Kwa wale ambao ni mara ya kwanza wanatupia macho kwenye ukurasa huu, hoja inayoendelea ni kwamba, kabla ya kuachana na mtu ambaye ni sehemu ya maisha yako lazima ujiulize maswali 10.
Lengo hasa la kukuletea maswali haya ni ili kutibu migogoro ambayo inaweza kuwakosesha furaha na kusababisha mihemko ya hasira ambayo madhara yake ni makubwa.
Utakumbuka wiki iliyopita niliishia kwenye swali namba nane ambalo ni je, unajua kupima mahitaji yako kwa kuunganisha uhusiano wako? Hapa nilimaanisha kwamba, asilimia kubwa ya watu huvunja uhusiano wao kwa sababu tu ya kushindwa kupima mahitaji yao kwa kuunganisha kwenye mzani mmoja wa hitaji la uhusiano wako.
Ukweli ni kwamba, mapenzi yanataka upokee kama wewe unavyotoa. Ikiwezekana wewe uwe msitari wa mbele kwenye kutoa ndiyo ukae mkao wa kupokea.
Hakika uhusiano ambao unajengwa na watu wawili wenye ubinafsi unakosa mbolea ya kutosha. Hata kama utadumu, hauwezi kuwa na rutuba inayostahili. Nikushauri tu kwamba, katika uhusiano wako wa kimapenzi hata siku moja usikubali ukose maelewano.
Hakikisha kadiri kila siku zinavyosogea, unaridhika na kile ambacho kinaendelea ndani ya uhusiano wako na siyo ili mradi siku zinakwenda.Tuhamie sasa kwenye swali la nane.
JE, TABIA ZAKO ZA ZAMANI ZINAATHIRI UHUSIANO WAKO ZA SASA?
Hili nalo ni swali muhimu sana la kujiuliza na majibu yake uyafanyie kazi kabla ya kuchukua uamuzi wa kuachana. Kumbuka kila mmoja ana vijitabia vyake ambavyo vingine vinaweza kuwa na madhara makubwa kwenye uhusiano kama vitapewa nafasi.
Yawezekana kabla ya kuingia kwenye uhusiano wako wa sasa, ulishawahi kuwa na mtu huko nyuma na kuna tabia ambazo ulikuwa nazo, ukazikumbatia na zikasababisha mwenza wako akashindwa kuzivumilia na kuamua kukuacha.
Kikubwa hapa ni kuzibaini na kuanza kuzifanyia kazi ukijua kabisa mwenza wako hawezi kuzivumilia. Naye pia kama ni muelewa, akigundua umezijua tabia zako zenye madhara kwenye uhusiano na unajaribu kuzifanyia kazi, lazima atakupa muda wa kuwa na wewe.
Kwa mfano, yawezekana kwenye uhusiano wako uliopita ulikuwa ukijifanya wewe ndiye mwenye sauti, ukitaka kila unachokisema wewe mweza wako asipinge. Huenda alikuvumilia lakini baadaye akaona akuache uende.
Kwenye uhusiano wako wa sasa ukiendelea na tabia hiyo ni lazima mambo yatakwenda mrama.
Kubali kwamba vijitabia vyako vya ajabuajabu ulivyokuwa navyo kama hutavifanyia kazi na ukavihamishia kwenye uhusiano mwingine, yatakuwa ni yaleyale na matokeo yake utakuwa ni mtu wa kubadili wapenzi kila siku.
Itakuwa hivyo kwa kuwa, hakuna atayeweza kuvumilia tabia zako mbaya. Awali atakupa nafasi ya kuzigundua na kubadilika, kama hutafanya hivyo atakuacha.
Akikuacha, utakwenda kwa mwingine, nako ukiendelea na vijitabia hivyo, ukae mkao wa kuwekwa pembeni.
Itaendelea wiki ijayo.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

