KIFO cha
mfanyabiashara aliyeshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari,
Ukonga jijini Dar es Salaam, Liberatus Damiani Temu (55) kilichodaiwa
kilitokana na kipigo kutoka kwa askari wa kituo hicho sasa ukweli
umejulikana.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Liberatus Damiani Temu (55) anayedaiwa kufariki kiutata.
Chanzo
makini kililiambia gazeti hili kuwa utata wa tukio hilo ulianzia mbali
kwani Mei, mwaka huu, marehemu alimgonga na gari mtu mmoja anayefahamika
kwa jina la Hamis Magoma na kujeruhiwa vibaya.
Mke wa marehemu, Naomi Liberatus (katikati) akihuzunika kwa kumpoteza mwenzake.
Baada
ya kusababisha ajali hiyo, ilidaiwa marehemu Liberatus alifuatilia
masuala ya bima ili aweze kumlipa aliyemgonga ambaye pia anatajwa kuwa
mteja mzuri katika Baa ya Meku iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu.
Naomi Liberatus akiwa amezimia wakati wa mazishi.
Chanzo
kinasema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, hali ya Magoma iliendelea
kuwa mbaya hadi Agosti 22, mwaka huu saa tano usiku marehemu
alipokamatwa na kufikishwa kituoni hapo akidaiwa kumjeruhi Magoma kwenye
ajali.
Padri akiiombea roho ya marehemu ya marehemu (Liberatus Damiani Temu).
Mke
wa marehemu, Naomi Liberatus aliyezimia mara mbili wakati wa mazishi,
alisema mumewe ambaye kwa kipindi chote tangu apate ajali hiyo, alikuwa
hafanyi shughuli yoyote, alikataliwa kupewa dhamana kwa madai kuwa
majeruhi (Magoma) alikuwa na hali mbaya.
Mwili wa marehemu Liberatus Damiani Temu ukichukuliwa kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
Kuhusu
hatua nyingine ilidaiwa kuwa marehemu akiwa mahabusu aligonga kichwa
chake kwa nguvu ukutani, hali iliyosababisha wenzake kupiga kelele za
kuomba msaada na kwamba baada ya askari kufika na kukuta hali ilivyo,
walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu ambako alifariki
dunia.
Marehemu Liberatus Damiani Temu enzi za uhai wake.
“Watu
wanasemasema tu kwamba Liberatus aliuawa na askari, si kweli. Kwa nini
tumuue? Kwa kosa lipi? Sisi tulimshikilia kwa sababu hali ya majeruhi
aliyemgonga ilikuwa mbaya, hivyo kumweka mahabusu marehemu ilikuwa kwa
ajili ya usalama wake pia.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua jambo.
“Wengi
wanaamini kila anayewekwa mahabusu ni mhalifu wa kiwango cha kuteswa na
polisi, si kweli. Wengine wanakaa hapa ili kuwalinda. Wewe ukiua
unadhani ndugu wa marehemu watakuacha?” alisema askari mmoja wa kituo
hicho bila kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji mkuu.
Alisema kuwa
mahabusu waliokuwa na marehemu ni mashahidi wakubwa kwamba jamaa
alijigonga kichwa ukutani lakini kabla ya kufanya hivyo, alikuwa
akisemasema maneno mengi kama aliyechanganyikiwa.
Hata
hivyo, marehemu amezikwa akiacha maswali kibao, watu wanajiuliza je,
kilichosemwa na polisi ndiyo ukweli au la! Kufuatia utata wa kifo hicho,
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameunda
tume kufuatilia sakata hilo.