BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Msanii
wa muziki nchini, Rehema Chalamila aka Ray C ambaye pia alianzisha
taasisi ya kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya, ‘Ray C
Foundation’, asema kazi ya kuwaokoa vijana walioingia kwenye dibwi la
matumizi ya madawa hayo imemfanya auweke muziki pembeni.

Ray
C ameiambia Bongo5 kuwa tangu January mwaka huu alikuwa na mpango wa
kuachia kazi yake mpya lakini majukumu ya kijamii yamemzuia kufanya
hivyo.
“Baada
ya Fiesta mwezi wa kumi na moja ntatoa wimbo wangu wa kwanza, itasikika
kwa mashabiki wote ambao wananisubiria. Ilitakiwa itoke tangu mwezi wa
kwanza ila kutokana na mimi moyo wangu kuwepo kwenye kusaidia jamii
nikasema ngoja nisubiri kidogo muziki niweke pembeni nisaidie vijana
wenzangu nao watoke kwenye madawa, kwasababu ni bahati nimekuwa hai.
Nikasema kama Mungu ameniokoa basi na mimi nisaidie wengine ambao wana
matatizo na muziki niweke pembeni kwasababu muziki hauna umri. Muziki
mpaka uzee nitafanya lakini nikaona niweke pembeni kidogo.”
“Namshukuru
Mungu response ya foundation yetu imekuwa nzuri sana, watu wanaingolea
vizuri na tumeshasaidia vijana zaidi ya 50 kuingia kwenye tiba.
Tumeshaajiri vijana kibao na kua mradi pia wa Ray C Foundation kupitia
mradi wetu wa Mmgahawa ambao tumeajiri waathirika ambao wameamua
kuachana na madawa ya kulevya ambao wanaendelea vizuri. Kwahiyo naona
sasa hivi nimekuwa super hata nikirudi kwenye muziki kidogo nikitoa
wimbo na foundation nikiipekeka kwa pamoja itakuwa vizuri,” amesema Ray
C.
Ray
C ameongeza kuwa taasisi yake inafikiria kufanya harambee mapema
mwakani ili kuongeza uchumi wa tasisi hiyo ambayo kwa sasa inajiendesha
yenyewe bila msaada wowote.
“Kwa
sasa hivi tumeanza hapa Dar es Salaam lakini tunatarajia kufungua
branch tofauti tofauti mikoa yote kwaajili ya kusaidia waathirika ambao
wako mikoani huko kuweza kutoka kwenye madawa na kupata elimu ya kutosha
ili waweze kuepukana na madawa ya kulevya,” ameeleza. “Changamoto kubwa
sisi ni wafadhili, bado hatujaanza kupata wafadhili rasmi. Sasa hivi
unavyoona kila kitu nachofanya kupitia foundation yangu ni kupitia
mfukoni kwangu, sijapata mdhamini yoyote. Kwahiyo far tunataka kama
mwaka kesho kama mwezi wa pili tutajaribu kufanya utaratibu wa kuyaalika
makampuni mbalimbali na kufanya harambee kuchangia mfuko wetu ili
kuwavuta vijana wengi zaidi ambao wameathirika na madawa wa kulevya.
Kama mikoani ni lazima tusafiri, tuwasaidie watu nauli ili wengine
waweze kufika Dar ili waweze kupata tiba na baada ya hapo kuwasimamia
ili wapate ajira ili waweze kumudu mahitaji ya kawaida kwanza. Kwa
sababu wengi ambao wanaacha madawa ya kulevya wakirudi katika mazingira
magumu wanakaa na wanaweza kupotea tena. Ni lazima tuwatengezee
mazingira mazuri.”
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI