Upo
uhusiano ambao umelengwa kudumu, hasa kwa wanandoa. Kuna wengine hawa
sura ya kudumu, wapo kwa muda kwa kuzingatia mazingira pamoja na kile
kilichomo ndani ya nafsi zao.
Unaweza
kujiuliza; Kwanini ufike wakati utake kuvunja uhusiano wako na
mwenzako? Iwe kirafiki au kimapenzi, Ipo wazi kwamba kuna sababu
mbalimbali zinazoweza kuwafanya wahusika kuamua.
Yawezekana
uhusiano wako na mpenzi wako au rafiki yako wa jinsia tofauti unakutia
hasara, au unakuharibia biashara, au unakupunguzia heshima katika jamii,
au pengine uaminifu wako kazini. Mathalan, mpenzi wako anapokuwa
anafahamika kuwa ni kahaba.
Inawezekana
uhusiano wako na mwenzako unaidhuru nafsi yako. Mfano, mwenzio ana
nguvu sana juu yako kiasi kwamba huwezi kusema “hapana” kwa lolote
analokwambia. Pengine kutokana na hali hiyo umekuwa ukilazimika kufanya
mambo ambayo huyapendi na ambayo hayaendani na maadili.
Lakini
pia yawezekana umeanza kumchukia mwenzako. Mazingira yamebadilika,
kwahiyo wewe na yeye hampatani tena. Unajitazama na kugundua kwamba
ulivyo huendani naye. Ni matokeo ya kuchokana!
Naam,
baadhi ya mahusiano, yawe ya kirafiki au kimapenzi, huwaweka katika
wakati mgumu watu kiasi kwamba ni lazima mtu achukue hatua ili aweze
kuishi kwa amani na furaha ya kweli. Hata hivyo, ikae akilini kwamba
inauma mno kuachana na mtu unayempenda!
Kumaliza
uhusiano wa kimapenzi au kirafiki si hatari, lakini la msingi ni
kuhakikisha kuwa unamwacha mwenzako akiwa hajaathirika kisaikolojia kwa
namna yoyote. Kwa sababu hiyo unapaswa kujifunza njia sahihi ya kumaliza
uhusiano wako na mwenzako inapobidi.
Kuna
jamii inaweza kuthubutu kusema, unapochoshwa na mtu, mchukue uende naye
mahali kisha umueleze kwa uwazi kuwa hutaki tena kujihusisha naye kwa
sababu moja, mbili, tatu. Hata hivyo, hilo si jambo rahisi kwa wengi.
Badala
ya kukubaliana na mtu ana kwa ana na kumweleza kuwa humhitaji tena,
zipo njia za kirafiki na za kidiplomasia ambazo unaweza kuzitumia na
kumaliza mambo bila kusababisha matatizo makubwa au madhara yoyote ya
kisaikolojia.
WEKA SABABU ZAKO MEZANI!
Unapotaka
kumbwaga rafiki yako au mpenzi wako ambaye hujampa ahadi yoyote ya
kuishi naye katika ndoa, anza mchakato kwa kuweka bayana sababu
zinazokufanya utake kuachana naye. Hakikisha kuwa sababu unazoziweka ni
zile ambazo mpenzi wako huyo hatapata namna ya kuzipinga.
Zitengeneze
sababu hizo kwa kuzingatia mtazamo wako mwenyewe, na si kwa mtazamo wa
mpenzi au rafiki yako huyo, ili hatimaye kusiwe na sababu ya mwenzako
huyo kudhani atajirekebisha ili aweze kuendelea kuwa na wewe.
Namna
hii utakuwa unayaangalia zaidi maslahi yako mwenyewe na iwapo
utalazimika kumweleza mwenzako ni kwa nini unataka kumaliza uhusiano
wako na yeye, sababu zako hazitaonekana kama shambulio kwake yeye
mwenyewe wala tabia yake.
USITHUBUTU KUWASILIANA NAYE!
Utakapaokuwa
umeweka wazi sababu zako na kuziamini, weka mkakati kuwa hutaanzisha
tena mawasiliano na mwenzako. Jiwekee msimamo kuwa hutampigia simu, wala
kumtumia ujumbe wa simu, wala baruapepe na kadhalika, ila utajibu tu
yeye atakapoanzisha.
Unapomwalika
mtu au kumpigia simu au kumtumia ujumbe ni kama unamtia moyo na
kumfanya aamini kuwa unampenda na kumjali. Kama mhusika ni mtu mwenye
fahamu atashtuka kuwa jitihada zote anafanya yeye na wewe uko kimya.
Akitafakari atagundua kuwa hauko naye tena.
AKIKWITA KATAA!
Iwapo
kweli umedhamiria kumaliza uhusiano wako na mwenzako, jaribu kukataa
mialiko anayokupa, mathalani kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana.
Pia kama atasema atakufanyia jambo Fulani, kataa kiaina.
Fanya
vivyo hivyo kwa matukio yote ya kijamii. Kataaa mialiko kwa njia ambayo
hatkushtukia haraka kuwa humhitaji tena, bali aje kushtuka baadaye
atakapojumlisha matukio.
Katika
hatua za awali, hii itamaanisha kuwa utakosa kwenye matukio Fulani
ambayo wewe mwenyewe ungependelea kuyahudhuria, lakini huna la kufanya,
maana umeazimia kumaliza uhusiano wako na mpenzi au rafiki yako.
Unapotaka
kupeleka ujumbe kwa mpenzi wako kuwa hayuko tena moyoni mwako, lazima
tu ujitoleee kupata hasara katika baadhi ya mambo. Kumbuka kuwa huhitaji
tena uhusiano wako na mwenzako.