Habari Kali
Loading...

MISS TANZANIA 2014 ACHA KABISA

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Acha kabisa! Fainali ya lile shindano kubwa la mrembo wa Miss Tanzania 2014 limechukua nafasi usiku wa kuamkia jana, Jumapili ambapo Ijumaa Wikienda lilikuwepo ndani ya eneo la tukio kukukusanyia matukio yote yaliyojiri mbele na nyuma ya pazia hivyo lina full story.
Warembo 30 walioshiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, wakionesha shoo ya kufa mtu.
WAREMBO 30
Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania na Mkurugenzi wa Lino International, Hashim Lundenga ‘Anko’ kukaribisha wageni waalikwa, warembo 30 walioshiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, walionesha shoo ya kufa mtu kupitia kwa msanii wa nyimbo za asili, Wanne Star.
Vanessa Mdee akifanya makamuzi jukwaani
VANESSA AFUNIKA
Kabla ya mambo mengine kuendelea, Vanessa Mdee alifunika kwa bonge la shoo alilokamua , akisindikizwa na wacheza shoo wake wawili ambao walikamua ile mbaya.
MVUTO KWENYE PICHA
Aliyeibuka kidedea kwenye kipengele hicho ni Evelyn Bassah huku Kipengele cha Top Model, mrembo Jihan Dimach akijitwalia taji.
Warembo walifanikiwa kuingia Top Five.
KIPAJI
Katika Kipengele cha Miss Talent (kipaji), taji lilikwenda kwa Nicole Sarakikya, Elizabeth Tarimo akaibuka kidedea kwenye Kipengele cha mwanamichezo mwanamke (Sports woman) huku Miss Personality ikitwaliwa na Salama Saleh.
KIFUTA JASHO
Baada ya kuenguliwa warembo 15, wale top 15 waliosalia walilamba Sh. laki saba kila mmoja kama kifuta jasho.
TOP 5
Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye Tano Bora ni Jihan Dimach, Siti Mtemvu, Dorice Mollel, Nasreen Abdul na Lilian Kamazima.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia shoo.
WAVALISHWA KAMA NDEGE TAUSI
Bila shaka unawajua ndege tausi hasa wale wanaoonekana pale Ikulu ya Magogoni. Warembo hao walioingia Top 5 walikuwa wamevalishwa kama ndege huyo isipokuwa rangi kwa namna walivyoonekana jukwaani.
MREMBO AMWAGA KIFARANSA
Wakati wa kipindi cha maswali na majibu, mrembo Siti Mtemvu aliwaacha watu midomo wazi aliposema atajibu kwa Kiingereza lakini baada ya kumaliza kumwaga ung’eng’e, akamalizia kwa kutema Kifaransa.
Meza ya majaji ikijipanga kutoa uamuzi wa mwisho katika kinyang'anyiro hicho.
MWINGINE ACHEMKA
Naye mrembo mwingine, Nasreen Abdul alijikuta akichemka kujibu maswali hivyo kuzomewa hasa pale alipochanganya kati ya maneno tourism (utalii) aliloulizwa na terrorism (ugaidi).
JIHAN ALA SHANGWE
Kwenye ‘segmenti’ ya maswali na majibu, mrembo Jihan alijikuta akipokea shangwe la kufa mtu kwa kujibu vizuri kwa ung’eng’e.
Siti Mtemvu (Miss Tanzania 2014 ) akiwa na anyedaiwa ni baba yake, Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu.
VITUKO VYATAWALA
Vituko vilivyojiri vilikuwa vingi kwa mfano katika shoo ya msanii Vanessa Mdee aliyetumbuiza katika shindano hilo, alijikuta akiachia  ‘nido’ moja nje wakati akicheza na kuchafua hali ya utulivu, akaibua zomeazomea ya ‘weweeeee’.
nyuma ya pazia
Kituko kingine ni cha mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash kutinga ukumbini akiwa ameongozana na kale kabinti ambako katika siku za hivi karibuni, amekuwa akionekana akiwa beneti nako bila Lady Jaydee kujua.
Ommy Dimpoz akipiga shoo katika fainali hizo
Baada ya shoo kali ya Ommy Dimpoz, washiriki walioingia fainali, walipanda tena jukwaani ambapo Mkurugenzi wa Lino International, Hashim Lundenga naye  alipanda jukwaani na kuanza kuwatangaza washindi, kuanzia namba tano mpaka namba moja.
Nasreem Abdul alishika nafasi ya tano, nafasi ya nne ikaenda kwa  Dorice Mollel.
TOP THREE
Jihan Dimach alitangazwa kuwa mshindi wa tatu (second runner up) wakati Lilian Kamazima, alishika nafasi ya pili (first runner up).
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania na Mkurugenzi wa Lino International, Hashim Lundenga ‘Anko' (kushoto) akisimamia shoo.
Nafasi ya kwanza, ilishikwa na Siti Mtemvu, mrembo kutoka Temeke ambaye alitawazwa kuwa Miss Tanzania 2014 na kuvalishwa taji na Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanya.
Pia Siti alijishindia shilingi milioni 18 za Kitanzania kama zawadi kwa ajili ya mshindi wa kwanza huku Lilian na akiondoka na shilingi milioni 6 za Kitanzania na Jihan akiambulia milioni 4.2.
MSHINDI ALIJULIKANA MAPEMA?
Swali kubwa ambalo wadau wengi wa mashindano ya umiss Tanzania walijiuliza usiku huo ni kwamba, je, mshindi alijulikana mapema?
Mashabiki wakipigia debe na kutoa sapoti kwa Mrembo Siti Mtemvu katika kinyang'anyiro hicho.
Viashiria vya mapema vilionesha kwamba, Siti ambaye inadaiwa ni mtoto wa Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu angeibuka mshindi kutokana na jinsi alivyokuwa akishangiliwa kwa nguvu huku wapambe wake wakiinua vipeperushi vyenye picha ya mshiriki huyo, hali ambayo haikuwepo kwa wenzake.
Waandishi: Issa Mnally, Gabriel Ng’osha na Musa Mateja

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top