Leo
nitazungumzia suala la penzi kuchuja. Ipo hali ya kujisahau baada ya
wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya
mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba,
mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha
wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja.
Kama
huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile ambacho
ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu angalia na
sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana.
Huenda
mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti
tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu
hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea
kuzingatia hayo.
Kuna
wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo
kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi alivyo fundi wa 'kuyarudi'
ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa.
Kawaida
yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kwa ajili ya chakula cha jioni lakini
tabia hiyo hutoweka, labda kila wiki ilikuwa lazima muende 'out' mara
tatu katika kumbi tofauti za starehe na kufurahia mapenzi yenu, hali
hiyo itabaki historia tu.
Hivi
hujawahi kusikia mtu anasema "Enzi zile naanza uhusiano na mpenzi wangu
mapenzi yalikuwa moto moto, kila wiki ilikuwa lazima twende beach
lakini, siku hizi nikigusia tu kwenda huko ni ugomvi."
Maneno
kama haya huwa yananiuma sana hasa ninapogundua kwamba walio wengi
wanakuwa na nguvu ya soda pale wanapoingia katika uhusiano lakini baada
ya muda mambo hubadilika kabisa.
Sijajua
ni kwasababu gani lakini kwa utafiti mdogo ambao nilioufanya kwa baadhi
ya wanaume ni kwamba, wao wanapofanikiwa ‘kuona ndani tu’ hujenga
kiburi fulani kwa wasichana wao huku wakiamini kwamba, hata wawe tofauti
vipi hawawezi kuachwa!
Labda
nijaribu kushauri kitu katika hili kwamba, kama uko kwenye uhusiano wa
kimapenzi ama uko ndani ya ndoa, unatakiwa kufanya kila linalowezekana
kulifanya penzi lenu lisichuje.
Wewe
ndio unaweza kulifanya likaendelea kuonekana kuwa jipya kila siku ama
kulifanya likachuja mithili ya nguo inayochuja rangi iliyotumbukiza
katika ndoo ya maji ya moto.
Hatukatai
kwamba, kuna mabadiliko ya kimaslahi, pengine mtu na mpenzi wake
wameketi na kuona wanatumia pesa nyingi viwanja, kwahiyo wanaamua
kupunguza au kuacha ili kujenga maisha bora ya baadae, si unajua tena
mnapokuwa na malengo ya kimaisha zaidi?
Lakini
ukweli unabaki palepale kwamba, penzi la dhati haliwezi kuchuja hata
siku moja. Tujue wapo ambao wameishi miaka zaidi ya hamsini lakini penzi
lao bado ni moto licha ya kuwepo kwa mabadiliko madogo ambayo
hayakwepeki kutokana na umri.
Yapo
mabadiliko mengi, lakini zaidi tujirekebishe, tukumbuke kwamba baadhi
ya vitu tulivyokuwa navyo huko nyuma ndivyo viliwavutia wepenzi wetu na
kukubali kuwa nasi kwa hiyo tukiacha tunakuwa tunawakatili.