KIMENUKA!
Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu
kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine
yameibuka!
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja.
Miongoni
mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita
nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ni
madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa ‘neno
la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa
Wema, Kajala Masanja.
KUNASWA KWA SAUTI NA PICHA
Baada
ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii
ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi
Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa
mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya
shilingi milioni 13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na
zuio la kisheria.
Wema Sepetu akiwa na mama yake.
KAJALA AAMUA ZITO
Katika
kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya
kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema.
Chanzo
chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na
familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa, timu hiyo na
Timu Wema wameingia vitani tena.
“Kajala
ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake, wao
wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika
sana.“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu
kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata
kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
Wema Sepetu akiwa na Kajala Masanja.
MATUSI YENYEWE
Katika
sauti, mama Wema anasikika akitamka matusi (hayaandikiki gazetini)
huku Wema naye anasikika akimsihi mama yake asimtaje jina Kajala kwa
kuwa kufanya hivyo ni kumpaisha. Hapa inamaanisha kwamba, Wema alitaka
mama yake afunguke lakini bila kutamka jina la mtu.
AGUNDUA TIMU KAJALA IMO NDANI YA BETHIDEI
Katika
hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba Timu Kajala
ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya huku najua humu
ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi mazito)”
KAJALA SASA
Baada
ya madai hayo yote, juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili
kumuuliza ukweli wa madai hayo. Licha ya kutopokea simu ya paparazi
wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila kitu.
Hata
hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama kumi na
tano alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo anadai
kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali iliyotafsiriwa kuwa
kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani, nimemkosea nini mama Wema?’
Mama yake Wema Sepetu.
ALICHOKIFANYA MARTIN KADINDA
Katika
hatua nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda alikuwa na
kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema na mama Diamond, Sanura Kasim
‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha ya kwamba watoto wao
wamependana.
“Kadinda
ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba mama Wema na
mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa nini, kwani hawa si watu
ambao watoto wao wana mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa mmoja.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Katika
bethidei hiyo, Wema alizawadiwa magari mawili, Nissan Murano lenye
thamani ya shilingi milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW 545i lenye
thamani ya shilingi milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na Kadinda!