Kweli Jumapili asubuhi mapema jamaa akaamka na kuanza kufanya matayarisho ya kwenda kanisani, mkewe akabaki amelala. Alipokuwa tayari tu ndugu yetu huyoo kakwea daladala hadi kituo karibu na kanisani. Ile kufika uwanja wa kanisa akawa anashangaashangaa maana hajafika kanisani siku nyingi, ghafla rafiki yake wa toka utoto akatokea wakaongea machache na kuingia kanisani. Muda si mrefu ibada ikaanza.
Unajua siku hizi kuna watu wengine wa ajabu sana, utakuta mtu anaingia kanisani na simu yake ya Kichina ina mlio wa muito mkubwa utadhani redio ya bodaboda, halafu unamkuta haiweki ‘silent’, basi ikipigwa hiyo kanisa zima mara mnajikuta mnasikiliza ngololo, basi tabu tupu, na ndilo lililotokea ghafla wakati jamaa yetu kainama anamuomba Mungu amsamehe na kumsaidia katika maisha, kuna simu ilianza kuita, taarabu ya mipasho ya Bi Khadija Kopa ikatanda, unasikia sana, basi ule mlio ukamzindua jamaa yetu akakumbuka simu yake.
Loh akachanganyikiwa, alikuwa kaisahau bafuni alipokwenda kuoga, na ilikuwa na mabomu mkewe angeyaona tu, dunia ingesimama kuzunguka. Kanisani hapakufaa tena, jamaa alichomoka utadhani kaambiwa Boko Haram wameliteka kanisa. Kafika barabarani anaangalia huku na kule kungoja daladala akaona hakuna dalili, upesi kakwea bodaboda huku anamuamrisha dereva.
“Kimbiza sana kuna uwezekano wa msiba mkubwa nikichelewa kufika nyumbani”. Ndani ya dakika tano jamaa alikuwa nyumbani kwake, kaingia haraka moja kwa moja bafuni. Akaikuta simu palepale alipoiacha, kucheki hivi hakuna ‘missed call’ wala meseji mpya, roho ikatulia. Akajiuliza “Mke wangu angeikuta hii simu..” lakini kwa woga akaingia chumbani kwake na kumkuta mkewe bado kalala.
Mkewe akashangaa kumuona mapema, akamuuliza, ‘Hee vipi baba umesharudi kanisani?”
Jamaa akajibu kwa kujiamini “Nilikuwa njiani padri kanitumia meseji, eti leo anaumwa hivyo hakuna ibada, hawa mapadri wa siku hizi wa ajabu sana mke wangu, siyo kama enzi zetu”
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

