Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.
Na Nicodemus JonasSHIRIKISHO la Soka Uganda (Fufa), limetajwa kuwa chanzo kikuu cha kuchelewa kwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, kuungana na wenzake kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Afrika Kusini, kufuatia kushindwa kutuma barua rasmi kuhusiana na kuachwa kwa mchezaji huyo.
Okwi, aliitwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa, The Cranes, kilichomenyana na Togo Jumamosi iliyopita katika michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika, hata hivyo, baadaye alitemwa kwenye kikosi cha Kocha Milutin Sredojević ‘Micho’ kitakachoivaa tena Togo leo.
Mpaka jana, Okwi ndiye mchezaji wa Simba, ambaye alikuwa hajafika kambini, baada ya wale wa Taifa Stars kuungana na wenzao juzi Jumatatu.Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Humprey Nyasio, alisema kuwa mpaka jana Okwi alikuwa nchini Uganda.
“Okwi bado hajafika kambini kuungana na wenzake na sisi tunamfanyia taratibu zote ili kati ya leo (jana) au kesho (leo) aweze kuungana na wenzake.
“Kikubwa kinachokwamisha ni kwamba tumepata taarifa za kutemwa kwenye timu ya taifa, lakini hazijaja rasmi, kwa hiyo sisi tunasubiria barua kutoka kwa shirikisho la nchini mwao kuhusiana na kuondolewa kwake na muda wowote baada ya kupata taarifa rasmi tutamfanyia taratibu haraka iwezekanavyo ili aondoke,” alisema Nyasio na kuongeza kuwa huenda nyota huyo wa zamani wa Yanga akapitia hukohuko Uganda.
Iwapo taratibu hizo zitakamilika leo, ina maana Okwi atajiunga na wenzake kwa siku moja ya Alhamisi kabla ya kikosi hicho kurejea Ijumaa, tayari kwa mchezo na watani wao Yanga, utakaopigwa Jumamosi wiki hii au akaja kuwasubiri Dar.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

