Habari Kali
Loading...

Rais wa Malawi kumuoa mpenzi wake wa muda mrefu…

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Rais Mutharika (kulia) ana umri wa miaka 74
Rais Mutharika ana umri wa miaka 74
Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika anatarajiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa muda mrefu,mwishoni mwa wiki.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Rais.
Taarifa hiyo ilisema: ”Ikulu ya Rais ina furaha kuwajulisheini kuhusu harusi ya kitamaduni itakayofanywa kati ya Rais Arthur Peter Mutharika na mwandani wake wa muda mrefu Madam Gertrude Hendrina Maseko.”
Taarifa hii iliwasilishwa na msemaji wa Rais Chikondi Juma aliyesema kuwa sherehe ya harusi itakuwa ya faragha.
Rais Mutharika aliibuka mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi jana ambapo mshindani wake mkubwa alikuwa rais aliyeondoka mamlakani Joyce Banda.
Rais Mutharika amewaambia maafisa wa serikali kuhakikisha kuwa hakuna pesa za serikali zitatumiwa katika shughuli hiyo.
Wa Mutharika ni Rais wa pili kufanya harusi akiwa mamlakani nchini Malawi
mutha 2
Mutharika, mwenye umri wa miaka 74 na ambaye mkewe alifariki , ana watoto watatu, wasichana wawili na mvulana mmoja.
Baadhi ya wadadisi wanaunga mkono harusi ya Mutharika wakisema kuwa itasaidia kuimarisha maisha ya kijamii na kisiasa kama kiongozi wa nchi.
Hii ni mara ya pili kwa Rais kufanya harusi akiwa mamlakani nchini humo.
Wa kwanza alikuwa Rais Bingu Wa Mutharika,aliyemuoa mpenzi wake Callista Chimombo, aliyekuwa waziri wa zamani wa utalii mwaka 2010.
Wa Mutharika alikuwa nduguye mkubwa rais Peter Mutharika.
Hata hivyo wakosoaji wanalalamika kuwa pesa za umma zitatumika kwa harusi hii kwa sababu shirika la habari la taifa lilatumika kupeperusha matangazo ya harusi hiyo moja kwa moja.
Pia wanasema kuwa Rais Mutharika atatumia rasilimali za serikali ikiwemo usalama wakati wa harusi yake ambayo wanasema bado ni gharama kwa serikali.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top