BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TANZANIA
imepata ushindi mnono dhidi ya Benin, wa mabao 4-1 katika mchezo wa
kirafiki wa kimataifa jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Hakizimana Louis, aliyesaidiwa na
Simba Honore na Niyitegeta Jean Bosco wote wa Rwanda, hadi mapumziko,
Stars tayari ilikuwa inaongoza mabao 2-0.
Mabao hayo yalifungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16 na kiungo Amri Kiemba dakika ya 39.
Cannavaro
alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kuruka katikati ya msitu wa
mabeki wa Benin kuunganisha kona ya Erasto Edward Nyoni kutoka kulia.
|
Juma Luizio (katikati) akipongezwa baada ya kufunga bao la nne |
Kiemba
alifunga bao zuri mno akipokea pasi ya Mwinyi Kazimoto na kuanza
‘kuwapunguza’ mabeki wa Benin kabla ya kumchambua kipa wa Benin Farnoue
Fabien.
Nyota
wa West Bromwich Albion, Sessegnon Stephanne alikuwa mwiba kwa safu ya
ulinzi ya Stars, lakini hata hivyo walifanikiwa kumdhibiti asisababishe
madhara.
Kipindi
cha pili, Benin walianza na mabadiliko wakimpumzisha kipa wao wa kwanza
mwenye umbo kubwa, Farnoue Fabien na kumuingiza Allagbe Saturnin.
Hata
hivyo, kipa huyo alitunguliwa sawa na mwenzake, mabao mawili ndani ya
dakika 45, huku Benin ikifanikiwa kupata bao la kufutia machozi.
|
Nadir Haroub 'Cannavaro' baada ya kufunga bao la kwanza |
|
Amri Kiemba kushoto baada ya kufunga bao la pili |
|
Kikosi cha Stars kilichoanza leo |
|
Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Benin |
Mshambuliaji
wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu aliifungia Stars bao la tatu dakika ya
49 akimalizia krosi fupi ya Mrisho Ngassa aliyemtoka vizuri beki wa
Benin.
Mshambuliaji
wa ZESCO United ya Zambia, Juma Luizio aliyetokea benchi kuchukua
nafasi ya Ngassa, aliifungia Stars bao la nne akimalizia kazi nzuri ya
Ulimwengu aliyemtoka beki wa Benin.
Benin ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Suanon Fadel dakika ya 90.
Stars,
leo ikitumia mfumo wa 3-4-3 ilicheza vizuri na kutawala mchezo kwa
kiasi kikubwa na ingeweza kupata ushindi mnono zaidi- kama ingetumia
vyema nafasi nyingine ilizotengeza.
Kikosi
cha Tanzania kilikuwa; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Nadir Haroub
‘Cannavaro’/Said Mourad dk75, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua,
Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba/Salum Abubakar ‘Sure Boy’dk58, Haroun
Chanongo/Said Ndemla dk77, Mrisho Ngassa/Juma Luizio dk60 na Thomas
Ulimwengu/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk86.
Benin;
Farnoue Fabien/ Allagbe Saturnin dk46, Tossavi Eric, Ore
Fortune/Dalmeida Sessy, Badarou Nana, Ogouchi Jean, Adeoti Jordan, Mama
Seibom, Sessegnon Stephanne, Pote Mickael, Djigla David/Suanon Fadel
dk49 na Dossou Jodel/Adudou Mohammed dk53.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Michezo
Monday, 13 October 2014