Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa, Askofu Bundala, alisema kuendelea
kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba ni kuzalisha maswali mengi
yatakayowafanya wananchi kuwa na shaka na serikali.
“Ikumbukwe
kuwa katiba siyo mali ya wanasiasa, katiba ni mali ya Watanzania wote
na kwa manufaa ya vizazi vijavyo, hivyo hakuna sababu yoyote ya kutumia
nguvu kuendelea na vikao vya katiba…
“Kwa
kuwa mwenye sauti ya mwisho katika katiba ni rais bora atangaze
kulivunja…kama ni suala la fedha ziwe ni za ndani za wafadhili ni bora
zikaelekezwa kwa matumizi mengine au kama hiyo haiwezekani kwa kuwa ni
za wafadhili zirudishwe fedha zao kuliko kuendelea na jambo ambalo
halina manufaa kwa Watanzania na badala yake wananufaika watu wachache,”
alisema Askofu Bundala.
Aliongeza
kuwa uwepo wa mvutano kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) uliofanya wajumbe wa UKAWA kugoma kurejea
kwenye vikao hivyo, ni bora Bunge likavunjwa ukatafutwa mwafaka wa
kweli.
Askofu
Bundala alishauri kuwa ikishindikana kupata mwafaka, suala la katiba
lirudishwe kwa wananchi watoe maoni yao kwa mara nyingine.
Alisema
suala la mchakato wa katiba linahitaji uwepo wa nguvu ya Mungu wala
siyo suala la kibinadamu na kuchukuliwa kama sehemu ya ushabiki, hivyo
kuna kila sababu ya viongozi wa kiroho kufanya kazi kubwa ya kuliombea
suala hilo.
“Hapa
inatakiwa kuelewa kuwa katiba siyo lelemama, kunatakiwa maombi, hata
hivyo suala la katiba linafanywa kama vile kinatungwa kitabu cha hadithi
bila kujua katiba ya nchi ni roho ya nchi, kutokana na msuguano uliopo
kwa sasa ni bora vikao vya katiba vikasitishwa huku wachaMungu wakifanya
maombi ili Mungu aweze kuonyesha nia ya dhati ya upatikanaji wa katiba
mpya…
“Wanasiasa
wasiyumbishe nchi na mawazo ya wananchi yanatakiwa kuheshimiwa ili
wananchi hao waweze kuwa na maamuzi yao kulingana na kile wanachokiamini
kuwa kinaweza kuwa msaada mkubwa katika kuwaondoa katika hadha kubwa
ambayo wanakutana nayo,” alieleza Askofu Bundala.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

