Wengi wanamjua Elton John kutokana na sauti yake nzuri awapo jukwaani ambapo nyimbo zake nyingi, zikiwemo Sacrifice na Candle in the Wind, zimemfanya atambulike dunia nzima. Kubwa zaidi, msanii huyu ni miongoni mwa watu wachache duniani waliokiri kuwa na uhusiano wa jinsia moja (shoga). Yafuatayo ni mambo kumi usiyoyajua kuhusu msanii huyu.
1. Elton Johh alianza kujifunza kupiga piano akiwa na miaka mitatu tu na akaweza kupiga vizuri ndani ya mwaka huohuo.
2. Alikuwa na tabia sugu ya utoro shuleni ingawa licha ya kutohudhuria masomo, alikuwa akifaulu kwa kiwango cha juu.
3.Wazazi wake walikuwa wakipigana mara kwa mara na akiwa na umri wa miaka 14, walitalikiana. Mama yake akaolewa na mwanaume mwingine, Fred Farebrother ambaye ndiye aliyemsaidia sana Elton kwenye sanaa ya muziki.
4. Akiwa na umri wa miaka 15 tu, alianza kufanya shoo kwenye baa iliyokuwa jirani na kwao, Northwood Hills Hotel akilipwa ujira wa pauni 35 kwa wiki.
5. Mwaka 1979, Elton John aliweka historia ya kipekee ya kuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kutoka nchi za Magharibi, kwenda kufanya shoo Urusi na Israel.
6. Mwaka 1986, alipatwa na tatizo la kukauka sauti akiwa ziarani nchini Australia, alipoenda kupimwa akabainika kuwa na kansa ya koo, akafanyiwa upasuaji na kuanzia hapo, sauti yake ikabadilika kabisa.
7. Alianza kuandamwa na kashfa za ngono mwaka 1987 ambapo inadaiwa alikuwa akiwakodi vijana wa kiume kwa ajili ya kufanya nao ngono ya jinsia moja.
8. Japokuwa Elton aliwahi kumuoa mwanamama Linda Woodrow, ndoa yao haikudumu, wakatengana na tetesi juu ya ushoga zikazidi kuwa kubwa.
9. Mwaka 1988, Elton alijitangaza hadharani kuwa shoga, taarifa zilizopokelewa kwa mshtuko mkuba dunia nzima.
10. Mwaka 1993, alianzisha uhusiano wa kimapenzi na David Furnish ambaye baadaye walikuja kufunga ndoa ya jinsia moja mwaka 2005. Wawili hao wamedumu mpaka leo na wana watoto wawili, Zachary Jackson Levon Furnish-John na Elijah Joseph Daniel Furnish-John.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

