BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Kampeni ya kuchunguza Ebola, Casablanca, Morocco.
Shirika
la Afya Duniani (WHO) linaonya idadi ya watu waliokufa kwa ugonjwa
hatari wa Ebola imepindukia 4,000 na kama hali haikudhibitiwa haraka
zaidi ya watu milioni 1 watakuwa wameambukizwa kufikia Januari 2015.
WHO
inasema watu 4,033 wamefariki dunia kutokana na Ebola hadi kufikia
tarehe 8 Oktoba kati ya wagonjwa 8,399 waliosajiliwa katika nchi saba
duniani. Takwimu hiyo mpya inazuka katika wakati ambapo shirika hilo
likisema kuwa fedha za msaada zilizohitajika kupambana na mripuko wa
maradhi hayo zikiwa na nakisi ya dola bilioni 1.
Licha ya kwamba
takribani maambukizi na vifo vyote vimetokea barani Afrika, kuambukizwa
kwa muuguzi mmoja nchini Uhispania akiwa anawahudumia raia wawili wa
nchi hiyo waliokuwa wamerejeshwa nyumbani baada ya kuuguwa nchini Sierra
Leone na Liberia, kumeongeza wasiwasi wa kimataifa. Uhispania yaimarisha kampeni dhidi ya Ebola![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s2ISB9tbr4qup7FfncnMFs0C-L6WnL3L46-JT7X6pbTPxdARnq7Jruk7uovSdyE_aDmFFxGSNFb4gRqLlqkVEI_vYGx7fPAorwIaD5Qxs8dw=s0-d)
Uwanja wa Kimataifa wa John F. Kennedy, New York, Marekani.
Siku
ya Jumamosi (11 Oktoba), maafisa wa serikali ya Uhispania walitazamiwa
kukutana kwenye kamati maalum inayoshughulika na hali ya dharura, huku
kukiwa na miito ya kuimarishwa kwa itifaki ya afya na kuchunguza
mapungufu yaliyosababisha muuguzi huyo, Teresa Romero, kuambukizwa
Ebola.
Wafanyakazi wa huduma za afya waliliambia shirika la
habari la AFP kwamba ghorofa iliyowekwa kwenye karantini katika
Hospitali ya Carlos II mjini Madrid, ambako Romero ndiko alikoambukizwa,
ilifungwa mwaka jana kutokana na mipango ya kukata matumizi na
ilifunguliwa tena pale tu wamishionari wawili walipoletwa kutoka Afrika
wakiwa tayari wameshaambukizwa Ebola mwezi Agosti.
Waziri Mkuu Mariano Rajoy alitembelea hospitali hiyo, huku Romero akisemekana kuwa kwenye hali mbaya ingawa thabiti. Jitihada za kilimwengu ![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sltlsEZpL2SmlJnFMq_uGRNvAnjLVnarNjbip_ZrW4EG1n68J9ajRezw2tncZUkLdR5KU09gHJcfkxQtc4tumRX6aCF0S7EEraMElKhpl3oQ=s0-d)
Wanajeshi wa Marekani wakijitayarisha kuelekea kwenye kampeni dhidi ya Ebola Afrika ya Magharibi.
Kwa
upande wake, serikali ya Canada siku ya Ijumaa (10 Oktoba) iliwataka
raia wake kuondoka kwenye mataifa ya Afrika ya Magharibi yaliyoathirika
vibaya zaidi na Ebola, huku ikichukuwa hatua kali kwenye mipaka yake kwa
kuwapima wasafiri ambao wanatoka maeneo hayo.
Hatua kama hizo
zinachukuliwa pia na Uingereza na Marekani kwenye viwanja vyake vyote
vikubwa vya ndege. Taasisi ya Udhibiti wa Maradhi ya Marekani
CDC,inakisia kuwa idadi ya watu walioambukizwa Ebola inaweza kufikia
milioni 1.4 kufikia Januari 2015, ikiwa hatua kali hazikuchukuliwa
kuyadhibiti maradhi hayo.
Kutoka Australia hadi Zimbabwe, na
Brazil hadi Uhispania, watu wanaoonesha ishara za homa au waliowahi
kukutana hivi karibuni na wagonjwa wa Ebola wamewekwa kwenye vitengo
maalum vya uchunguzi au kuamuriwa kubakia majumbani mwao. Fedha zaidi zinahitajika ![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s_zNLm2E0672OAx9mZ3vtG6PdBbACb19fXbPQCU80VxgIjneW3NRUOo5VV3FIz-EXB_Ol6Xc0ALmy__y4ymPGtCj_mfx8iuxAT2WVfOnYhZw=s0-d)
Mtu anayeshukiwa kuwa na Ebola akihamishiwa hospitali nchini Brazil.
Umoja
wa Mataifa na viongozi wa mataifa yaliyoathirika vibaya kwa Ebola -
Guinea, Liberia na Sierra Leone - wametoa wito wa msaada zaidi kwenye
mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya Ebola barani Afrika.
Rais
wa Guinea siku ya Ijumaa alikutana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha
Duniani (IMF), Christine Lagarde, aliyeahidi kuwa shirika hilo "lilikuwa
tayari kufanya mambo mengine zaidi ikihitahika" katika kupambana na
maradhi hayo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan
Eliasson, alisema ni robo moja tu ya "dola bilioni moja zinazohitajika"
kupambana na maradhi hayo ndizo ambazo zimeahidiwa kutolewa hadi sasa.
Aliomba wapatikane madaktari, wauguzi na wafanyakazi zaidi wa huduma ya
afya
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Kimataifa
Monday, 13 October 2014