Habari Kali
Loading...

MATATIZO YA UGONJWA WA MOYO WA KUZALIWA (CONGENITAL HEART DISEASE) -3

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >


Wiki iliyopita tuliona sehemu ya pili ya matatizo haya ya ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao. Leo tunamalizia sehemu iliyobakia.
Tatizo hilo huweza kugunduliwa pia wakati watoto wanapokuwa wadogo kutokana na kuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida wakati wa vipimo hospitalini.
DALILI
Moja ya dalili za tatizo hilo  ni kupumua kwa shida hasa wakati wa mazoezi, kupata maambukizi ya mara kwa mara ya mfumo wa kupumua kwa watoto, kuhisi mapigo ya moyo kwenda kasi, uchovu, kujaa miguu au kuvimba tumbo na ngozi kuwa ya bluu.
MADHARA
Madhara ya kuwepo tundu kwenye kuta za juu za moyo ni kupata shinikizo la damu la mapafu (yaani Pulmonary Hypertension).
Tatizo lingine la kuwa na tundu katika upande wa juu wa moyo ( Eisemnenger Syndrome). Hii ni hali inayotokea wakati mkondo wa damu kutoka upande wa kushoto wa moyo unapoelekea upande wa kulia kupitia kwenye matundu yaliyo kwenye kuta zinazotenganisha chemba za moyo.
 Hali hiyo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya mapafu na kusababisha ongezeko la shinikizo la damu katika mapafu, hali inayosababisha kuongezeka pia shinikizo la damu katika upande wa kulia wa moyo.  Madhara mengine ni upande wa kulia wa moyo kushindwa kufanya kazi vizuri na pia hatari ya kupata kiharusi.
Wajawazito wenye tundu katika kuta za juu za moyo (ASD) huweza kuvumilia hali hii na kuendelea na ujauzito bila matatizo yoyote lakini kwa wale ambao wameshapata madhara, huwa katika hatari ya kupata madhara zaidi katika ujauzito.
Hivyo kwa wale ambao wameshapata madhara hushauriwa kutoshika mimba kwa sababu huweza kuhatarisha maisha yao.
MATIBABU
Matibabu ya awali kwa watu wenye tatizo la kuzaliwa na tundu katika kuta za juu za moyo au Atrial Septal Defect (ASD) ni kupewa dawa ili kupunguza matatizo yanayosababishwa na hali hiyo.
Kuna dawa mbalimbali zinazotumika kutibu lakini mtu anapogundulika kuwa na tundu katika kuta za juu za moyo anaweza kuchunguzwa ili kuona kama anaweza kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha hali hiyo au la.
Imeonekana kuwa upasuaji kwa ajili ya kuziba tundu la ASD huwa wa mafanikio iwapo mgonjwa bado hajapata matatizo ya shinikizo la damu katika mapafu. Yaani pale ambapo shinikizo hilo la damu bado liko chini ya 40 mm Hg.
Lakini iwapo Eisemnenger Syndrome imetokea na kupata shinikizo la damu upande wa kulia wa moyo, mara nyingi upasuaji huwa hauna mafanikio kwa mgonjwa.
Iwapo tundu la ASD katika moyo litafungwa kabla ya mtu kufikia umri wa miaka 25 huwa halina madhara makubwa.
Mbali na upasuaji, urekebishaji wa tundu hilo la moyo pia huweza kufanywa kwa njia ya kupitisha mrija  wa catheter kwenye mshipa wa damu wa femoral hadi kwenye moyo na kupachikwa kiraka katika tundu hilo na kurekebisha tatizo hilo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top