Habari Kali
Loading...

Gari lililobeba MAITI kumi laua watu Wawili Mikese

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Gari la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lililokuwa likisafirisha maiti 10  za watu kwenda katika Hospitali ya Mtakatifu Francis Ifakara, wilayani Kilombero, limewagonga watu wawili waliofariki dunia papohapo, eneo la Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro. 
 
Waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea saa 5:25 asubuhi jana ni dereva na abiria wa bodaboda.
Maiti hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika mifuko maalumu ya plastiki, zinaelezwa kuwa zilikuwa zikipelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, ili zitumike kwa mafunzo.
Akizungumzia ajali hiyo katika eneo la tukio, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Pankrasi Pascal, mkazi wa Ifakara, wilayani Kilombero.
 Mbao  aliwataja waliokufa kuwa ni Shaaban Rajabu na Ally Benulo, wakazi wa Kijiji cha Mikese, waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki.
Tukio hilo limekuja siku kadhaa baada ya mabaki ya miili ya binadamu kugunduliwa ikiwa imetupwa katika dampo moja lililoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 Chuo kimoja cha mafunzo ya udaktari wa magonjwa ya binadamu, kilihusishwa na tukio hilo lililozua hofu kwa wakazi wengi wa jiji hilo.
gari
 Kamanda Mbao alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa gari ambaye kwa sasa,  anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Kuhusu maiti 10 zilizokutwa kwenye gari hilo, ofisa huyo wa polisi alisema wanafanya mawasiliano ili kupata usafiri wa kuzifikisha katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, ilipokusudiwa.
Mashuhuda wa ajali hiyo walisema chanzo ni mwendokasi wa dereva wa gari, huku wakilalamikia kukithiri kwa  ajali katika eneo hilo.
 Walisema ajali hizo zimekuwa zikisababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia na kwamba kuna haja Serikali kuweka matuta na vibao vya kuashiria kona zilizopo eneo hilo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top