Ni maisha ya huzuni! Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu aondokewe na mkewe kipenzi, Shuea Hamis ’Mama Shuu’, Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Choki, kwa mara ya kwanza amefunguka mazito kuhusiana na maisha anayoishi sasa.
Mke wa Choki alifariki dunia hivi karibuni baada ya kusumbuliwa na miguu na fangasi iliyosambaa kwenye damu.Akizungumza na Ijumaa katika spesho intavyu, Choki anasema maisha yake kwa sasa ni magumu kuliko kawaida kutokana na ukweli kwamba alikuwa amemzoea mama Shuu aliyekuwa akishirikiana naye katika mambo mengi.
Anasema: “Kama ni kunitesa kwa kweli ananitesa sana. Kila ninapoingia chumbani naiona sura yake, wakati mwingine najihisi kama niko naye lakini kumbe ndiyo sitamuona tena.
“Hili ulisikie kwa mwenzako tu, kuna ugumu sana kufiwa na mke, nateseka sana.
MAMBO YAMEYUMBA?
“Mke wangu alikuwa ni nguzo muhimu sana hasa katika mambo ya biashara zetu.”
Choki alisema mkewe alikuwa ni nguzo kubwa kwake katika suala zima la biashara mbalimbali walizokuwa nazo. Walikuwa wanafanya biashara zao kwa pamoja lakini kwa sasa zimeyumba na kila kitu kimetikisika hivyo anamuomba Mungu akimaliza arobaini, aanze kujipanga tena.
Choki aliendelea: “Baada ya arobaini tutakaa na familia tujue tunafanyaje, naamini tutaendelea tu, kikubwa namuomba Mungu sana na kujipanga, itawezekana na bendi itaendelea.”
CHOKI ANA MPANGO WA KUOA TENA?
“Ukweli sijui, kwa sasa hivi kwanza nitakaa hivihivi maana kumpata mtu kama mkweli na mwenye mapenzi ya dhati, moyo mzuri kama Mama Shuu ni ngumu sana kwa dunia ya leo, kikubwa ninajipanga kwanza katika kazi na kuendeleza biashara tulizokuwa tukifanya pamoja.”
KUMBE BANZA ALISUSIA MSIBA?
“Kilichonihuzunisha ni kwamba Banza Stone (Ramadhan Masanja) hakuonekana msibani hata wakati alipokuwa akiugua mke wangu ndiye alikuwa kiongozi wa kwanza kusema tukamuone na kumsaidia, sijagombana naye wala nini.
“Ukweli alivyofanya siyo vizuri kama ingekuwa ni mimi nimefanya hivyo ningelaumiwa sana na watu mbalimbali lakini kwa yeye inaonekana sawa tu, jamani hata kama amehama bendi angekuja tu mbona wanamuziki wengine wa bendi tofauti walikuja? Kuhama bendi siyo ishu, ishu ni ubinadamu lakini sijafurahishwa na kitendo hicho, kinaniuma na kunihuzunisha sana.”
ANAZUNGUMZIAJE BANZA KUJIENGUA KWENYE BENDI YAKE?
“Ninawatakia kila la heri yeye na Athanas ambaye wameunda naye kundi moja, unajua mara nyingi kumfadhili binadamu ni ngumu, kama ameona anaweza kuongoza kundi haina shida na mtu hakatazwi kuanzisha bendi au kundi lake maana ni sehemu ya maendeleo.”
EXTRA BONGO ITAENDELEA?
“Tutajipanga tu sisi kama Extra Bongo na tutasimama kwa uwezo wa Mungu kwani hakuna linaloshindikana kwake hivyo baada ya kumaliza arobaini itakayofanyika Novemba 14, mwaka huu ndipo tutaendelea na michakato.”
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

