Mapenzi
yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku
na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.
Kama
huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini
nyuso zao zimetawaliwa na furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo
hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.
Lakini
pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume
anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.
Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?
Utapambana
kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana
na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia
hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye
mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii kama ifuatavyo...
CHUNGUZA
Tumia
muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao
umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa
sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu
na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza
uhusiano wake kwanza.
USITAFUTE UADUI
Baada
ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta
subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama
utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui
bure, kaa pembeni.
UNA NAFASI KWAKE?
Sawa
umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama
una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda
kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na
wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na
nafasi.
NI RAHISI KUBADILI UAMUZI WAKE?Unadhani
huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo
aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na
kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.
PINGANA NA MOYO WAKO
Ifike
wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka
kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine
utakuwa unakupotosha.
Kwa
hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye
mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya
kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.
URAFIKI NI POA?
Umempenda
sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba
tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba
angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka
kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.USIUMIE, YUPO MWINGINE
Haina
haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini
uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu
wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe
kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya
furaha.
Naomba
nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana
kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa
gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe
ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!