfano wanaume nao
wakiamua kuitana sweet, darling naamini sisi wanawake hatutawaelewa hata
kidogo.”