Rashidi alisema kwamba alipofika 
Muhimbili alishangaa alipojikuta akiwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa 
kwa muda na madaktari akidaiwa ni mwizi wa mtoto.Alisema, aliwaonyesha 
kadi ya kliniki ya mtoto Zainabu yenye jina lake (Rashidi) akiwa ndiye 
baba mzazi wa mtoto huyo, jambo ambalo madaktari hao walilishangaa. Bw. Rashidi akiwa amembeba mwanaye, Zainabu Rashidi.
Bw. Rashidi akiwa amembeba mwanaye, Zainabu Rashidi.
Hata hivyo, madaktari hao walimwachia kwa sharti la kutopatiwa cheti 
cha kuzaliwa hadi ampeleke Paulo Mlela ambaye jina lake lipo kwenye 
makabrasha hospitalini hapo likionyesha naye ni baba mzazi wa Zainabu.
Katika kudadisi, Rashidi alionyeshwa fomu 
ya discharge (kuruhusiwa) baada ya mkewe kujifungua iliyoonyesha jina la
 Paulo Mlela kama mume wa Fatuma badala ya jina lake, jambo 
lililomchanganya na kuamua kufuatilia ukweli kwa mkewe ambaye alikataa 
tuhuma hizo na kudai kuwa hakuwa akijielewa wakati fomu hiyo ilipokuwa 
inajazwa kwa kuwa alikuwa ametoka kujifungua.
Rashidi alisema kuwa siku mkewe alipokuwa 
anajifungua yeye na ndugu zake wa karibu walikuwa safarini mazishini 
hivyo huenda mwanaume huyo alipata nafasi ya kuingiza jina lake. Rashidi
 alisema aliamua kumtafuta Paulo kisirisiri ndipo akagundua kuwa anaishi
 mtaa wa pili kutoka nyumbani kwake na mara kadhaa aliwahi kumwona akiwa
 na mkewe.
Akizungumzia hatua ambazo alizichukuwa, 
Rashidi alidai kuwa amelifikisha suala hilo polisi na baraza la kata 
ambako linashughulikiwa kupitia ustawi wa jamii.Rashidi aliongeza 
kwamba, kwa sasa mkewe ameondoka nyumbani.
Nao ndugu wa mwanamke walipotafutwa kulizungumzia suala hilo, 
walisema wanamtambua Rashidi kama baba halali wa mtoto Zainabu huku 
wakimkataa Paulo. Waliomba kwamba, kwa kuwa Rashidi amejua ukweli na 
kwamba mtoto ni wake basi akae na mkewe wayamalize maisha yaendelee 
kwani wametoka mbali.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== > 


