BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
sehemu ya maisha yake. Tena inaaminika kwamba, kukosea ni kujifunza,
maana kosa utakalofanya leo ni funzo la kesho. Hii ipo pia hata katika
uhusiano na wapenzi wetu, mara kadha wa kadha tumejikwaa na kuwakosea.
Hakuna
cha ajabu. Ni kawaida kabisa, lakini jambo la msingi hapo ni kwa namna
gani tunajifunza kupitia makosa. Ni kwa jinsi gani tunamaliza tofauti
hizo. Maana unaweza kuwa hodari wa kukosea au ukawa bingwa wa kusamehe,
lakini wimbo huo ukaendelea kubaki hivyo hivyo kila siku.
Lakini
pia, wapo ambao kwa bahati mbaya, bila matarajio yao, wanajikuta wakiwa
wamewaudhi wapenzi wao. Ni bahati mbaya na yawezekana kabisa wanaumia
sana mioyoni mwao, lakini wakashindwa jinsi ya kumaliza ‘bifu’ hilo
katika penzi lake.
Siku
zote mkosewa hukosa raha, hupoteza hamu ya kukutana na mpenzi wake
lakini kubwa zaidi, hujishusha/hukushusha thamani ya mapenzi yake kwako.
Lakini mkosewa huyo huyo, akioneshwa kwamba makosa yaliyofanyika
hayakuwa ya makusudi na kutumia njia bora za kufikisha hisia zako kwake,
hujisikia amani na hali yake kurejea kawaida.
Soma hapa chini mambo 5 unayotakiwa kuyafanya pindi tu pale unapomkosea mpenzi wako........
KOSA LINA UKUBWA GANI?
Hapa
tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba
unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwasababu hujamwambia chochote, naye
hana raha na wewe. Hana amani ya moyo.
Hapa
unashauriwa kutulia na kutafakari ukubwa wa tatizo. Kufahamu ukubwa wa
tatizo kutakupa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kutatua tatizo hilo.
Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango gani?
Mathalani unaweza kuwa ulimuudhi kwasababu alikupigia simu zaidi ya mara kumi bila kupokea, akakasirika. Hili ni kosa dogo.
Lakini
yawezekana alikuta sms ya mapenzi kwenye simu yako au alikufumania;
haya ni makosa makubwa. Tafakari na ujue ukubwa wa kosa lako.
ONESHA UNAVYOJUTIA
Hii
ni kwa ajili yako wewe mwenyewe. Rafiki zangu, kutakuwa hakuna maana
yoyote kuomba msamaha wa kinafiki au kuomba msamaha ili kumaliza mambo,
kama msamaha wako haujatoka moyoni.
Ukiwa
peke yako, jiaminishe kwamba umekosea na kwa hakika unahitaji
kusamehewa. Jutia ndani ya moyo wako, kwa dhati kabisa ukiwa na ahadi
kwamba hutarudia tena. Hili ni zoezi la Kisaikolojia, ambalo
litakusaidia baadaye wakati ukikutana na mpenzi wako kwa ajili ya kuomba
msamaha.
KUWA MKWELI
Omba
kukutana naye. Yawezekana hata mawasiliano si mazuri sana, lakini hapa
jitahidi kumuomba mkutane, ikishindikana, tumia mtu wa karibu sana na
yeye. Omba kutoka naye kwa ajili ya kuzungumza.
Mweleze
ukweli wa kosa lako, onesha jinsi linavyokutesa na kukusumbua.
Usijaribu kuongea uongo wowote katika suala hili. Kuwa mkweli. Jutia kwa
moyo, aone majuto yako usoni mwako.
Mwambie
jinsi unavyoteseka na jinsi msivyo katika maelewano mazuri. Kauli yako
ya ukweli, hisia zako wakati wa kuzungumza, ndivyo vitakavyokuweka
katika mazingira mazuri ya kuweka mambo sawa.
MHAKIKISHIE HUTARUDIA
Bila
shaka, kama utakuwa umefuata taratibu zote hizo kwa umakini, uwezekano
wa kusamehewa ni mkubwa sana. Hili ndiyo matarajio yangu, naamini hata
wewe pia, lakini ili msamaha huo ukamilike, mhakikishie mpenzi wako kuwa
hutarudia tena.
Mwambie
kwa kumaanisha, kwamba umegundua udhaifu wako na haupo tayari kumfanya
tena asiwe na furaha tena. Hakuna uchawi ni maneno tu!
FANYA KITU MAALUM
Hapa
unatakiwa kufanya kitu maalumu kwa ajili ya mpenzi, ukionesha kwamba
umekubaliana na msamaha wake na mambo yameisha. Kitu utakachokifanya
hapa utalinganisha na ukubwa wa kosa kama nilivyosema awali.
Mathalani
unaweza kutoka naye na kwenda kulala naye hotelini, ukihakikisha unampa
mahaba mazito kama shukrani kwake. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya
kulingana na uwezo wako kifedha. Fanya vyovyote ili kosa lile
lisahaulike moja kwa moja!
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Tuesday, 14 October 2014